Jinsi nilivyopata milioni 70 kwa mwaka mmoja

Jinsi nilivyopata milioni 70 kwa mwaka mmoja

Mamujay

Senior Member
Joined
Dec 24, 2022
Posts
149
Reaction score
348
Haloo

Niliingia mjini juzi juzi tu hapo

Nilisikia Kuna eneo Lina utata, linatakiwa na muwekezaji kwa muda mrefu Ila hawajafika muafaka na wananchi. Mzee nikajirisk nikanunua tu maeneo baada ya kuona watu wanauza kwa bei nafuu, hii ni baada ya kuona muwekezaji hakuwa na mashiko kwenye sababu zake.

Basi mwaka 2021 Feb 15 nikahamia eneo ilo baada ya kujenga chumba changu Cha slope. Nilipokuwa pale nikajenga vyumba 5 vya slope vingine nikaweka wapangaji, muwekezaji, ameshindwa kesi eneo likabaki Mali yetu, akataka eneo Basi tukajadiliana kuwa kias Cha mil 70 ndio nitanyanyuka.

Eneo nilinunua mil 3 nyumba nimejenga kwa Kama mil 10 hivi maana eneo Hilo lina full mchanga na bati niliweka used mwaka unaanza tu 2023 nikapewa zangu mil 70.

Bahati hii sio kwasababu nina akili Sana hapana Ni Mungu kanipatia neema yake maana nimeokoka na nimezadharaulika Sana saizi Kila nilisikia sehem ina mgogoro naenda kuuliza marambili mbili.

Maisha hayana fomula .
Nimehangaika Sana kutafuta kazi, nna diploma ya civil engineering nimefanya Sana interview utumishi Sekretarieti ya Ajira pale Kigamboni Ila nilikosaga
 
Mambo ya viwanja ni bahati tu.

Sio biashara nyepesi kuotea kama wewe ulivyootea
 
Hiyo 70m ila elekea juu Au ndio kila siku ina pungua elfu moja moja, mwaka ukiisha una elfu kumi kutoka 70m
 
Kwahiyo we tayari umekua tajiri au milionire ghafra, sasa mtihani uko kwenye kutunza na kuzalisha hiyo pesa baada ya miaka miwili uwe na 140m.

Ila unekosea sanaa tena kuingia kwenye upuuzi wa kuokoka, hizo pesa zinaenda kupigwa na wachungaji vizuri na utarudi pale pale.
 
Ukiwa mlevi, mcheza kamali, mtu wa mademu hutoboi mwaka utarudi JF hapa kukumbushia nyuzi za KATAA NDOA
 
Back
Top Bottom