Jinsi nilivyotapeliwa Kariakoo mwaka 2012 (True Story)

Jinsi nilivyotapeliwa Kariakoo mwaka 2012 (True Story)

Ukiingia kumi na nane za wakulungwa huna bahati...nahisi jamaa wana dawa za kupumbaza si bure
 
Pole sana,.mi kuibiwa ilikua hapo Morocco hoteli migo.
Nilipigwa roba ya mbao enzi hizo na na majanki wa3.
Hela nilikua nazo dola,za kibongo na pamba kali,kuna saa ya mjerumani gorenthe nilipewa zawadi tu.
Thamani yake ilikua zaidi ya milioni 2 miaka hiyo.
Waliiba vyote.
Sasa katika kuuza saa mwizi connection kaletwa kwangu tena,
Aniuzie
Na saa ni yangu.
Kumbe hawakujua sie tulikua wastaafu tu wa matukio.
Tulipomkamata yule janki na ile saa baasi.
Tulitambaa nae na kupata kichapo mpaka atuonyeshe wenzie.
Hapo mi nataka hela zangu.
Tukawavamia chimbo lao hao hapo.
Sijui hata siku hiyo tulifanya nini.
Hela hatukupata ila walikiona cha moto.
 
Du, ulikuwa kama wazee wa kijijini. Ku-set bass mpaka urudishe dukani? Umenikumbusha miaka ya nyuma mjomba alikuwa na zile redio cassette za zamani hizo. Nyumba nzima hakuna aliyekuwa anaweza kuitumia isipokuwa yeye.
Jamaa mvivu kusoma manual, mvivu kubeba radio, ilikuwa anaalika kupigwa yeye mwenyewe kwa uvivu wake.
 
Mi niliibiwa Mwenge mwaka 2010 sa 4 usiku kipindi hicho daladala za kwenda Mbezi-Tegeta ikifika sa 12 jioni ni mtihani kuzipata ko sometimes daladala za route nyingine zinaua hizo route zao zinashika route ya kwenda Tegeta. Sasa ikitokea daladala imefika hilo vurumai kuwahi seat ni balaa. Makonda wa daladala nao walikua wanahusika sana kwenye hii michezo michafu.

Toka hapo sijawahi kuibiwa tena
 
Hapo kariakoo kila mtu akileta true story yake nazani kila baada ya sekunde story my change JF itashindwa kusomwa kwa true stroy
 
Njia sahihi ya kutembea Kariakoo ni kuwa serious sana, na usiongee na watu hovyo hovyo.
Hii ndo njia yenyewe sasa,usifanye mazoea na mtu yoyote kkoo kama humjui hata wale wauza mifuko sio wa kuwaamini.pale kkoo kuna watu kazi yao kuchora watu ili wawaibie
 
Uzuri wa kkoo mwizi hakurupuki kukuibia anakusoma kwanza. Na anachokiangalia kwanza mapepe yako, ushamba, kushangaa kwako nk
 
Back
Top Bottom