pbwmasanja
Member
- Mar 20, 2013
- 5
- 7
UTANGULIZI
Watu walio wengi kwa sababu moja au nyingine huwa hawawezi kutengeneza fursa za biashara kutokana na kuanza kwa biashara moja kupitia Mnyororo wa Thamani. Fuatilia Makala hii kwa makini uone jinsi unavyoweza kufanya hivyo kwa biashara yoyote.
Mnamo mwaka 2019 nilianzisha na kusajili kampuni binafsi ya huduma za ulinzi kwa malengo yafuatayo:
Wanahisa wa kampuni hii tupo watatu ambao ni mimi, rafiki yangu mmoja na kampuni nyingine ambayo wanahisa wake ni mimi na watoto wangu wawili. Ile kampuni ya mimi na watoto wangu watatu ndiyo yeye hisa nyingi ambazo ni 550 kati ya 850 ambazo zimegawiwa. Mimi na rafiki yangu kila mmoja anazo hisa 150 tu. Wakurugenzi wa kampuni hii tupo wawili mimi na rafiki yangu. Wakati kwenye ile kampuni ya mimi na watoto wangu ambapo mimi na mtoto mmoja ni wakurugenzi, mimi ninazo hisa 60 kati ya hisa 80 zilizogawiwa, na hao watoto wangu wawili wanazo hisa 10 kila mmoja.
BIASHARA YENYEWE
Usajili na Kibali
Baada ya kupata usajili wa BRELA utaratibu wa Jeshi la Polisi unataka kampuni husika ipate kibali cha Inspekta Jenerali wa Polisi cha kufanya shughuli za ulinzi katika mkoa au mikoa husika ukiwemo mkoa mmoja ambao ndiyo makao makuu ya kampuni. Sisi tulipata kibali cha kwanza kwa mkoa wa Geita ambao ndiyo makao makuu ya kampuni. Baada ya kama miezi miwili tangu kuanza kutoa huduma tulipata kibali cha mkoa wa Mwanza, Dodoma, Dar Es Salaam na Pwani.
Wateja na Askari
Kwenye sekta hii ya ulinzi wale waliozoeleka kuitwa walinzi hujulikana kama askari na kimsingi ni askari. Hadi kufikia Julai 2020 tulikuwa na wateja katika mikoa hiyo mitano (5) na askari waasiopungua 250. Lengo letu hadi kufikia 2025 tuwe na askari 1,000. Wateja ni wale watu binafsi, maofisi, makampuni, biashara na taasisi tunazozipatia huduma yetu ya ulinzi. Askari ni wale wafanyakazi (walinzi) wetu wanaotoa huduma ya moja kwa moja ya ulinzi kwa wateja wetu.
Ada za Huduma Zetu za Ulinzi
Ada zetu tunazolipwa na wateja wetu kwa wastani kwa huduma ya ulinzi kwa mwezi mmoja ni 250,000/= kwa askari mmoja asiye na silaha.
Mshahara wa Askari Wetu na Matumizi Yake
Mshahara tunaolipa kwa askari wetu kwa wastani kwa kazi ya ulinzi kwa mwezi mmoja ni 120,000/= tu.
Mshahara huu wa askari hutumika kwa ajili ya kukidhi mahitaji mhimu kama kununua chakula, kulipa pango la nyumba, na matibabu.
Changamoto za Huduma za Ulinzi
Utafiti wangu umenionyesha kuwa changamoto za pamoja kwa makampuni madogo madogo binafsi ya ulinzi ni hizi zifuatazo:
Matokeo ya kucheleweshwa kwa mshahaara hupelekea askari kukopakopa kwenye maduka ya mahitaji ya chakula, kuchelewa kulipa pango la nyumba kwa wenye nyumba, kukosa pesa ya kulipia dharura za ugonjwa na nyinginezo. Ikumbukwe kuwa ajira hii ndiyo dhamana ya kuaminika kwa askari hawa.
Suuhisho la Changamoto kuwa Fursa ya Biashara
Kwa kuwa kampuni haina mtaji wa kutosha kulipa mshahara kwa wakati bila kutegemea malipo ya wateja mimi binafsi kama mmoja wa wanahisa mkuu na mkurugenzi nilizichukulia changamoto hizi kama fursa ya kibiashara kama ifuatavyo:
Kwangu mimi nimeweza kutengeneza soko la wateja wapatao 250 kwa kila bidhaa ambapo naweza kuuza kwa mfano tu walau kilo 30 za mchelle na kilo 30 za unga kwa wateja 250 wa uakika kila mwezi (kilo 7,500 za mchele na kilo 7,500 unga). Fanya hivi kwa bidhaa nyingine. Kwa kifupi kiasi chote cha mshahara (120,000/=) ambacho ni kipato cha uhakika nakichukua chote kwa njia ya kuuza bidhaa zangu huku nikitatua changamoto zao na za kampuni.
Nafikiri kama umefuatilia vema utaona jinsi nilivyotengeneza soko la kuaminika ambalo haliwezi kuingiliwa na mshindani yeyote. Kwangu wafanyakazi ni wateja wangu. wakuu
Tuwe wabunifu. Ukihitaji ubunifu wa wazo la biashara lenye kuweza kuwa na Mnyororo wa Thamani tuwasiiane 0715771677.

- Kutoa huduma ya ulinzi nchini Tanzania;
- Kutengeneza fursa za ajira kwa watanzania hasa vijana;
- Kuboresha hali ya maisha ya wafanyakazi kwa kuwalipa mshahara;
- Kampuni kujipatia mapato kutokana na utoaji wa huduma ya ulinzi kwa wateja wake;
- Kuchangia pato la taifa kwa kulipa kodi kwa serikali kutokana na mapato ya kampuni na mapato ya wafanyakazi.
Wanahisa wa kampuni hii tupo watatu ambao ni mimi, rafiki yangu mmoja na kampuni nyingine ambayo wanahisa wake ni mimi na watoto wangu wawili. Ile kampuni ya mimi na watoto wangu watatu ndiyo yeye hisa nyingi ambazo ni 550 kati ya 850 ambazo zimegawiwa. Mimi na rafiki yangu kila mmoja anazo hisa 150 tu. Wakurugenzi wa kampuni hii tupo wawili mimi na rafiki yangu. Wakati kwenye ile kampuni ya mimi na watoto wangu ambapo mimi na mtoto mmoja ni wakurugenzi, mimi ninazo hisa 60 kati ya hisa 80 zilizogawiwa, na hao watoto wangu wawili wanazo hisa 10 kila mmoja.
BIASHARA YENYEWE
Usajili na Kibali
Baada ya kupata usajili wa BRELA utaratibu wa Jeshi la Polisi unataka kampuni husika ipate kibali cha Inspekta Jenerali wa Polisi cha kufanya shughuli za ulinzi katika mkoa au mikoa husika ukiwemo mkoa mmoja ambao ndiyo makao makuu ya kampuni. Sisi tulipata kibali cha kwanza kwa mkoa wa Geita ambao ndiyo makao makuu ya kampuni. Baada ya kama miezi miwili tangu kuanza kutoa huduma tulipata kibali cha mkoa wa Mwanza, Dodoma, Dar Es Salaam na Pwani.
Wateja na Askari
Kwenye sekta hii ya ulinzi wale waliozoeleka kuitwa walinzi hujulikana kama askari na kimsingi ni askari. Hadi kufikia Julai 2020 tulikuwa na wateja katika mikoa hiyo mitano (5) na askari waasiopungua 250. Lengo letu hadi kufikia 2025 tuwe na askari 1,000. Wateja ni wale watu binafsi, maofisi, makampuni, biashara na taasisi tunazozipatia huduma yetu ya ulinzi. Askari ni wale wafanyakazi (walinzi) wetu wanaotoa huduma ya moja kwa moja ya ulinzi kwa wateja wetu.
Ada za Huduma Zetu za Ulinzi
Ada zetu tunazolipwa na wateja wetu kwa wastani kwa huduma ya ulinzi kwa mwezi mmoja ni 250,000/= kwa askari mmoja asiye na silaha.
Mshahara wa Askari Wetu na Matumizi Yake
Mshahara tunaolipa kwa askari wetu kwa wastani kwa kazi ya ulinzi kwa mwezi mmoja ni 120,000/= tu.
Mshahara huu wa askari hutumika kwa ajili ya kukidhi mahitaji mhimu kama kununua chakula, kulipa pango la nyumba, na matibabu.
Changamoto za Huduma za Ulinzi
Utafiti wangu umenionyesha kuwa changamoto za pamoja kwa makampuni madogo madogo binafsi ya ulinzi ni hizi zifuatazo:
- Mtaji mdogo kwa makampuni mengi madogo madogo;
- Wateja kutokulipa ada zao kwa wakati ndani ya mwezi;
- Askari kucheleweshewa kulipwa mshahara yao kwa wakati.
Matokeo ya kucheleweshwa kwa mshahaara hupelekea askari kukopakopa kwenye maduka ya mahitaji ya chakula, kuchelewa kulipa pango la nyumba kwa wenye nyumba, kukosa pesa ya kulipia dharura za ugonjwa na nyinginezo. Ikumbukwe kuwa ajira hii ndiyo dhamana ya kuaminika kwa askari hawa.
Suuhisho la Changamoto kuwa Fursa ya Biashara
Kwa kuwa kampuni haina mtaji wa kutosha kulipa mshahara kwa wakati bila kutegemea malipo ya wateja mimi binafsi kama mmoja wa wanahisa mkuu na mkurugenzi nilizichukulia changamoto hizi kama fursa ya kibiashara kama ifuatavyo:
- Nimeanzisha maduka ya bidhaa za chakula kama mchele, unga, maharage, sukari, mafuta, chumvi, na kadhalika popote walipo askari wetu ambapo nawakopesha kimkakati na kwa umakini ili wakati kampuni inalipa mshahara madeni yao yakatwe moja kwa moja kulipia bidhaa walizokopa; katika hitaji hili mahitaji ya askari mmoja kwa wastani ni 70,000/= kwa mwezi; hii inawapunguzia usumbufu wa kudaiwa ovyo mtaani;
- Nimeanzisha maduka ya dawa muhimu za binadamu ambapo askari wanakopa kwa ajili yao na famiia kama inavyofanyika kwenye mahitaji ya Chakula; katika hitaji hili askari hukopa kwa wastani wa 10,000/= kwa mwezi;
- Kuna huduma ya vinywaji na viburudisho pia ambapo askari hutumia wastani wa 10,000/== kwa mwezi;
- Nimeanzisha huduma ya mikopo midogo midogo ya fedha ambapo kwa mahitaji ya fedha taslimu askari wanakopeshwa kwa wastani wa 30,000/= na kurejesha kwa riba ya 10% kwa mwezi na pesa hii nayo hukatwa kutoka kwenye mshahara wa mwezi husika;
- Natarajia kuanza kutoa huduma ya nyumba za kupangisha kwa askari popote walipo ili kuwaondolea kero ya kusumbuliwa na wenye nyumba kwa malipo ya kila baada ya miezi mitatu au sita kwa mkupuo ambapo kwangu watakuwa wanalipa kila mwezi kwa njia ya kukatwa kwenye mshahara kwa wastani wa 20,000/= kwa mwezi.

Upvote
8