Jinsi nilivyothibitisha Uchawi, hutoamini nakwambia!

Mimi nmekujibu wewe,
Jibu wewe kama wewe ambaye unapinga uwepo wa maswala ya uchawi, Simama wewe kama wewe

Yeye pia atasimama yeye kama yeye.
Naam! Kama umefuatilia comments zangu kwenye mada hii ni wazi kwamba mimi sikubaliani na wala siamini Uchawi upo. Kwa muktadha wa hoja yako nisimame mm kama mm ni kwamba hapa unaunda aina fulani ya viscous circle kwa maana yupo i.e. wewe anayedai Uchawi upo lakini hawezi kuthibitisha kuwepo kwa uchawi ila anawaelekeza wapinzani wa hoja hiyo eti waende kwa ghara zao mikoa mbalimbali wakajithibitishie. i.e. wewe umejivua jukumu hilo. Waliokwenda huko kunakodaiwa wapo wabobobezi wa fani hiyo wamerudisha mrejesho kwamba hawakuona lolote bado unai-narrow down hoja kwamba ni mtu binafsi ndo aende. Dah! Ni mpaka waende wangapi? Wewe bro nakukubali. Una akili sana kwamba sasa unachomokaje hapo. Eti kila mmoja asimame yeye binafsi. Wewe umejikalia zako pale kwa mangi unakunywa soda.
 
😅 kumbuka lengo ni kupata uthibitisho, Mimi natamani wewe ujionee wewe mwenyewe

Sijahitaji nijikite kwenye mabishano kwasababu hatuwezi kufikia tamati,

Haya mambo ni magumu mno yanahitaji ushuhuda wa mtu binafsi, That's why sio rahisi kuelewa/kuwaelewa watu ambao wameshudia mambo kama haya

Binafsi yangu nlikua siamini kama ilivyo wewe kwa miaka mingi tu, Lakini kwa sasa imekua tofauti ( Hapa wala sitahitaji kuelezea kipi kilifanya nikatambua kuwa haya mambo yapo )
 
Ina maana nyinyi mnaopinga ndio mpo sahihi sana ? Kwanini yeye umemuamini haraka haraka kuwa hakuona

Ila mtu mwingine akileta kisa chake namna alivyoshuhudia jambo la ajabu unampinga

Why ?
Simpingi kwa maana ya kukataa tuu just like that, bali ninahoji ili niweze kubaini authenticty ya hoja yake ili nijiridhishe kama kuna ukweli wowote.
Je, ingekuwa ni wewe ungekubali tuu kichwa-kichwa? Bila shaka ungejiuliza maswali mengi na pengine ungetaka kupata uthibitisho au sio.
Sasa kama uthibitisho haupatikani inakuwaje? au unaambiwa eti uende huko ww binafsi.
 
Umebarikiwa ww uliyepata bahati hiyo adimu ya kuthibitisha uwepo wa Uchawi.
Nasubiri labda zamu yangu itakuja. Lakini mpaka sasa naamini HAUPO Uchawi.
 
Eeh aisee ndani ya sec watu hawapo😆
 
Hatare.
Kuna wale jogoo anarushiwa punje za mchele.

Anakula then anachinjwa zinahesabiwa kafara zipo za aina nyingi Sana..

Ila watu ni wabishi Sana hasa hasa wabongo walio MAJUU.

Una umri gani? You must be as dumb as a brick.
 

UDSM hapo wakiongozwa na Dr. Richard Sambaiga walifanya utafiti juu ya ushirikina TZ nzima wakaishia kuhitimisha hakuna uthibitisho. Tafuta andika lao.

Mtu kufanya matambiko, kuandika, kusema, kuamini kama uchawi upo hakufanyi uchawi wenyewe kuwepo. Unaweza amini wewe ni paka hakufanyi wewe kuwa paka kweli.

Ukitoa story za kijinga za hearsay sijui nani alifanya hivi au vile na imani za kijinga uchawi haupo. Hakuna mtu hata mmoja atakuonyesha ushirikina zaidi ya kutoa excuses laki1. Tumeomba humu turogwe mwaka wa 10 sasa ni excuses tu, huwezi kuona mtu anapaa au anatokea ukutani hata siku moja maisha yako yote zaidi ya kulishana upuuuzi tu.
 
Wajuaji watakwambua unaota au una malaria plus bin plus.
 
Kwa mifano yako ya mtu kupaa na kutokea ukutani,

Pengine mimi na wewe tuna uelewa tofauti kuhusu maana ya neno "uchawi"
 
Kwa mifano yako ya mtu kupaa na kutokea ukutani,

Pengine mimi na wewe tuna uelewa tofauti kuhusu maana ya neno "uchawi"
Woy! Bufa amekupeleka mpaka kwenye Tafiti zilizofanyika hapa hapa Bongo na matokeo yake i.e. walivyohitimisha utafiti wao. Sasa unageukia kutafuta malumbano na makubaliano ya maana ya neno "Uchawi." Ndo zenu hizo - hakuna Uchawi ila kuna kutishana-tishana kwa kitu ambacho HAKIPO narudia tena; HAKIPO.
 
Yani mimi nliyeshuhudia mambo ya kichawi wazi wazi, Leo hii nkasome tafiti ya mtu mwingine ili kuelewa madai yako wewe ambaye hauamini

Nadhani ntakua ni mtu nsiye na akili timamu au ambae siamini utimamu wangu wa akili

Na sitakua tofauti na wazee wetu wa zamani ambao walibeba wazungu kuwapeleka ( mfano mlima kilimanjaro ) ili wakaugundue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…