Jinsi nilivyothibitisha Uchawi, hutoamini nakwambia!

I had this experience....

Nyumba yetu ilikuwa iko karibu na bahari ... wakati wa usiku mwingi ninapenda kupanda balcony ghorofani kuvuta fegi.....mbele ya uzio wa nyumba ni barabara kubwa ,niliona washkaji wawili wamesimamisha pikipiki (250 XLR)...pembeni yao kulikuwa na demu wanamuongelesha....mara nikaona pikipiki imeondolewa kasi huku yule aliyekuwa ameshuka chini kuongea na Cutie akamdandia mwenzake mgongoni wkt pikipiki inaondoka hapo....nikawa ninamuangalia yule demu na barabarani taa zilikuwa ni kali tu ....ghafla demu akapotea...ilihali pembeni yake kulikuwa na kuta za nyumba pande zote....nilitupa kichungi nikakimbilia chumbani kujifunika mashuka....

Hizo mbanga zipo wakuu....
 
Hili tukio bado halitoshi kusema kuwa umemshuhudia mchawi. Bado haileti picha ya muujiza wa kichawi kwa haya matukio umesema hapa.

Na sijui kwanini unahusisha kifo cha huyo jirani na tukio la kuona hicho unachosema umeona? Na sijui kwanini umeita 'kupambania naye' wakati uliona tu na ukakimbilia ndani.

Labda kuna maelezo umesahau kuyaeleza hapa. Yaani kwa kukabwa koo lako sauti isisikike ndiyo uwe umepambana na mchawi hadi akafa? Kweli?

Na kiukweli tukio la kukabwa koo lako lilifanya nihisi ulikuwa kwenye ndoto ndefu ukadhani ni tukio halisi baada ya kuzinduka usingizi.

Ova
 
Nice !
 
Huamini kama Kuna uchawi?

Kuamini is one thing to show proof is another. Hakuna proof ya uchawi mahala popote pale zaid ya hearsay stories kama yako zinazosimuliwa na kuaminiwa na watu wajinga.

Kuna watu wanaamini wao ni mbwa, wengine wanaamini wao ni malaika na wengine mizimu. Mimi naamini nimewahi kwenda zanzibar kwa mguu toka DSM, mimi binafsi naamini na nataka na wewe uniamini. Ukiwa zwazwa utaamini.
 
Una vituko sana, nimechekaaaa.

Sijasoma hata post ya jamaa ila hii reply yako imenifanya nicheke kila aya!
 
Mwaka 2012 nilikuwa na geto chumba changu kipo usawa wa barabarani. Siku moja nimelala nikasikia sauti ya mkwaruzo kule barabarani wa ile watu kama wanafagia nikajiuliza inamaana ndio kumekucha?
chap nikainuka kuchukua sim niangalie saa nikakuta ni saa nane dk mbili nikajiuliza nani anafagia sasa muda huu? nikainuka kuelekea upande wa dirisha nikafunua pazia..
aisee nilichokishuhudia macho hayakuamin mpaka leo!
niliona watu wanafagia barabarani kilichonishangaza ni kwamba watu wanafagia barabarani halafu namna ya mjongeo wao wanatembea kinyume nyume!
niliwaza sana nini nakiona ama naota nikafikicha macho kuona vizuri.. ni watoto wamama na wanaume wachache kilikuwa kama kikundi cha watu zaidi ya 10 wanafagia wanatembea kinyume nyume kwenda kuzoa taka.
nikasema ngoja niende sebleni nicheki kwa engo nyingine.. nhee! si nikajigonga kwenye mavyombo nikasikia pametulia tulii! kwenda kufungua pazia nione tena nakuta peupe hamna mtu yani ndan za sekunde chache watu wamepotea. nikalala zangu huku nimejawa na hofu
 
Watu hawaamini kama uchawi upo mara nyingi nasema watu wenye mapepo wakiombewa kanisani na kupiga Yale makelele sio wajinga it's real na ni uthibitisho wa nguvu za giza
 
Unataka ku prove uchawi upo?
 
Tatizo uliparamia karai la vyombo 🤣🤣
 
N
Ngoja baadae nita andika Uzi mwingine apa wa jamaa yangu mmoja alikutana na jini porini
 

Mkuu upo vizuri sana kwa UTUNZI unafaa kuwaandikia bongo movie story.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…