Ilikuwa usiku wa manane, hapo nimelala ghorofa ya 4 jengo (naliweka kapuni, mtaa (nauweka kapuni) lakini ni mkoa wa dar es salaam......
Wakani nimelala ghafla nikashtuka, nikawa kama nauwoga flani hivi... nikawa najiuliza mbona natetemeka hivi... ikabidi nijigeuze upande wa pili... nikaona kama kivuli cha jitu ukutani.. dooh! Moyo ukapiga paah! Si unaelewa hofu tena,, nilitulia hivyo kama nilivyo geuka nikajifanya nimelala, lakini nimefumbua macho kwa mbaali huku naomba kwa imani yangu... hapo nipo stand by nikiona sielewi nitoke speed... wakati naendelea kuomba (wakati naomba kuna muda maneno yalikuwa hayatoki aiseh) lakini nilikaza, baadae nikaona kama lile jitu linaelekea chooni... daah! Asubuhi yake nikasema hii nyumba sikai... sikukaa sana.. nikaondoka.