Jinsi nilivyotibika Bells Palsy/Facial Paralysis (Uso kupooza upande mmoja)

Jinsi nilivyotibika Bells Palsy/Facial Paralysis (Uso kupooza upande mmoja)

Beige

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2022
Posts
234
Reaction score
515
Hello all,

Ninapenda kushare nanyi nilivyotibika tatizo la uso kupooza. Ninafanya hivi kumsaidia mtu yeyote ikitokea amekutana na changamoto kama hii.

Niligundua wakati naswaki usiku najaribu kusukutua mdomo unagoma hauna uwezo wa kuhold maji mdomoni nikapata panick attack moja ya heshima. Ikabidi nitulie nijaribu kuona shida ni nini. Najiangalia kwa kioo nafunga macho, jicho moja halifungi kabisa, najaribu kusmile mdomo unavutwa upande mmoja ndio nikagundua kuna shida.

Nikaenda hosp the next day daktari nliyemkuta hakuelewa hata shida nini akaishia kunipima pressure akaona iko normal (110/70) akaniambia tu ntakuwa sawa bt sikuwa sawa nikazama kwa akili mnemba nikampa symptoms nikapata mwanga. Nikarudi to a different hospital bahati nzuri nikakutana na daktari aliyekuwa anatutibu toka utotoni ndio akaniambia nina hiyo Facial Paralysis na Symptoms zote za Bells Palsy nlikua nazo and zikawa mbaya zaidi kila panapokucha.

Symptoms zenyewe:
• Maumivu makali 😫 behind your ear(ule upande ulioopooza)
• Jicho halifungi na linalia 24/7 upande huo huo huwezi kukonyeza wala nini 😜
• Huo upande ulioopoza unahamia upande mwingine (sanasana mdomo)
• Maumivu around the jaw sijui jaw inaitwaje ila maumivu yakueleweka yanakua hapo pamoja na mild headache
• Unakua sensitive na sauti kubwa yani sauti kubwa ni kama mtu anakutoboa huko sikioni
• Kula ni kazi 🤦🏽‍♀️Na nlikua nakula na kijiko cha chai. Ukifungua mdomo kula haufunguki wote and you make funny sounds while eating. Hii ilikua inanidisturb sana nikawa nangoja watu wote wale ndio nile mwenyewe out of embarrassment.

Treatment:
Nilitumia Corticosteroids, multivitamin tabs, massage oil na painkillers kama ifuatavyo:
• Prednisone 60mg per day kwa siku 5 halafu a five-day taper.
• Multivitamin
• Piroxicam twice a day (asubuhi na jioni)
• Castor Oil (Hii Castor Oil sikuandikiwa na Dokta niliisumbua sana chatgpt wee mpaka ikanipa hii recipe ambayo ilisifiwa sana. Niliichanganya castor oil na Rosemary & Karafuu kisha nikawa nachemsha maji ya mchaichai yakishachemka na kuwa na ile rangi ya kijani, ninadumbukiza ile chupa ya mafuta yapate moto kidodo kisha nikawa na massage uso hasa ule upande baada ya kumassage nikawa nafanya warm compress kwa kutumia kitambaa cha towel nakiweka kwenye yale maji moto kisha nakanda uso kuamsha misuli for 20minutes) Maji unakua makini usiungue uso. Pia wakati nikikanda uso nilikua nikisema this simple prayer throughout (Lord Jesus trail wide the hem of your garment, bring healing, bring peace)

Baada ya wiki 3 nikaanza kuona tremendous changes, nikawa naskia uso unacheza (unafeel kama unatekenyeka) kila dakika kumbe ndio nilikua naelekea kupona mpaka imegonga tar 6 Dec i had almost regained all of my facial expressions. Nliweza kucheka tena, kuswaki bila shida, kula bila shida, kukonyeza 😉 na yale maumivu yamekwisha.
Ninamshukuru Mungu sana sana maana nilikosa amani kabisa. Ugonjwa wowote kawaida unakosesha amani.

P.s
Tafadhali elewa nimeshare my personal experience incase umekutana na changamoto hii angalau uelewe unadeal na nini na unaanzia wapi. There's no one-size-fits-all treatment na watu twatofautiana. Wengine inawachukua mpaka mwaka kupona kabisa, wengine wiki 1 tu na wengine kama mimi mwezi. Tafadhali nenda hospital nina hakika your healthcare professional may suggest medicines or physical therapy to help speed your recovery.
 
Back
Top Bottom