Jinsi ninavyopata Faida ya 45,000/= kwa siku, huku nikiendelea na kazi zangu kila siku

Nimerudia kusoma bandiko lako mara ya pili. Kama kweli unafanya hii biashara hongera Sana Ila kama umeanzisha thread ili uone wengine watasema nini ndio ukafanye maamuzi, nakushauri kua makini Sana. Hakuna linaloshindikana.
Mkuu nina mwaka sasa katika hili gemu, hapa inaonesha ni idadi ya pikipiki 15 kwa watu tofauti na hizo nyingine zinaingia january. Nimeweka viambatanisho hesabu zilianza December 2021View attachment 2459125


View attachment 2459142
 
Unanunua pikipiki mil 2.3 halafu kwa siku inakuingizia aftatu 3000 biashara kichaa hiyo.
Halafu umeshahau service kubwa ni juu ya bosi
Tangia nimenunua pikipiki sijawai kufanya service mimi hata siku moja, service ni juu ya dereva mwenyewe ndio mkataba unavyosena iwe service ndogo au kubwa ni juu yake.

Biashara zipo nyingi mkuu, ningeweza kutafuta kazi nyingine ya kufanya kwa hiyo 2.3m ila hapo mm nina kazi yangu, ninachofanya ni kuizungusha hela iingie kwenye mzunguko nipate faida kuliko hizo hela zingekaa benki tuu.

Kingine ukiwa na pikipiki moja huwezi kuona faida kabsa, utaipenda hii business ukiwa na pikipiki zaidi ya 5 maana kwa pikipiki 5 tu utapata faida ya 15,000 per day na 450,000 per month na hapo unaendelea kuchukua salary yako ya mwezì kama kawaidaa.
 
mb
ona hiyo excell siioni naona piki piki tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…