Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uliibiwaje mkuu?Hii kazi niliifanya kwa mafanikio makubwa sana nikaibiwq kama pipki 4 nikaachana nayo ila sasa nataka nirudie nimepitia mkataba wako upo bora sana nimeusave mwez5 natoa chombo
Hongera. Huo uzoefu nao ni pesa. Mi nakushauru huo uzoefu ukusanye nukta kwa nukta kila siku baada ya miaka mitano andika kitabu.Jinsi mimi ninavyopata faida ya 45,000 kwa siku.
Kwasasa nina pikipiki aina ya Fekon na Huoniao jumla zote zipo 15 mtaani kwa mkataba wa miezi 12. Nilianza na mtaji wa 8,300,000/= mwaka Jana November 2021 ambao ulinisaidia kununua pikipiki 3 mpya aina ya Fekon na baada ya hapo nikawa naongeza pikipiki nyingine kwa marejesho ya pikipiki nilizonazo na hela kidogo kutoka kwenye mshahara wangu.
AINA ZA PIKIPIKI:
Kwa nini hizi pikipiki ni kwasababu ya aina ya eneo ambapo mimi nipo, kiuhalisia ni kwamba Boxer huku nilipo hazifai kwasababu ya barabara zilizopo sio rafiki. Boxer inahitaji barabara tambarare ambayo haina mabonde mengi maana ni rahisi kuharibika tofauti na Fekoni, Huoniao, Sinoray, Haojue etc
BEI ZA PIKIPIKI NA FAIDA ZAKE:
Fekon ni mkataba wa miezi 12, inauzwa 2.3m na kwa miezi 12 yaani mwaka mzima napata jumla ya 3.6 millions kwa maana hiyo faida yangu ni 1.3 millions kwa mwaka mzima (miezi 12) na kwa mwezi napata faida ya 108,000/= gawanya kwa siku 30 kwa siku kwa pikipiki moja ni faida ya 3,600/=.
Huoniao nafanya kwa mkataba wa miezi 11, inauzwa 2.1 millions na kwa miezi 11 nitapata jumla 3.3 millions kwa maana hiyo faida yangu ni 1.2 millions kwa miezi 11 tuu, na kwa mwezi mmoja napata faida ya 100,000/= gawanya kwa siku 30 kwa pikipiki moja ni faida ya 3,300/=
Kiufupi ni kwamba pikipiki moja inazalisha faida ya 3,000/= kwa siku hivyo kwa pikipiki zangu 15 kwa siku moja napata faida ya zaidi ya 45,000/= yaani (3,000/= x 15). Na kwa mwezi mmoja pekee napata Faida ya pikipiki 15 sio chini ya 1,350,000/=.
MAREJESHO:
Marejesho ya pikipiki moja kwa siku ni 10,000/= kwa hiyo kwa pikipiki 15 kwa siku nakusanya 150,000/= na kwa mwezi nakusanya jumla ya 4,500,000/= kwa pikipiki zote 15.
Kiufupi nina kazi yangu, so kwa mwezi kwa marejesho ya pikipiki nilizonazo nina uwezo wa kuongeza pikipiki mpya 2 kwa kila mwezi. Kwa maana hiyo kwa mwaka mzima nina uwezo wa kufunga pikipiki mpya 24 huku faida inaongezeka na makusanyo ya kila mwezi na siku yanaongezeka.
Faida ya pikipiki moja ni milioni moja na kuendelea inategemea wewe na dereva wako mtakubaliana vipi kuhusu mkataba wenu. Kuna sehemu nyingine mkataba wa pikipiki ni miezi 10, kwingine miezi 11 na wengine mpka miezi 13 hapa ni makubaliano ya pande mbili.
Hapa natumia tu mshahara wangu kiasi na 10% ya makusanyo naweza nikaweka kama akiba pembeni.
CHANGAMOTO:
Changamoto zipo nyingi kwenye bodaboda hasa kwa vijana kushindwa kurudisha hesabu ya siku lakini ukiweka mkataba vizuri na ukikaza hamna kinatoshindikana. Kingine ni kuwa na maelewano mazuri na madereva wako maana sio kila dereva anauwezo wa kupata elfu 10 kwa siku so kuna maelewano binafsi yafanyike.
MKATABA:
Mkataba wa pikipiki lazima uwe mkali usainiwe na pande zote mbili, kuwe na sehemu ya mashuhuda wa pande mbili na lazima usainiwe na mwenyekiti wa kijiji pamoja na mwanasheria wa serikali.
Kukata tamaa sio suruhisho dereva asipotoa hela kwa siku kadhaa unaongea nae kwa maelewano ya kurudisha tarehe fulani, weka MFUMO mzuri wa Microsoft Excel ambao utakuwa unaonyesha hela ya kila dereva iliyoingia na hela ambayo ipo nje anayodaiwa. Lazima Excel yako iwe na Formula ambayo itafanya majumuisho ya hela zinazoingia na kutoka kwa madereva wote wakiwa wengi bila ya hivyo utakosea mahesabu yako.
KUPATA VIJANA WAAMINIFU:
Mtafute mtu sahihi ambaye yupo uraiani unayemuamini awe anakusaidia kutafuta vijana waaminifu na ambao wana pikipiki zao walizomaliza mkataba. Kuna madereva wakongwe katika kila sehemu ambaye umezoeana naye mueleze na yeye atakusaidia kucontrol pikipiki zote na madereva wako maana yeye anajua wanapoishi na maisha yao kiujumla.
Vijana waaminifu wapo ila tu hamna ambaye ni mkamilifu zaidi asikose hela kwa siku fulani. Sio kwamba kila dereva muaminifu wa pikipiki ana uwezo wa kupata hiyo hela elfu 10 kila siku hapana.
ONYO:
Usimpe pikipiki, kijana ambaye anategemea pikipiki moja kurudisha 10,000/= kwa siku. Jaribu kutafuta vijana wenye pikipiki zao walizomaliza mkataba uwape wakuletee hesabu maana na yeye pikipiki yake atampa mtu mwingine kama DEWAKA ambapo yeye atapewa 7,000/= kwenye pikipiki yake na yeye atatafuta 3,000/= kwenye pikipiki yake mpya ya mkataba ili ajazie ifike 10,000/= kwa siku kama hesabu ya boss. Bila hivyo utafeli katika hii biashara
Usimpe pikipiki ndugu yako au rafiki yako eti kwasababu tu amekwambia atakupa hiyo hela 10,000/= kila siku. Hawa hawaaminiki utashindwa hata kusaini nae mkataba, usikubali undugu au urafiki kwenye biashara. Hauwezi kumpeleka rafiki yako mahakamani au polisi so kataa undugu katika kazi. Tafuta mtu ambaye utamuweza katika hizi biashara.
MAELEWANO BAADA YA MKATABA KUISHA:
Nina mwaka mmoja sasa kwenye hii biashara, dereva akimaliza mkataba wake na ana deni unauwezo wa kumuongezea siku kadhaa mbele za kumaliza deni lake.
Biashara sio vita kwamba dereva asipomaliza deni basi unampokonya tu pikipiki. Kama ameweza kulipa 3 millions na ana deni la 300k kwann usi pe siku kadhaa amalize hata kama ni mwezi mmoja tu.
Mnaelewana kama ana deni unamuongezea miezi miwili pamoja na riba ya 20% mpaka 40% ya deni lake. Ni maelewano ya pande mbili.
RIBA YA KUMUONGEZEA MUDA WA KUMALIZA DENI LAKE:
Mfano kama dereva alikuwa anadaiwa 300,000/= baada ya mkataba wake kuisha mnaongea kwa makubaliano yenu, unaweza ukamuongezea miezi 2 mbele kwa riba ya 30% ambayo itamfanya alipe tena 390,000/= kwa miezi miwili inayofuata. Ambayo hapo wewe utakuwa na faida nyingine ya 90,000/= kwa miezi inayofuata.
[emoji281]Pikipiki ya kwanza kabsa mnamo November 2021.
[emoji837]Kwenye comments chini nimeweka Microsoft Excel inayoonyesha jinsi pikipiki zote ninavyozifanyia mahesabu kwa excel kuweka kumbukumbu sawa pamoja na majina ya madereva wote. Utaona mpaka sasahivi wapo 15 na 16,17.... etc ni mwezi unaofata January 2023
Blessed [emoji120]Afisa masoko. Safi sana
Unakubaliana nae tu mfano kwa unaweza ukamlipa kila mwisho wa mwezi au kwenye kila rejesho unampa fungu lake kdgo la usumbufu wa kuwafata watu kwa ajili ya makusanyo.ipo good naitaji kujua uyo anaesimamia hizo boda mkataba wake upoje hasa kwenye malipo
Hizi biashara ni rahisi mtu akikusimuliaNilinunua pikipiki aisee nilipata marejesho mara 2 tu wiki ya kwanza 50,000 ya pili 42,000 baada ya hapo dogo white akawa hapokei simu zangu kumfatilia mdhamini wake ambae ni mjomba wangu wakasema pikipiki ilishikwa na watu wa jiji na me nilkua mkoani ndo ikawa nitolee mpaka wa leo, madereva ni changamoto sana
Ukimpa mtu pikipiki tafuta ostadhi aje asomee albadili mbele ya kijana wa pikipiki atakuw na nidhamu ya wogaNilinunua pikipiki aisee nilipata marejesho mara 2 tu wiki ya kwanza 50,000 ya pili 42,000 baada ya hapo dogo white akawa hapokei simu zangu kumfatilia mdhamini wake ambae ni mjomba wangu wakasema pikipiki ilishikwa na watu wa jiji na me nilkua mkoani ndo ikawa nitolee mpaka wa leo, madereva ni changamoto sana
Ni shida mkuu, kupata mtu muaminifu kazi kweli kweli na usirogwe ukampa ndugu yako utatafta lawama bure tu. Me nilimpa cousin wangu gari afanye bolt mbona niliichukua nikaingia front mwenyewe kuangalia kweli hela haipatikani 😂 mtu wiki 3 mfululizo anakupanga tu hata havielewekiUkimpa mtu pikipiki tafuta ostadhi aje asomee albadili mbele ya kijana wa pikipiki atakuw na nidhamu ya woga
Ninazo pia sema dereva wengine heshima sana dereva wangu mmoja ndio shida
Ukitaka kuwa boss trust me unatakiwa uwe na roho mbaya sana. Hawa jamaa ukiishi nao kirafiki hawana jema hata kidogo. Leo tu nimeona jamaa wangu wa bodaboda anakanyagia break anateleza nikajikuta tu nacheka🤣Ni shida mkuu, kupata mtu muaminifu kazi kweli kweli na usirogwe ukampa ndugu yako utatafta lawama bure tu. Me nilimpa cousin wangu gari afanye bolt mbona niliichukua nikaingia front mwenyewe kuangalia kweli hela haipatikani 😂 mtu wiki 3 mfululizo anakupanga tu hata havieleweki
Me nmeshakata tamaa bro nimelizwa sana biashara tofauti tofauti coz sina muda wa kuzifatilia nategemea uaminifu wao tu..sahivi najipanga nipate mtaj mkubwaa niachane na ajira kwa mara ya pili nisimamie mwenyeweUkitaka kuwa boss trust me unatakiwa uwe na roho mbaya sana. Hawa jamaa ukiishi nao kirafiki hawana jema hata kidogo. Leo tu nimeona jamaa wangu wa bodaboda anakanyagia break anateleza nikajikuta tu nacheka🤣
Ukipata vijana waaminifu kazi nzuri sana. Nakomaa nazo kibishi sana alafu number zote D mpya nyepe😊
Kuna kipindi sikutaka kukaa dukani au nifungue duka nikatafuta wana watatu nikawa najaz maduka yao mali faida tunagawana nusu na vitu vya electronic imagine prices ziko juu. Nilipoteza about 6m.Me nmeshakata tamaa bro nimelizwa sana biashara tofauti tofauti coz sina muda wa kuzifatilia nategemea uaminifu wao tu..sahivi najipanga nipate mtaj mkubwaa niachane na ajira kwa mara ya pili nisimamie mwenyewe
Nakusoma vizuri mkuu ukipoteza pesa hiyo hasira unakua nayo sio poa, ndo mana ukawa villain ubaya ubaya tuu 😂Kuna kipindi sikutaka kukaa dukani au nifungue duka nikatafuta wana watatu nikawa najaz maduka yao mali faida tunagawana nusu na vitu vya electronic imagine prices ziko juu. Nilipoteza about 6m.
sasa yeyote anayecheza na kazi yangu sina masikhara nae nishapoteza sana. Nina hasira mda wote 😡
Kuna watu wana roho za uharibifu usipoangalia wanakuharibia sana. I am super villain, master of the minionsNakusoma vizuri mkuu ukipoteza pesa hiyo hasira unakua nayo sio poa, ndo mana ukawa villain ubaya ubaya tuu 😂
ipo good mungu atusaidie vijana tufike ulipofika asante kwa ku share nasi siri ya Mafanikio nchi inakuitaji mtu kama weweUnakubaliana nae tu mfano kwa unaweza ukamlipa kila mwisho wa mwezi au kwenye kila rejesho unampa fungu lake kdgo la usumbufu wa kuwafata watu kwa ajili ya makusanyo.
Kwa mwezi unaweza kumpa 5pK mpka 100K hapo katikati mtaelewana tu au kwenye kila rejesho unampa hela ya mafuta kidogo between 10K mpaka 25K ni maelewano tu hizi ni biashara usimuumize sana maana wewe boss unapata faida kubwa na hausumbuki sana kwasababu yeye ndio Master mind wa kukusanya marejesho yote maana anafahamiana vzuri na hao watu wote uliowapa pikipiki.