Jinsi nywila (password) zilivyookoa maisha ya ndugu yangu.

Jinsi nywila (password) zilivyookoa maisha ya ndugu yangu.

dimaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
4,174
Reaction score
5,658
Habari zenu viongozi,


Kila kitu kina faida yake na hasara.


Ni katika tukio lililotokea juzi, katika maeneo ya kipawa, majira ya saa nne asubuhi.

Ni katika majukumu ya kila siku, ya kutafuta kipato cha hahali alikuwa akitokea. Baada ya kuvuka barabara ya kwanza kuelekea ya pili na kukutana na dhahma ya kugongwa na pikipiki ikitokea upande wa uwanja wa ndege kuelekea tazara.

Hakika alikuwa amepata majeha makubwa sana.


Wasamaria wema walivoiona simu yake yake na kuichukua, kizuri katika simu yake alikuwa hajaweka mywila (passwords) wakawapigia ndugu kutoa taarifa ya hiyo ajali.


Wakamkimbiza hospitali ya temeke , kibaya zaidi hakupatiwa matibabu wakidai pesa ya matibabu, huku mgonjwa akiwa katika hali tete, bahati nzuri ndugu walifika ndo wakalipia hiyo pesa kwa matibabu zaidi.

Je bila kuwatafuta ndudu zake ni nani angeilipa ile pesa?, na ni kwasababu ya kutokuweka nywila katika simu yake.

Watu tunatumia nywila kwakuhifadhia simu zetu kutokana na udokozi mbalimbali, ambao hufanya documenti zetu ziwe salama zaidi.

Ila kama siku za kufa mtu bado ni bado.

Alikiri kamwe hatoweka nywila katika simu yake kabisa .

Fundisho; tukumbuke faida za nywila (passwords) na hasara zake.



Nawasilisha.
 
Hizi Lugha Eti "Nywila"
Kiswahili Chenga Ung'eng'e Chenga
Daah Kaazi Kweli.
 
Ni ujumbe mzuri, japo hujasema kama:

1. NDUGU YETU ALIKUWA NA SIMU AINA GANI...??

2. AMEOA/ AMEOLEWA au HAJAOA/ HAJAOLEWA..!!

3. UMRI wake na ISSUES zake kwa ujumla.

Hayo ni mambo muhimu ktk suala zima la password. Kama alikuwa na kitochi hapo sawa...!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku ikitokea jamaa alikuwa mafuta kwenye pikipik akala mzinga akazimia na simu yake alikuwa ameweka so called nywila
Ila wale waungwa walitoa line wakaweka kwa simu nyingine na msaada wa taarifa ulipatika kwa kuchek namba ambazo ni familiar

Ahsante nywila!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila kitu kina faida na hasara . Nimeacha sim yangu mezani kazini haina password basi kuna bint kachukua kaanza kucheki x aka forward kwa dada na group letu la dini wakanitoa mda huo huo nilichoka. Nikakumbuka kuweka nywila kila wakati

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom