Jinsi Profesa Lipumba alivyowatosa CUF na UKAWA kumnusuru rafiki yake Ramadhani Dau asifungwe jela na Hayati Magufuli

Jinsi Profesa Lipumba alivyowatosa CUF na UKAWA kumnusuru rafiki yake Ramadhani Dau asifungwe jela na Hayati Magufuli

pesa za walipakodi kufujwa au kupigwa kwenye hii nchi ni kawaida. na bado zitapigwa sana kwenye miradi mingine kwasababu ya kujuana au kubebana.

watu wanaoneana haya kwasababu wa kumshughulikia mwenzie nae ana yake machafu ya ufujaji wa fedha na ufisadi.
 
Wafanyakazi wa umma wateseka wakistafu kisa DR Slaa , prof Lipumba na DR Dau
 
Mapato ya hili Taifa kama yangekua yanatumika ipasavyo kimaendeleo aisee Bongo ingekua kama ulaya, ila ndo hivo tena Ngozi nyeusi......
 
Namalizia kisa cha mwisho cha visa na mikasa vya Hayati JPM.

Vikao vya CCM baada ya kumpitisha JPM kuna wana CCM waliofurahi ila wanaomjua vizuri walijua kumekucha, walijua magereza yatajaa watendaji wakiboronga na mafisadi.

Mmoja kati ya watu waliokosa usingizi ni mtoto wa mjini ila msomi Dkt. Ramadhani Dau.

Akiwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF alianzisha miradi mikubwa iliyotafuna Matrilioni ya michango ya wananchi.

Leo nitaongelea mradi wa Dege Eco village wa Kigamboni ambao una thamani ya mabilioni yalivyoishia mifukoni mwa viongozi wa NSSF na wanasiasa wakubwa walioko na wasioko serikalini.

Sasa basi jina la JPM limeshapitishwa, korido za Lumumba hazikaliki vikao usiku na mchana, upepo wa Lowassa na Ukawa unawatetenesha. Timu ya kampeni ya CCM wanawaza jinsi ya kushindana ba Ukawa chini ya Edward Lowassa aliyejiunga nao baada ya jina lake kukatwa.

Chama cha CUF chini ya Prof Lipumba nacho kimeungana na timu ya ukawa, sasa timu imesheheni,huku kuna Lowassa,Lipumba na Dk Slaa,
CCM mambo sio mepesi.

Timu ya kampeni ya CCM inaazimia mambo mengi ila kubwa ni kuusambaratisha umoja wa Ukawa kabla ya kampeni, Dkt. Slaa na Prof Lipumba wanatakiwa kutoka ndani ya UKAWA kwa gharama yoyote.

Nani wa kumvaa Lipumba, nani wakumvaa Dkt. Slaa ili wajitoe Ukawa?

Taarifa zinamfikia mtoto wa mjini Ramadhani Dau kupitia kwa kigogo mmoja ndani ya CCM, Dau anawafuata Kinana na Nape na kuwaeleza kuwa ana uwezo wa kumtoa Lipumba Ukawa ila kwa masharti.

Anaomba akutanishwe na hayati JPM mgombea wa CCM kumuomba amlinde atakapoingia madarakani endapo atamtoa Lipumba UKAWA.

JPM anapewa taarifa na wanakubaliana hilo kuwa akimtoa Lipumba Ukawa atamlinda.

Siku hiyohiyo saa mbili usiku Dkt. Dau anaendesha mwenyewe VX V8 nyeusi, anawasili Mbezi Beach nyumbani kwa Prof Lipumba akiwa na uso wa wasiwasi macho mekundu, anamueleza Prof Lipumba akumbuke urafiki wao na kumtaarifu kitu kimoja.

Anamwambia kama yuko tayari kumuona akifia jela au ajitoe Ukawa. Anamtaarifu kuhusu madudu ndani ya NSSF ambayo aliyafanya kwa maelekezo toka juu lakini yatampeleka jela, anamfahamisha makubaliano yake na mgombea wa CCM.

Lipumba anampigia simu Kinana kuthibitisha habari hizo anajibiwa kuwa ni kweli, na yeye anaakikishiwa fursa nzuri baada ya uchaguzi akikubali kujitoa Ukawa.

Kesho yake tarehe 6 August 2015 Lipumba anatangaza kujiondoa Ukawa na kuacha taharuki upinzani, one man down!

Bado mtu mmoja Dkt Wilbroad Slaa nani wa kumtoa Slaa Ukawa,?
Msafara wa magari ya vigogo wa CCM unawasili Kurasini yalipo makazi ya Askofu Pengo.

Pengo anampigia simu Dk Slaa wanaongea kwa Dk kadhaa tarehe 25 Sept Dkt. Slaa anajiondoa Ukawa,

Niwakumbushe ndugu wasomaji kama mnakumbuka Dkt. Slaa aliwahi kuwa Padri wa Kanisa Katoliki, lakini alijiondoa na kuamua kuingia maisha ya ndoa,mpaka leo sielewi kiapo cha upadri huwa wanaapa vitu gani,
Mapadri wengi wakijitoa kwenye daraja la upadri iwe kwa njia yoyote ile bado watakuwa watiifu kwa kanisa.

Dkt. Slaa bado alikuwa akiwaheshimu sana viongozi wa kanisa katoliki bila shaka ndio maana baada ya kupokea simu ya kardinali Pengo hakuleta ubishi.

Mfano mwingine ni padri Privatus Karugendo, huyu alitofautiana na Askofu wake Severin Niwemugizi wa jimbo la Rulenge Ngara akajitoa upadri na kumuoa Dkt. Rose lakini usingemsikia akilisema vibaya kanisa katoliki. Alikuwa bado na mahusiano mazuri na kanisa katoliki,hata alipofariki mwaka jana,ibada ya mazishi kanisani Segerea na makaburini Kinondoni iliongozwa na mapadri watatu na walikuwa wakimuaddress kana marehemu Padri Karugendo. Once a priest,always a priest.

Haya turudi Ukawa, sasa Ukawa ukawa ukiwa, Ukawa bila Dkt Slaa,ukawa bila Prof Lipumba,Ukawa na Lowassa pekee.

October 2015
Uchaguzi mkuu unafanyika mgombea wa CCM anaibuka kidedea.

26 Aptil 2016
CAG Prof Mussa Assad rafiki mwingine wa Prof Lipumba na Dkt. Dau, anatoa ripoti bungeni.

Ripoti inaonyesha ufisadi na udanganyifu wa hali ya juu NSSF
Mradi wa Dege Eco village chini ya NSSF na kampuni ya Azimio Holding
Mradi unaonyesha kutumia ekari 20,000 lakini ripori inaonyesha ekari 3500 tu.

Ripoti ya CAG inaendelea kuonesha kuwa ekari moja ilinunuliwa kwa sh milioni 800 badala ya milion 8.
Mradi wote una thamani ya dola milioni 350 zaidi ya bilioni 780 hautekelezeki
Kumbuka huu ndio ufisadi mkubwa kuwahi kutokea nchini

Mkataba wa Richmond ulikuwa USD 172M ,EPA USD 133M ,Esrow USD 130 M. Dege Eco village USD 350 M.

Baada ya ripoti hiyo wakurugenzi sita wa NSSF walisimamishwa kazi kupisha uchunguzi.

Ikumbukwe wiki moja kabla ya ripoti ya CAG yaani tarehe 19 April, Rais Magufuli alizindua daraja la Kigamboni lililojengwa na NSSF na kuwasifia Dau na Mfugale

Kabla hatujakaa sawa Ramadhani Dau na Dkt Slaa wakapewa zawadi ya ubalozi kwa kazi nzuri.

Lipumba akarudishiwa chama chake cha CUF kwa kazi nzuri ya kujiondoa Ukawa.

Askofu Pengo akaakikishiwa maslahi ya Kanisa Katoliki kulindwa.

Haya yote yakifanyika Zitto Kabwe yuko nyumbani kwake Masaki akitazama Luninga akila popcorn.

Zitto akiwa mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya mashirika ya Umma hakuwahi kutamja lolote kuhusu ufisadi wa muda mrefu wa NSSF.

Zitto kabla ya kuhamia Masaki ameishi sana kwenye flats zilizojengwa na Nssf zilizoko Tabata Magengeni, alimuacha mama yake humo mpaka umauti unamkuta.

JPM alikufa akiwa na Sonona kuhusu ufisadi huu maana mwaka 2018 alitamka bayana kuwa ulikuwa mradi wa ovyo na ya kwamba NSSF wajitafakari maana serikali inahamia Dodoma, hakuhitajiki huo mradi kwa Dar es Salaam.

Mwezi November 2022 mradi huu wa wa mabilioni unauzwa baada ya kuona hautekelezeki.

Mnasema Yanga wanatoa bahasha kwa waamuzi?huu mradi umetembeza bahasha kwa wahariri na waandishi wa habari na wanasiasa haijawahi kutokea.
Mkuu kwa kusoma nyuzi zako naweza sema wewe ni mtu wa kitengo au unaukaribu na watu hao au mwanasiasa mkubwa hapa tz.

Sisi wengine acha tujisomee kwa ajili ya kumbukumbu tu ila kuna watu wanaramba asali hasa jamani..
 
Magufuli alikuwa shetani siyo mtetezi wa wanyonge
Natamani kauli kama hizi zipigwe marufuku kwa sababu zinakera sana. Huwezi muita majina hayo mtu ambaye alijitoa kwa watanzania kuwatumikia kwa moyo wa kizalendo. Tunaamini nyie mnaompakazia na kumuita majina ya ajabu siku za vifo vyenu mtakumbuka na kutubu. Poleni sana. Dkt Magufuli ataendelea kuwa the best president kwa nchi yetu. Mungu aipe pumziko la amani roho yake. Na kauli zenu ndizo zinafanya Rais Samia chukiwe sana na watanzania.
 
Nakubaliana na wewe kabisa sababu niliwahi kufanya kazi kwenye miradi ya ujenzi ya nssf ya Dr dau na kushuhudia jinsi pesa zilivyokuwa zikipigwa kwenye miradi mbalimbali ya ujenzi. Kitu ambacho hukukisema au hujui, baadhi ya pesa ya ufisadi ilikuwa ikipelekwa CCM kwa ajili ya kampeni za uchaguzi nk.

Nilishangaa nilipoona Magufuli aliyekuwa akijitanabahisha kama mpiga vita ufisadi akifumbia macho ufisadi wa Dr dau. Sasa nimepata picha kamili na ndio maana wakurugenzi waliosimamishwa kazi kesi zao ziliisha kimya kimya sababu hakuna namna ambavyo wangeweza kutenganishwa na Dr dau
Dau aliibiwa mamilioni ya shilingi na walinzi wa nyumba ambayo alikuwa haishi nadhani hiyo nyumba aliifanya benki ndogo. Kuna mzee mdau humu rafiki yake Dau alimtetea sana rafiki yake humu wakati wasomaji walipokuwa wanamshutumu Dr Dau kwa uwizi, tokea alipokuwa bandari na kuhamia NSSF, ajabu pamoja na tuhuma zote hizo akateuliwa balozi wetu huko Malaysia
 
na walikuwa wakimuaddress kana marehemu Padri Karugendo. Once a priest,always a priest.
I don't know about all that "once a priest always a priest" everything. Na sijawahi kusikia mtu anamwita Dr. Slaa Father Slaa, sijui huyo Karugendo.

Yani jitu limekimbia upadri, limeoa, limezaa, limekufa kama raia huru, halafu wamuite Marehemu Father Karugendo ?? Weka video ya mazishi!

WIKIPEDIA

In the canon law of the Catholic Church, the loss of clerical state, commonly referred to as laicization, dismissal, defrocking, is the removal of a bishop, priest, or deacon from the status of being a member of the clergy.

Catholic cleric may voluntarily request to be removed from the clerical state for a grave, personal reason. Voluntary requests were, believed to be by far the most common means of this loss, and most common within this category was the intention to marry

A laicized cleric loses rights to such things as clerical garb and titles such as "Father".
 
MIMI ningekubali tu,nikishinda nawageuka Rasmi!!

Siwezi kubali hongo ya kizembe kama Hiyo!
Kwasababu ,2015 Lowasa angeshinda KWA kura hata kama Mbowe angehamia CCM!

Dola pekee Ndio ushindi KWA Marais wote Wala Sio kura!!


Kama Hayo ni kweli,mi ningewaambia live nikiingia ikulu TU,NATAKA hizo usd 350 millions ziwemo KWENYE akaunti ya SERIKALI Ili zikawahudumie WANANCHI!!

Pole Sana jpm,walikuumiza mno kwa kwenda kinyume na dhamira yako!!
 
Elewa ndugu kuna kuteuliwa na kupangiwa kituo cha cha kazi yeye aliteiliwa mwezi December na kupangiwa nchi ya kwenda ilikuwa tarehe hiyo.elewa
Najua hilo, lakini nadhani mleta hoja yuko sahihi akisema aliteuliwa April 2016. Magufuli hata baraza la mawaziri alichelewa sana kulitaja iweje mabalozi awateule Desemba?

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Nakubaliana na wewe kabisa sababu niliwahi kufanya kazi kwenye miradi ya ujenzi ya nssf ya Dr dau na kushuhudia jinsi pesa zilivyokuwa zikipigwa kwenye miradi mbalimbali ya ujenzi. Kitu ambacho hukukisema au hujui, baadhi ya pesa ya ufisadi ilikuwa ikipelekwa CCM kwa ajili ya kampeni za uchaguzi nk.

Nilishangaa nilipoona Magufuli aliyekuwa akijitanabahisha kama mpiga vita ufisadi akifumbia macho ufisadi wa Dr dau. Sasa nimepata picha kamili na ndio maana wakurugenzi waliosimamishwa kazi kesi zao ziliisha kimya kimya sababu hakuna namna ambavyo wangeweza kutenganishwa na Dr dau
Hayati naye hakuwa mpiga vita ufisadi kwa dhati hususan pale ufisadi ulipoelekea kumnufaisha yeye!
 
Huo ndio ukweli,Dau alitakiwa kuwa segerea lakini yuko ubalozini
Nachoshukuru Mungu hii mijizi na MITAPELI mingi ya Chama Cha Mambuzi imeshazeeka na Itakufa punde kwa magonjwa mengi waliyonayo miilini
 
Back
Top Bottom