Jinsi Semina na Makongamano yalivyobadili Mitazamo ya Vijana.

Singidan

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2015
Posts
881
Reaction score
942
Habari Wakuu!
Kila kona, kila mtaa na viunga vingi ambavyo ndani mwake kuna changanyikeni ya watu, habari ni ujasiliamali. Vijana wengi wamebadilika na kuamua kufanya biashara flani ili kujiingizia kipato.

Hali hii ni tofauti na miaka ya 2009 kurudi nyuma ambapo UJASILIAMALI ilikuwa kitu cha kigumu sana na wengi waliwaza ni kina Bakhresa, Dewjn n. wengine ndiyo wanaweza. Hii ni matokeo chanya ya semina na makongamano ya ujasiliamali ambayo yamekuwa yakifanyika mara kwa mara.

Watu wengi walilala sana, brain feeders wamesaidia mno, shuhuda za safari za ujasiliamali zemeboost minds za vijana wengi. Sasa, kila alieyehamasika na events hzo nae anawaza namna ya kujiajiri.

Kwa kweli, Bila SEMINA NA MAKONGANO YA UJASILIAMALI nadhani kundi kubwa la vijana lingekuwa bado halijitambui kuhusiana na self emloyment.
 
Waliowengi wanaoandaa hayo makongamano sio Mfano wa kuigwa!
Mtu anaandaa Kwasababu ana uwezo Mkubwa wa kuongea sana ila sio utendaji......

Wengi wao wanasoma vitabu vya akina kiyosaki Ndio wanakuja kukusanya vijana Na kuwaibia viingilio!

Ukiwa msomaji wa vitabu vya mbele hawa mamotivational speaker wa bongo kuwasikiliza utaona kichefu chefu
 
[emoji122][emoji122][emoji122]
 
mkuu Ngushi upo sahihi, lakini Wengi ni wavivu wa kusoma vitabu!
Wenzetu huwa wana kitu tunaita appreciation!
Mpe credit mwenye kazi yake!

Unafaidika nini mtu kusoma kwa kiyosaki au wengine halafu uje uwasimulie as if wewe ndiye unayefanya hicho kitu?

Wengi wanahubiri biashara fulani inalipa na anatiririka vizuri tu, Kumbe hajawahi hata kumiliki banda la chipsi!
Ila mifano Na maelezo vyote amekopy huko.....
Na anatoza watu elfu 20!
Ukija kwa waandishi wa vitabu hivyo vya kuhamasisha ujasiriamali ndio kichekesho kabisa!

anyway endeleeni kuwachuna za viingilio hao wavivu wa kusoma vitabu
 
Aisee pamoja na kuchunmwa lakini nahisi kuna hawatoki kapa! Kwa upande mwengine kuna kundi flan limekuwa lenye kazi yake n kuhudhuria tu, lakni hawabadilili zaidi ya ufahar na kupost vipicha wakiwa na kina Shigongo. Vile vile pia, kutokumiliki vibanda hakuwanyimi fursa ya wao kupitisha na kuwaonyesha wengine fursa.
 
. Vile vile pia, kutokumiliki vibanda hakuwanyimi fursa ya wao kupitisha na kuwaonyesha wengine fursa.
Hiki kitu ndio kinafanya vijana waone kama kwenda kwenye hizo workshop za kuhamasishana kama hakuna utofauti na kwenda kwenye vijiwe vya kahawa!
Tujifunze kuhamasisha kile ambacho sisi wenyewe tunakifanya!
Sio kuhubiri faida na changamoto za matikiti maji kwa kusoma kwenye vitabu
 
Waliowengi wanaoandaa hayo makongamano sio Mfano wa kuigwa!
Mtu anaandaa Kwasababu ana uwezo Mkubwa wa kuongea sana ila sio utendaji......

Wengi wao wanasoma vitabu vya akina kiyosaki Ndio wanakuja kukusanya vijana Na kuwaibia viingilio!

Ukiwa msomaji wa vitabu vya mbele hawa mamotivational speaker wa bongo kuwasikiliza utaona kichefu chefu
Word! [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Back
Top Bottom