Innngassaco
New Member
- Aug 30, 2021
- 2
- 2
Utangulizi
Ndugu zangu wanajamii forum ningependa kuanza na nini maana ya Afya ? Ni hali ya kujiskia vizuri kimwili, kiakili, kiroho na kiutu bila kusumbuliwa na ugonjwa wowote. Katika Afya kuna aina zake Nazo ni Afya ya akili, Afya ya mwili, Afya ya jamii, kijinsia, chakula, mazingira, Umma na kiuchumi.
Zifuatazo ni baadhi ya maelezo ya aina za Afya
*Afya ya akili ni pamoja na ustawi wetu wa kihemko, kisaikolojia na jamii. Kukosekana Kwa afya ya akili husababisha magonjwa ya akili ambayo huathiri ubongo na humfanya mtu kuwa na hisia, fikira na matendo tofauti na Yale yanayotarajiwa.
*Afya ya mwili
Ni hali ambayo mtu anakuwa na Afya njema na uwezo wa mwili kujitegemea na hii inasababishwa na kufanya mazoezi.
*Afya ya jamii
Ni kigezo katika Afya ya Umma ambayo inajihusisha na Afya na ubora wa jamii.
*Afya ya mazingira
Ni shamba la afya la umma linaloangalia na kushughulikia mambo hayo ya kimwili, kemikali na kibayolojia ambayo hatuwezi kuwa na udhibiti wa moja Kwa moja lakini inaweza kuathiri Afya yetu.
Ni njia gani zinaweza kutufanya kupata Afya bora, zifuatazo ni kanuni bora za Afya;
(i)Lishe bora
Hapa tunaangalia mlo au chakula mtu anapaswa kula ambapo mtu ataitaji kula mlo kamili unaojumuisha angalau makundi mengi ya chakula ikiwezekana yote
(ii)Hewa safi
Ili mtu awe na afya bora hewa safi inahitajika ambapo hewa hiyo inatokana na mazingira safi.Chanzo kikuu cha hewa safi ni miti na mimea ya asili ambayo inatakiwa kutunzwa ili kusaidia katika kutengeneza hewa safi.
(iii) Mazoezi
Ili binadamu awe na Afya njema mazoezi ni muhimu katika kujenga na kuuweka mwili katika hali nzuri.
(iv)Kuepuka kutumia pombe kupita kiasi na sigara
(v)Kupumzika
Vilevile ili mtu awe na Afya bora mwili unahitaji kupumzika ili kuruhusu akili ya binadamu kutulia ambapo mtu atahitajika kupumzika angalau Kwa Masaa kuanzia 5 mpaka 8.
+Lakini kiujumla serikali inalojukumu kubwa kuwashauri wananchi wake kuhusu Afya japo kua katika sekta ya Afya bado kuna changamoto nyingi ambazo zinaweza kuwa Ndio sababu ya kuiludisha nyuma sekta ya Afya kwa jamii. Zifuatazo ni changamoto zinazoikumba sekta ya Afya ;
1.Upungufu wa vituo vya kutolea huduma za Afya, Japo serikali inajitahidi sana kujenga hospitali na Zahanati mjini na vijijini.
2. Upungufu wa watoa huduma za Afya katika vituo mbalimbali. Hili ni tatizo kubwa sana linaloikumba sekta ya Afya kwani serikali huajiri watoa huduma wengi lakini hawakizi mahitaji ya vituo vya kutolea huduma nchini.
3. Upungufu wa vifaa vya kutolea huduma za Afya pamoja na madawa. Hili ni tatizo jingine ambapo wagonjwa wanapoenda kupata huduma hukutana na upungufu wa vifaa au madawa hivyo kupelekea kwenda kupata iyo huduma seheme nyingine au hospitali Kwa gharama kubwa .
4.Ukosefu wa utoaji wa elimu ya kutosha kuhusu Afya Kwa jamii, Apa tukiangalia mfano utoaji wa elimu ya kuhusu chanjo ya uviko 19 watu bado hawajapewa elimu ya kutosha kuanzia umuhimu wa kuchanja , faida ya kuchanja na ni madhara yapi unaweza kupata usipochanjwa chanjo.
5.Mazoezi ya ufanyaji kazi Kwa wahudumu wa Afya. Hapa unakuta mtoa huduma yuko bize na shughuli zingine ambazo zipo nje na majukumu yake ya kazi.
Zifuatazo ni vitu ambavyo serikali inabidi izifanye ili kuimarisha sekta ya Afya Kwa wananchi wake;
1. Kuongeza utoaji wa elimu ya Afya Kwa wanajamii. Hapa serikali inabidi ihamasishe wanajamii mambo mbalimbali kuhusu afya mfano ni jinsi gani mtu anaweza kujikinga na magonjwa na jinsi gani wanaweza kuimarisha mwili Kwa kuzingatia Milo bora.
2. Kuwepo na ukaguzi wa Mara Kwa Mara Kwa wafanyakazi au watoa huduma za Afya ili kuongeza umakini na ufanisi katika utendaji kazi
3.Kuhakikisha kila mtoa huduma za Afya anafanya kazi sake kuendana na kitu alichosomea mfano Mfamasia kwenye madawa na wahudumu wengineo.
4. Kuongeza au kuajiri watoa huduma katika vituo vya huduma hii itasaidia katika utendaji kazi na vilevile huduma bora Kwa wananchi katika muda muafaka.
5. Kuhakikisha uwepo wa vifaa na madawa katika vituo vya Afya, hii itakua ni bora sana maana wagonjwa wanaofika kwenye vituo vya Afya kwaajili ya kupata huduma watatimiziwa kulingana na mahitaji ya matatizo yao au magonjwa.
Hitimisho
Serikali ili kuboresha huduma za Afya au sekta ya Afya inatakiwa kuzingatia sana katika utoaji wa elimu maana hii ndo nguzo kuu Kwa wanajamii hasa katika televisheni, redioni, mitaani na hata mashuleni.
Elimu ya Afya inaweza kutolewa katika nyanja mbalimbali za aina za Afya lakini Mimi nitaangalia katika Afya bora hasahasa katika lishe bora ni vitu gani mtu anaweza kupata asipopata lishe bora navyo ni ;
Mwisho kabisa naomba kura yako usisite kunipigia kura

- Kuongezeka Kwa magonjwa kama vile ,madonda ya tumbo, shinikizo la damu, saratani(Kansa) na Utapiamlo.
- Vilevile mtu anaweza kujikuta anakoswa ; Hamu ya kula, Uchovu wa Mara Kwa Mara na kuharisha.

Upvote
1