OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Tukiwa katika kupigania katiba mpya nimejikuta natafakari jinsi serikali ya Magufuli ilivyoichezea katiba ya nchi. Hii ni sababu tosha tunahitaji katiba mpya ya kuweza kuchukua hatua kali dhidi ya mhujumu wa katiba. Katiba iliyopo imeweka kinga kwa Rais. Kwa nini ajiwekee kinga kama anafanya mambo kwa ajili ya ustawi wa nchi-woga wa nini.
1. Kukataza miradi ya maendeleo majimbo yenye wabunge wapinzani.
2. Kushindwa kulinda haki za kuishi kwa rais wake huku akiruhusu watu kama kina Sabaya na Makonda kufanya watakavyo
3. Kubinya haki ya kujieleza na kutunga sheria kandamizi.
4. Kumuondosha CAG Prof. Assad kwa hila kinyume na katiba
5. Kuingilia mihimili mingine kama Bunge na Mahakama.
6. Kukata shughuli za kisiasa kwa vyama vya upinzani huku CCM wakiendelea na siasa