Jinsi siasa inavyowafaidisha wachache, wengi wakitumikishwa

Jinsi siasa inavyowafaidisha wachache, wengi wakitumikishwa

wilsonwizzo3

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
625
Reaction score
2,704
Ndio, wachache wanafaidika na siasa ya Tanzania na wengi wakiitumikia kwa hasara,
nayasema haya baada ya kujua wenzangu wanatajirika kupitia siasa bila jasho

kumbe watu mnalipwa kupitiaha agenda za wanasiasa na hamsemi?

Ndio, watu manazoa malaki kwa mamilioni ili kupromo agenda za kisiasa.

Nayasema haya ikiwa sina muda mrefu toka nikatae deal la kumsema kiongozi fulani alishafariki.

Sio huyo tu ninmeshakataa deal kibao tu zikiwemo moja ya twitter ya kupush hashtag za katiba mpya, deal ya kushinikiza waziri fulani ajiuzuru et kisa alishawahi kuliongopea taifa na sababu kedekede, deal la kumsifia kiongozi fulani wa ngazi katika nchi.

Deal la kumpromote waziri flani kisa anapunguza athari za kimazingira kwa kuwagawia watu majiko ya gesi, deal la kumsema kiongozi flani wa taasisi ya jeshi flani na mengine mengii

Ukweli nimepata madeal mengi sana ya kisiasa ambayo mengine nimeyakubali na mengine nimeyakataa kwa sababu fulanifulani ila niliyoyakataa ni mengi kuliko niliyo yakubali.

Naandika hapa si kwaajili ya kujisifia bali na nataka niwasanue baadhi yenu ambao hamuelewi haya mambo yanavokuwa ili muache kuchangia hovyohovyo kwa nyuzi za watu;

Ukiona hapa Jf imeanzishwa thread usichangie kwa kukurupuka maana maranyingi hapa watu wapo makazini

ukweli hii tasnia ya siasa inalipa sana hebu fikiri unapushi agenda ya mtu kwa weak moja na hela unalipwa 400,000, muda huohuo unakuta una agenda za watu watatu kwa weak nzima au kila weak unakuta unapushi agenda tu mpaka mwezi unaisha;hizo agenda zote ni pesa zinaingia

either nilikuwa na pasaka chache hapa mjini mpaka nashangaa kulipwa hivi kisa kutetea agenda za watu kwenye mitandao au haya mambo yameanza sahivi!!?

ila tasnia ya siasa inapesa sana,unakuuta mmetengeneza kabisa na group la Whatsapp lenye zaidi ya watu ishirini- arobaini na wote mnapokea kitita bila dhuluma!

kama wapwa tunalipwa hivi vipi kuhusu hao middlemen?

maana hizi kazi bila middlemen huwezi kuzipata, unakuta mwanasiasa anazaidi ya middlemen ishirini na wote wanapewa fungu kwaajili ya kupushi agenda zake na kila middleman anawatu zaidi ya ishirini!!;

Na je vipi kuhusu hao wanaopushiwa agenda zao wanapata mabilioni mangapi?

wanasiasa washawajua watanzania ni keyboard worrior na ndio maana wanamajeshi yao ya kimtandao,ndo maana unakuta hata humu Jf imeanzishishwa thread ya kumsema kiongozi flani halafu kumbe huyo kiongozi anamajeshi yake Sikilizia hayo mashambulizi 😂

vijana msiwe mnarukia hizi thread za kisiasa nyingi hua tunalipwa na hua tunawachora tu mnavyochangiaga ugoro wenu😂😂.

Nimeamua kuwaambia maana najua hamuwezi kunishitukia kwa kuwa nina id yangu nyingine ndo huwa inawafanyiaga mashambulizi

mwanzo nilikuwa nayataa haya madeal yote ila nikaona kwanini nikatae noti wakati ni nchi ya kitumwa hii🤭 nikaona sio kesi wacha nifungue id mpya ili niipe ushwawishi ikubalike na watu halafu nipige pesa..

Tengenezeni ushawishi kwenye id zenu maana ndio sifa ya kuaminiwa na kupewa kazi na hao middlemen ili nanyinyi kwa ambao mpo interested mfaidi mema ya nchi muache kulialia kwenye mitandao


Ahsanteni sana🙏
 
Usisahau wako waandishi wa habari baadhi nao ni waChawa na wanalipwa kuandika yasiyo kweli.
exactly,
sio hao tuu mtu yeyote ukionekana unaushawishi kwenye mitandao ya kijamii hasa Twitter facebook ni vyepesi sana kutumikia watu kisiasa,viongozi walichajua issues za Tanzania hua zinaishia mtandaoni ndo maana wanamwaga sana mapesa kwenye mitandao
 
Back
Top Bottom