Vikwazo, hata avator yako inatosha kuwakilisha hii mada. Nchi yetu inatafunwa sana na hawa wageni, kwa kazi ambazo hata kijana aliyehitimu drs la saba anaweza kuzifanya. Ukifuatilia vibali vyao vya kufanya kazi nchini utakuta ni tofauti kabisa na kazi anayoifanya. Lakini haya yanafanyika kwa kusaidia na Ma-HR kwenye makampuni kwa kuwaita ni wataalam wenye fani zisizo hapa nchini.
Ni aibu na inatia hasira sana, leo hii ukienda kwenye makampuni ya migodi, walinzi na wapelezi wake ni weupe kutoka bondeni. Wagawa vyumba vya kulala ni hao hao. Ukikaa nao ukawauliza hivi inakuwaje mnapata vibali vya kazi hata hizi; wanakujibu "kwenye nchi yenu kama una pesa, kila kitu kinawezekana" Hili jibu mimi huwa linanitia aibu sana. Kuna mmoja anasema wakati anaitwa kuja hapa nchini kufanya kazi anayoifanya, alikuja lakini kwa mashaka sana kwa kuhofia angerudishiwa uwanja wa ndege, kwani alijua kzai hiyo kuna wazawa wanaweza kuifanya. Lakini alistaajabu, hadi leo ana miaka minne anafanya kazi hiyo bila bughudha yoyote.
Kuna hawa wenzetu wa bondeni SA, ni wanyanysaji sana. Lakini ndio viongozi wetu wanawaleta kila siku kama wataalam na wawekezaji. Enzi za nyuma waliitwa makaburu lakini sasa ni wawekezaji. Hivi huwezi kuwekeza, na kazi zikafanywa na wazawa?