SoC02 Jinsi Tanzania inavyoweza kujikwamua kiuchumi licha ya kuwepo kwa changamoto za uchumi zilizosababishwa na UVIKO -19 na vita kati ya Urusi na Ukraine

SoC02 Jinsi Tanzania inavyoweza kujikwamua kiuchumi licha ya kuwepo kwa changamoto za uchumi zilizosababishwa na UVIKO -19 na vita kati ya Urusi na Ukraine

Stories of Change - 2022 Competition

Meck Mwakihaba

New Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathiriwa na janga la UVIKO-19 pamoja na vita kati ya Urusi na Ukraine katika Nyanja ya uchumi wa mtu mmoja mmoja na uchumi wa taifa kwa ujumla. Majanga haya yamesababisha kuwepo kwa mfumuko wa bei za vyakula ,ongezeko katika bei ya mafuta na gesi pia kupungua kwa pato katika utalii na watalii,hii imepelekea gharama za maisha kupanda sana. Pamoja na chamagamoto hizo bado Tanzania imeendelea kutafuta namna ya kujikwamua kiuchumi kwa kutunga sera na sheria zinazoendana na wakati ili kuimarisha uchumi.

Yapo maeneo mengi yanayoweza kuchagiza kupunguza changamoto ya kiuchumi Tanzania licha ya madhara makubwa yatokanayo na UVIKO-19 na vita kati ya Urusi na Ukraine, miongoni mwa hayo ni;

Uwekezaji katika gesi Asilia
Tunaelekea kufunga mwaka mmoja sasa, Tanzania inapitia wakati mgumu wa namna ya kupata nishati ya kutosha kwa bei nafuu.Hii ni kutokana na bei ya mafuta na gesi kupanda ulimwenguini kote ikisababishwa na vita kati ya Urusi na Ukraine ,wakati huo dunia ikitegemea mafuta kwa na gesi kwa wingi kutoka Urusi hii ni kutokana na kwamba Nchi ya Urusi ni ya pili kwa uzalishaji wa wa gesi na bidhaa zote zitokanazo na petroli duniani.Hii ni changamoto, na yaweza kutatuliwa kwa kuweka nguvu ya kutosha katika uwekezaji wa gesi asilia inayo patikana ndani ya nchi hasa maeneo kama Songongo,Mkuranga na Kiliwani ili tuwe na nishati ya kutosheleza.Gasi asilia ni kitu muhimu sana kwenye gridi ya taifa ya kufua umeme kwani hadi kufikia Mei 2022 imechangia asilimia 60.27 sawa na megawati 1021.32.Huku uzalishaji gesi asilia ukiongezeka kwa asilimia 20 pekee hadi Mei 2022 kutokea mwaka 2020/2021 hii ni kutokana na ongezeko la matumizi ya gesi asilia kwenye magari,uzalishaji umeme,majumbani na viwandani.

Nishati itokanayo na maji ambayo kwa sasa imekua ikikabiliwa na changamoto mabaliko ya tabia ya nchi hasa ukame na kupelekea vyanzo vingi vya maji kupungua ujazo au kukakauka kabisa na pia kutegemea petroli na dizeli katika magari,ipo tija sasa kuanza kuona fursa kubwa katika nishati ya gasi asilia kwa matumizi ya magari na kuzalisha umeme kwa kushirikiana na wadau mbali mbali kama sekta binafsi,Benki Kuu ya Dunia na Serikali ya Japan kama inavyoshiriki katika baadhi ya maeneo yenye gesi asilia ili tuweze kujengewa uwezo zaidi kwa kuzalisha gesi asiia kwa maslai mapana ya nchi.

Uwekezaji katika Utalii
Kutokana na janga la UVIKO-19, idadi ya watalii waliongia nchini mwaka 2021 ilifikia 922,692 ambayo ni ndogo ukilinganisha na mwaka 2019 watalii waliongia nchini walikua milioni 1.5 na milioni 1.4 ya mwaka 2018.Pia kwa kipindi cha mwezi Januari 2022 hadi Aprili 2022 idadi ya watalii walioingia nchini ilikua 367,632 tu.

Zipo jitahada mbalimbali zinazoofanywa na serikali inayoongozwa na Mheshimiwa raisi wa Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan kuikwamua sekta ya utalii licha ya kuwa na kikwazo cha janga la UVIKO-19 mfano THE ROYAL TOUR yenye lengo la kuvitangaza kimataifa vivutio vya kitalii nchini pia kuvuta uwekezaji katika sekta utalii lengo likiwa kukuza uchumi na pato la taifa.

Ipo sababu sasa ya mabalozi wanaoiwakilisha nchi ya Tanzania katika nchi zingine duniani kumuunga mkono Mheshimiwa raisi kwa kutangaza vivutio vya kiutalii vya tanzania katika nchi wanazowakilisha.

Ni wakati sasa wa kuona fursa kubwa ya uwekezaji katika sekta ya utalii kwamaana ya kuboresha miundombinu ya utalii ili kuvuta wawekezaji nje na ndani ya nchi kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira na utamaduni wa Kitanzania.Hii itasaidia si kupata watalii wanaokuja na kutalii bali kuwekeza pia.

Uwekezaji katika Kilimo.
Watanzania walio wengi wanategemea kilimo kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.Hii imepelekea Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuongeza bajeti Zaidi ili kukuza uzalishajiji zaidi kutoka bilioni 294 mwaka 2021/2022 mpaka billioni 954 mwaka 2022/2023.Pamoja na jitahada zote zinazo fanyika bado ukujaji wa kilimo uko chini ya asilimia 10 kwasababu njia zinazo tumiwa katika shughuli za kilimo bado si rafiki kwa uzalishaji zaidi kwani Watanzania wengi hawana uwezo wa kutumia njia za kisasa kama umwagiliaji badala yake hutegemea mvua kwaajili ya umwagiliaji jambo ambalo limekua si la uhakika kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Vita kati ya Ukraine na Urusi, janga la UVIKO-19 limechangia pakubwa kupunguza uzalishaji jambo ambalo limepelekea kupanda kwa bei za bidhaa hasa mafuta ya kula.

Ipo sababu sasa ya Tanzania kuona fursa kubwa katika kilimo cha alizeti na michikichi zaidi katika maeneo yanayo ruhusu ulimaji wa mazao hayo,kwa kutoa elimu zaidi Pamoja na amasa ya kilimo cha kisasa,miundombinu ya pamoja baina ya Wakulima, umwagiliaji wa kisasa na kutoa ruzuku katika bei ya mbolea na punguzo la kodi kaika zana za kilimo.

Kuwepo kwa ushirikishwaji wa vijana katika kilimo;
  1. Kwa kutoa elimu juu ya fursa zilizopo kwenye kilimo ili kuondoa dhana ya zamani kwamba kilimo ni cha watu masikini.
  2. Vijana wanaojifunza maswala ya kilimo katika vyuo vikuu na vyuo vya kati wahusishwe katika kupewa maeneo yaliyotengwa na wizara ili wahusike moja kwa moja katika kilimo hasa pale wanapokua katika mafunzo ya vitendo(field) ,waweza kupewa maeneo kama kikundi wakijumuishwa na wananchi wa maeneo husika kwa maana ya kutoa ajira na elimu , pia kuendeleza miradi hii moja kwamoja wanapomaliza masomo yao.Dhana hii imekua na mafanikio makubwa katika makampuni makubwa ya kilimo kama JATU PUBLIC LIMITED COMPANY na Mr.Kuku Farmers Limited.

Ni wakati mzuri sasa wadau wa kilimo kuungana (serikali na sekta binafsi) kujikita katika otoaji elimu na misaada kwa wanachi juu ya kuongeza samani bidhaa zinazotokana na kilimo,kutoa ruzuku na zana za kilimo.

Pia sheria na sera za kilimo ziangaliwe vizuri na kwa upya ili ziwe na lengo la kumkomboa mkulima ,hii itasiadia kuongeza uzalishaji na kuvutia uwekezaji wa kutosha katika kilimo kutoka ndani na nje Tanzania.Kumbuka, uzalishaji unapoongezeka pia bei ya bidhaa hupungua, hii husaidia kupunguza mfumuko wa bei katika bidhaa.

Hitimisho,
Ubunifu ni adui mkubwa kwa watu waliofanya vizuri katika mazingira ya zamani,na rafiki mzuri kwa watu wanaotaka kufanya vizuri katika mazingira mapya na njia mpya.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom