Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,434
Sidhani kama hili ni sahihi; Nyerere hakuwahi kupinga na kusema kuwa sheria zilizotungwa na mkoloni zilikuwa batili; na wala hakusema kuwa baraza la kutunga sheria lilikuwa haramu vile vile. Kuna tofauti ya msingi ya hoja ya Nyerere na watu wanaosema kuwa Muungano ni haramu lakini wakati huo huo wanakubali madaraka waliyonayo yanayotokana na Muungano huo. Mtu hawezi kusema ndoa ni haramu halafu wakati huo huo akataka wagawane mapato ya ndoa!
Mkuu Mzee Mwanakijiji:
Nadhani una fahamu kwamba Nyerere alijiuzulu muda sio mrefu baada ya kuteuliwa kuwa mjumbe wa baraza la kutunga sheria kwa hoja kwamba mazingira yale hayakumtendea haki kusimamia maslahi ya wananchi walio wengi - kwa maana ya kwamba mfumo mzima wa kisheria na kiutawala kwa ujumla haukuwa ukiangalia maslahi wa walio wengi (watanganyika weusi) hivyo asingeweza kuwatumikia wananchi hawa kupitia sheria na mfumo ule.
Hatua aliyochukua Mwalimu ndio ile ile ambayo Nguruvi3 ameijadili awali - kwamba inafikia wakati wa watu kuamua kwenda msituni kuendeleza mapambano ya kudai haki zao. Nadhani unaelewa kwamba TANU ilikuwa ni a political movement ambayo Mwalimu alijitahidi sana kuizuia isigeuke kuwa Militant licha ya temptations za hapa na pale.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Last edited by a moderator: