Jinsi Tundu Lissu Alivyojikaanga Kwa "Mafuta ya Taaluma Yake!!"


Mkuu Mzee Mwanakijiji:

Nadhani una fahamu kwamba Nyerere alijiuzulu muda sio mrefu baada ya kuteuliwa kuwa mjumbe wa baraza la kutunga sheria kwa hoja kwamba mazingira yale hayakumtendea haki kusimamia maslahi ya wananchi walio wengi - kwa maana ya kwamba mfumo mzima wa kisheria na kiutawala kwa ujumla haukuwa ukiangalia maslahi wa walio wengi (watanganyika weusi) hivyo asingeweza kuwatumikia wananchi hawa kupitia sheria na mfumo ule.

Hatua aliyochukua Mwalimu ndio ile ile ambayo Nguruvi3 ameijadili awali - kwamba inafikia wakati wa watu kuamua kwenda msituni kuendeleza mapambano ya kudai haki zao. Nadhani unaelewa kwamba TANU ilikuwa ni a political movement ambayo Mwalimu alijitahidi sana kuizuia isigeuke kuwa Militant licha ya temptations za hapa na pale.




Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Kwa kuwa ni Batili lazima iwekwe wazi, na siyo kukaa kimya. Hivyo baada ya Batili kujulikana, ni wakati Muafaka kukaa chini na KUHALALISHA!

Unahalalishaje kwa Sheria HARAMU ya Mabadiliko ya Katiba!
 
mkuu huu waraka unamfaa huyo ndugu asiye na heshima kwa kazi za wazee wetu, huko ni kupungukiwa adabu tu, na kupenda sifa za magazeti
 
ndio maana vijana wengi wa lumumba akili zao ni batili:embarassed2:
 

Kwenye nyekundu umekosea, yote sawa.
 
Ni mchakato wa kupata katiba mpya, kwa mujibu wa maelezo yako ubatili wa yote uliotokea huenda ukawa kweli lakini kinachotakiwa hapa ni kufanya mabadiliko wa ubatili huo kuwa halali kwa kuwa mwanzoni huo muda wa kufanya marekebisho hayo haukupatikana, (muda wa kupata katiba mpya ulikuwa bado). Kwa mantiki hiyo, ule uozo wote sasa ndo unatakiwa kurekebishwa!
"I HOPE HATA WEWE UNAKUBALI HOJA HIZO ILA HUTAKI KUTAMKA HADHARANI"
 
Inasikitisha sana
1. Kusubiri waasisi wafe ndo kujadili muungano.
2. Kutumika serikali ilihali huna imani nayo.

3. Kuingia ktk chaguzi na kuwa viongozi ktk jamuhuri kwa unafiki.

Nb. Tumirudishwa nyuma na maadui walojiingiza ktk utumishi wa umma ndani ya serikali ya jamuhuri yetu. Nchi hii siyo ya sultan seyd said. Tunapenda amani zaidi.
 
Ni maoni yako, siwezi kuyapinga, japokuwa hayatekelezeki! Tundu Lissu ajue kwamba tukiamua ku-rewind mkanda hatutafikia muafaka, he is smart enough to know that!

CCM mmejivika vazi la KiMungu ndo maana hamuishi vituko kama hiki cha kutishana maisha!! Kurewind mkanda upi zaidi ya aibu ya Kikwete hapo hapo bungeni aliyoitoa bila kuwa smart enough kwa baadaye.
 
Duuh! Raisi wetu Kikwete naye ni BATILI,
waziri mkuu Pinda ni BATILI,
Daah hata mimi ni Raia BATILI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…