carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Twaha Mwaipaya alitekwa siku chache baada ya John Pambalu kukamatwa na kufunguliwa kesi ya uhaini. Pambalu na Twaha walikimbilia Kenya ambako waliishi, karibu mwaka mzima ili kuokoa maisha yao.
Taarifa tulizonazo ni kuwa Jeshi la Polisi nchini Tanzania lilipata taarifa za Twaha Mwaipaya na taarifa za baadhi ya wanaharakati, viongozi wa CHADEMA, wachungaji pamoja na maaskofu walioikimbia nchi zilipatikana kwa Pambalu. Taarifa hizo muhimu ni pamoja na namba zao za simu na sehemu au mahali wanakoishi.
Inaelezwa kuwa siku aliyotekwa Mwaipaya kule Kenya alikuwa ameita 'taxi' (Bolt kwa Tanzania) kwa kutumia simu yake. Watekaji walifanikiwa kuifuatilia gari ile kwa njia ya kuifuatilia simu ya Twaha. Kwa ufupi, Twaha's mobile number was being tracked by his abductors! Watekaji wa Twaha walimfuatilia kwa kutumia simu.
Kwa sababu hiyo, ni muono wetu kuwa taarifa za Twaha ambazo watekaji walizitumia kule Nairobi, zilitoka kwa maafisa wa Jeshi la Polisi waliomhoji John Pambalu akiwa chini ya ulinzi Tanzania kabla hajafunguliwa kesi ya uhaini.
Tunashawishika kuhitimisha ya kuwa maofisa wa usalama waliomhoji John Pambalu, Jeshi la Polisi Tanzania na Serikali ya Tanzania kwa ujumla wanahusika na utekaji wa Mhe. Twaha Mwaipaya kule Nairobi, Kenya. Uthibitisho wa jambo hilo ni jinsi ambavyo media za Tanzania (za Serikali na zilizo karibu) na Serikali au CCM zilivyojitahidi kuzifukia taarifa za kutekwa kwa Twaha kwa kutotangaza habari hizo pamoja na kuibua picha za Dkt. Nchimbi wakidai ya kuwa alionekana Dubai. Lengo lao lilikuwa ni kutaka kuhamisha mawazo na akili za Watanzania ili waache kujadili kuhusu kutekwa kwa Twaha.
Hivyo, pamoja na kuibana Serikali ya Kenya juu ya kutekwa na kupotea kwa Twaha Mwaipaya akiwa katika ardhi ya Kenya, inafaa pia jumuiya ya kimataifa iihoji Serikali ya Tanzania kuhusu taarita za Twaha Mwaipaya ikiwemo simu yake na mahali anapoishi. Lakini ni kwa nini Twaha Mwaipaya atekwe na kupotezwa muda mfupi baada ya Jeshi la Polisi Tanzania kupata taarifa za Twaha Mwaipaya kupitia kwa John Pambalu wakati wanamhoji akiwa chini ya ulinzi?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 28 Oktoba 2026; Saa 2:42 asubuhi