Jinsi ubepari wa ardhi unavozidi kutesa watu

Jinsi ubepari wa ardhi unavozidi kutesa watu

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Sio neno geni kusikia mabepari.

ubepari ni mfumo wa kuongoza unaoruhusu mtu kua na mali yake binafsi.

Ni mambo mengi nchi kama ya kwetu imejikuta ikifata fomula ya kibepari japo sio kwa asilimia kubwa au kutokana na nchi yetu bado inaendelea.

Kwa nchi zilizoendelea ubepari una nafasi kubwa sana kama maana yake inavoeleza.

Kwa nchi yetu ukilala nje au kukosa kuwa na ardhi yako ni kujitakia ila kwa nchi zilizoendelea sio wamejitakia ila itatakiwa.

Ubepari wa ardhi unatesa sana watu ambao wasio kuwa na ardhi kisha kupelekea maeneo kuitwa slum.

Slum ni maeneo yasiyo kuwa na huduma yoyote wala umuhimu wowote.hata uswahilini kwetu tanzania ni kuzuri ndio maana wakenya wanatutamani sana.

ubepari wa ardhi usababisha watu kuwa duni sana na watu kuwa matajiri sana kupitiliza. mfano familia ya uhuru inaogopwa na serikali, Trump, Makaburu wa South Africa, India, Ulaya kote na magaribi yote.

Tanzania imebarikiwa kuwa na ardhi nzuri yenye kukufanya ufanye kitu chochote ila kwa wenzetu ardhi imegawanyika kwa ajili ya mabepari na utakayo achiwa wewe iwezekani kulima, kukaa au kuwa na watu wengi.

Ubepari wa ardhi leo unamfanya raisi aliyepita trump kuwa na ukwasi mkubwa sana.

ubepari wa ardhi unapelekea kupadisha kodi na hakuna anaye kukugusa ndio maana wanaitwa landlord.

Tulio bahatika na waliobahatika kuishi nchi zenye ubepari wa ardhi basi wanafahamu hata kodi ya jengo la kuishi ni kubwa hata kama unalipwa vipi kibaruani.

kwa mfano jiji la new york kodi ya chumba kimoja cha kuishi hapo mjini ni usd 3000. ukiwa south africa jozi ni rand 3500 chumba kimoja ni kwa mwezi sio mwaka.

Ombi langu: Vijana msije kuuza maeneo wala ardhi yenu ya kulimia,huko mbele mtakuja kutesa ukoo.

Kuna kipindi niliangalia wajapan wanatunza shamba lao la ukoo ambalo linazaidi ya miaka 600.
sasa wewe mtu kafa unakimbilia kuuza imagine wale waliuza kariakoo wanajuta.

IMG_0307.jpg
 
Back
Top Bottom