Corona bado ni gonjwa jipya, hakuna anaayejua hata utalificha vipi, kwenu huko sijasema mnaficha, nimesema hamna uwezo hata wa kupima, mnapima watu 300 kwa wiki tatu wakati sisi tunapima hao 300 kwa siku moja.
Sema ni kwamba hili gonjwa halionekani kuwa na makali yoyote kwa Mwafrika, maana hata huku kwetu tunakopima watu wengi kwa mkupuo, bado vifo ni vichache, na hata idadi kubwa ya wanaogundulika nacho wanadunda tu ndani ya karantini, yaani hawapo kwenye ventilators wala nini, wengi hata wanatamani watoroke maana mtu anajihisi mzima ila kipimo kimeonysha anacho kirusi.
Hivyo kwa Mwafrika utakuta wengi wanadunda mtaani wanatamba tu nacho mwilini, akikohoa kidogo anchukulia poa kama mafua ya kawaida, na hadi anapona bila kujua lilikua Likorona limemtembelea bila ya yeye kujua. Hili limewashangaza wazungu maana walitegemea tufe kama milioni kumi hivi, ila Afrika yote vifo bado vichache na kirusi kinazagaa kimya kimya.
Wasiwasi wangu ni kisije kubadilika na kuanza kuzamisha watu huku, tuombe mzungu awe ameshapata dawa maana kawaida Miafrika hadi mzungu agundue hatuna uwezo huo.