Jinsi UKIMWI ulivyogunduliwa

Jinsi UKIMWI ulivyogunduliwa

hKichaka

Senior Member
Joined
Apr 23, 2011
Posts
199
Reaction score
19
UKIMWI uligunduliwa mwaka 1981

HIV

Mwaka wa 1981, daktari mmoja wa California Marekani aliona vijana wa kiume watano, walioshiriki katika mapenzi ya jinsia moja, wakiwa na ugonjwa usiokuwa wa kawaida.

Walikuwa na homa ya pneumonia na saratani ya ngozi.
Dakta Gottlieb hakujua kuwa ripoti zake, ndio zitakuwa historia ya kwanza kuandikwa juu ya ugonjwa ambao baadae utakuja kuwa janga kubwa la AIDS, au UKIMWI.

Virusi vya HIV viligundulikana miaka miwili baada ya ugunduzi huo wa Dakta Gottlieb.

Tena damu ikaweza kupimwa kama ina virusi vya HIV, na baadae zikapatikana dawa kadha za kudhibiti ugonjwa huo.

Umoja wa Mataifa unakisia kuwa tangu mwaka wa 1981, UKIMWI umeuwa watu milioni 30, na idadi kama hiyo hivi sasa wanaishi na virusi vya HIV.

Lakini juma lilopita, umoja huo uliripoti kuwa idadi ya watu wanaoambukizwa inapungua katika nchi kadha, lakini mamilioni ya wagonjwa bado hawapati dawa wanazohitaji.

Matabibu wanasema virusi vya HIV sasa wanavifahamu sawasawa, na wagonjwa wanaofululiza kula dawa kwa wakati, wanaweza kuishi karibu maisha ya kawaida.


Source BBC website. BBC Swahili - Habari - UKIMWI uligunduliwa mwaka 1981
 
Kuna kitabu k1 kinasema AIDS will kill all the people in Uganda and Tanzania...hakika ukicheza tu kidogo unao

mimi naamini hii ndo Nuhu ya2 ya wanadamu walipofanya dhambi hadi kumsahau kabisa Muumba wao,umalaya na uasherati navyo vimekuwa vitamu mno na kupewa jina tamu la Ngono alafu wakahararisha Ngono eti kuna Ngono salama,Infiderity???
 
wanatengeza viruses kutuua, mbona kwao hawafi??
 
wazee hizi theory ya kuwa ukimwi ulianza africa ni kweli au ndio uzushi tu. wanakataa kusema umeanza kwa ma gay wa marekani. wanadai eti unatokana na masokwe ndio ukawafika wanadamu, wengine wanasema umetengezwa laboratory................
ipi sahihi?
 
inamaana baada ya kugundiliwa 81,mwaka 83 ukatua bukoba,hii kali.
 
Jaman naomben mnisaidie anayejua dawa ambayo nkiitumia itamalza tatzo la fangasi sehemu za siri kwan nmetumia dawa za hosptal had nmekata tamaa.
 
Nina wsiwasi Ukimwi Ulitengenezwa Maabara, kwa ajili ya either (1) Silaha ya kibaiolojia (2) kwa makusudi kuwipe out portion ya binadamu hususan Afrika(rejea kampeni za kucontrol population) (3) Kupunguza wingi wa Africa- Americans huko Marekani (rejea tuskgee experiment).
 
huu ugonjwa chanzo chake ni nini hasa; ulianzia wapi?

Je huu ugonjwa haukuwepo karne ya 19 ( yaani miaka ya 1800)

Na imekuwaje ukasambaa sana, kutoka bara moja kwenda jingine; halafu ukawa kwa wingi huku Afrika..

Ina maana sisi waafrika sio waaminifu sana?? Au ni vipi
 
Back
Top Bottom