Jinsi unavyoibiwa ukipima shamba kwa hatua

Yaani bwashe uliyeleta mada naona kila unavyokoment unazidi kunipoteza. Mimi Nina futi kamba....nikinunua shamba la 70*70m kwa hesabu za haraka nina 4900m2. Hizo 4000 za yard unazileta za Nini hapa bongo???? Nieleweshe
Ok shamba lako litakuwa na eneo la 4900m2 lakini hiyo sio eka ni zaidi ya eka.
 
sio sahihi pace yaani hatua huwa inakadiriwa meta 0.9 na sio .75 ulizozitaja. hivyo meta (0.9*70)* (0.9*70)=3969 kadirio ni 4000 au 4047.
 
sio sahihi pace yaani hatua huwa inakadiriwa meta 0.9 na sio .75 ulizozitaja. hivyo meta (0.9*70)* (0.9*70)=3969 kadirio ni 4000 au 4047.
mita 0.9 ni sawa rula tatu za daftarini (30cm). huo msamba, hatua?
 
Elimu yako kwangu imechelewa maana shapigwa na mipaka ilishawekwa.
 
70m * 70m = 49,000 m2 ; mita za mraba 4,047 umezipataje mkuu?
Ekari ni mita 4000,hekta ni mita 10,000, inamaana hekta 1= ekari 2.5
Kupata ekari unapima mita mia urefu kwa upana mita arobaini ,au vyovyote jumla tu ikupe elfu nne .
 
Hatua hiyo ya 75cm hapana ,nenda kashuhudie hatua za wapima mashamba unaweza lia hatua huwa ni 90cm to 1m maana wanapiga hatua hatembei kama wanavyotembea kawaida .hivyo muuza shamba huwa anaibiwa ,nayakuta sana haya unaenda shamba kufanya kazi ukijua eka au robo ukifika robo ni sawa na nusu ya vipimo .
Robo=1000m2
Nusu eka=2,000m2
Ekari moja=4,000m2
Hekta moja=10,000
Pia hekta 1= ekari 2.5
Hii hesabu muhimu saana kwenye kujua idadi ya miche shamban kwako hapa ndio unakuta unanunua mbegu ya eka ukifika kwako imeishia nusu shamba maana vipimo vya eka kwako ni kubwa zaidi ya uhalisia
 
hahaahhahahahahahahhahaahahaha
Nimecheka sana aisee daaah....ndo mana wanasemaga miguu mirefu kama mpima viwanja!
 
wenye mashamba wengine watata. wanakuuliza ''hizo ndiyo hatua gani? ndiyo unavyotembeaga??'' labda kama unanunua kwenye ardhi ya kijiji.
 
wenye mashamba wengine watata. wanakuuliza ''hizo ndiyo hatua gani? ndiyo unavyotembeaga??'' labda kama unanunua kwenye ardhi ya kijiji.

Hahhahaahahaahaha
Wazee inaelekea mmekutana na watu wenye character au kutoka sehemu tata sana
 
As the saying goes if something is easy its not worth doing
 
Hili jina Red Giant kama nshalionaga kitambo kwenye ishu ya ndizi/migomba au nimekosea
 
Amekuja n mantiki nzuri ila nahisi amewakilisha thread yake kama si alikuwa anasinzia basi itakuwa alikuwa anawahi 00:00 leo si unajua 16/6/2016 TCRA wanafanya yao
 
Amekuja n mantiki nzuri ila nahisi amewakilisha thread yake kama si alikuwa anasinzia basi itakuwa alikuwa anawahi 00:00 leo si unajua 16/6/2016 TCRA wanafanya yao
kuna kitu wanaita the curse of knowledge. unahisi unachojua kila mtu anajua. ila nimejitahidi niwezavyo kurahisisha.
 
kuna kitu wanaita the curse of knowledge. unahisi unachojua kila mtu anajua. ila nimejitahidi niwezavyo kurahisisha.
Nilifikiri unawahi TCRA mkuu,ila umesema ukweli kuhusu ununuzi kiwanja lazima tuwe makini sana
 
nafikiri bongo tumezoea mita. watu wengi hasa wa kitunguu hulalamika kuwa mavuno kwa hekari siyo kama walivyoambia lakini kumbe walilima 70% ya eka na si ekari kamili. vipi miti mkuu, hupanda mingapi kwa ekari?
Ekari 152 sawa mita za mraba ngapi
 
Hii nikweli kabisa.
Nilishawahi kupigiwa hesabu za eka kwa hatua sabini, nilivyokwenda na futi nikakuta kila heka moja ina 60m. Shamba la heka 30 nilipata 25. Ilikuwa too late maana mazao tayari yalikuwa yamekomaa.

Sikufikisha malengo.
 
Kama eneo lako ni mraba, ekari moja upana 63.3m na urefu 63.3m = 4,006m2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…