Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
JINSI YA KUJILINDA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII
1. Sio kila taarifa ni ya kushiriki katika Mitandao ya Kijamii, angalia umuhimu wa taarifa unayoishiriki. Internet haisahau
2. Kuwa makini na kuweka wazi eneo ulilopo na ikiwa ni muhimu kuweka eneo, fanya hivyo ukiwa haupo eneo husika
3. Epuka kutoa taarifa zako binafsi kwa watu usiowafahamu kwenye Mitandao hiyo
4. Usimpe mtu Nywila zako na hakikisha unabadilisha mara kwa mara
5. Wezesha kifaa/vifaa unavyotumia kuwa na ulinzi wa pili wa kuingiza Nenosiri (2 Factor Authentication) au ‘Passkeys’ inapowezekana
Sababu za Kujilinda kwenye Mitandao ya Kijamii
Faragha katika mitandao ya kijamii ni muhimu sana, kwani watumiaji huacha alama za taarifa zao bila kujua, jambo ambalo linaweza kuwaweka hatarini.
Matapeli na walaghai wa mtandaoni wanaweza kutumia taarifa zako kufanya uhalifu kwa kutumia utambulisho wako. Aidha, akaunti zako zinaweza kudukuliwa na kuathiri vifaa vyako kama simu au kompyuta.
Mhusika anaweza kuwa hatarini zaidi iwapo ataweka sehemu alipo kupitia 'live location' kwenye mitandao ya kijamii. Mitandao hii inaweza pia kutumiwa kwa uonevu, unyanyasaji, na kusambaza taarifa potofu au za uongo.
PIA SOMA
- Haya ni mambo ya kuzingatia uwapo mtandaoni ili kulinda taarifa zako binafsi kutumiwa vibaya na watu wenye nia ovu