Jinsi Uzushi wa WhatsApp Ulivyosababisha Mauaji nchini India

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Tukio lilivyoanza.

Julai 13, 2018 Marafiki watano walisafiri kwenda kijiji cha Handikera katika jimbo la Karnataka, India, kwa ajili ya matembezi ya mapumziko (picnic). Wanaume walifahamika kwa majina alham al-Kubassi, Mohammed Salman, Mohammed Azam, Mohammed Afroz and Noor Mohammad

Wakiwa njiani, walikutana na watoto wanaotoka shuleni na kuwapa chokoleti. Chokoleti hizo zililetwa na mmoja wa marafiki hao (Salham al-Kubassi) aliyekuwa amekuja kutembelea India akitokea Qatar. Hili ni jambo la kawaida kwa wageni wanaotembelea maeneo hayo.

Uvumi uliokuwepo hapo awali kupitia mitandao ya kijamii kuhusu utekaji wa watoto.

Kabla ya tukio hilo, kulikuwa na uzushi uliosambazwa kwa miezi mingi kwenye WhatsApp ukidai kuna magenge yanayoteka nyara watoto. Hali hii ilizua taharuki kubwa ya umma (mass hysteria) na kuwafanya wazazi kuwa na mashaka makubwa na wageni.

Kushukiwa kwa watekaji (Wale marafiki watano).

Wanakijiji waliowaona marafiki hao wakitoa chokoleti waliamini ni watekaji nyara. Walikaribia gari lao na kuanza kutoa upepo kwenye matairi.

Marafiki watatu walifanikiwa kutoroka kwa gari (wakiwaacha wenzao wawili nyuma). Hata hivyo, kabla hawajatoroka, wanakijiji walipiga picha na video za gari lao na kuzituma kwenye kikundi cha WhatsApp cha kijiji jirani cha Murki, wakiwaonya kuwa "watekaji nyara wanakimbilia huko."

Mauaji.

Wanakijiji wa Murki waliweka kizuizi barabarani, wakawavuta wanaume hao kutoka kwenye gari na kuanza kuwapiga vikali. Shambulio hilo lilimsababishia kifo Mohammed Azam (32), mhandisi wa programu za kompyuta na baba wa familia, huku marafiki zake wengine wawili wakijeruhiwa vibaya. Police walishindwa kudhibiti umati huo mkubwa.

Chanzo: Washingpost
 
Hata huku TZ nadhani Arusha kuna wafanya biashara ya vyakula kwenye harusi walinusurika kuuawa baada ya kuwapa watoto pipi.
 
Hii imenikumbusha tukio la kupigwa na kuchomwa moto mtu mmoja aliyekuwa akipandwa na kichaa huko Moro.
Jamaa kuna siku kakodi boda ampeleke safari ya mbali. Njiani vituo vikawa vingi mara kuchimba dawa!
Boda akaamua kugeuza chombo warudi walikotoka, abiria akaendelea kukalia pkpk mpaka kijiweni alipoanzia safari. Alipoombwa nauli akawa anaongea havieleweki ndo boda wakambadilikia na kuanza kumshushia kisago kisha wakamtia kiberiti.
Ndg zake walikuja kumtambua tayari kafa ndo raia wakajua kumbe ni mgonjwa wa kichaa!

Haya yote ni madhara ya kujichukulia sheria mkononi.
 
Daah inasikitisha sana asee, sad.

Ikawaje sasa mkuu?
 
Daah inasikitisha sana asee, sad.

Ikawaje sasa mkuu?
Ndo ikawa imeisha hiyo wakachukua mwili kwenda kuzika.
Bodaboda wao walifikiri kwamba jamaa alikuwa na mpango wa kupora pikipiki. Sasa raia tukawa tunajiuliza kama kweli huyo abiria alipanga kupora why akubali kurudi nyuma alikotoka hadi kijiweni kwa bodaboda?
 
Kwenye maisha inatakiwa uangalifu sana, wema umeua wengi sana!
Dada yangu haruhusu mtoto yoyote wa jirani ale kwake wala mazoea cz huko mahakamani uwa analetewa kesi za ovyo sana .
 
Back
Top Bottom