Jinsi vimashine vya Kamari holela vinavyoondoa sarafu katika mzunguko na kuathiri maisha ya wananchi

Jinsi vimashine vya Kamari holela vinavyoondoa sarafu katika mzunguko na kuathiri maisha ya wananchi

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Siku hizi katika nchi hii kuna biashara ya kamari holela ambapo kuna watu husimika vimashine vidogo vya kamari katika mitaa ya wananchi. Mara nyingi utavikuta vinashine hivyo katika sehemu zenye mikusanyiko mingi ya watu lakini vinakuwa vimefichwafichwa.

Wamiliki wengi wa vimashine hivyo ni Wachina, ambapo hushirikiana na Wabongo wachache ambao wao huwa ndo wako front, na Wachina wao huja baadae Usiku na kukusanya Sarafu kwenye ndoo.

Hii kitu serikali inajua, polisi inajua, serikali za mitaa zinajua lakini hawafanyi lolote. Huenda watu wa serikali za mitaa na baadhi ya polisi wana migao yao humo.

Soma pia:
Rais Samia athibitisha kuna uhaba wa Shilingi nchini. Bila ya kifo cha Mafuru tungelijua hili?



Huu ni uhujumu uchumi wa hali ya juu. Athari za mambo hayo ni ukosefu wa chenji, na kuondoa mzunguuko wa pesa ndogo kwa watu wenye kipato kidogo. Hii inafanya gharama za maisha kupanda kwa sababu watu wanapeg huduma zao kwenye pesa za juu kwa kutokuwa na uwezo wa kutoa chenji.

Haya mambo ya kipuuzi huwezi kuyakuta kwenye nchi zinazojielewa. Huwezi kuyafanya CHINA ukasurvive hata siku moja. Nashangaa nchi yetu inageuka shamba la bibi, tunakuwa kama MIJINGA fulani hivi kwa kuruhusu na kulea UPUMBAVU huu wa Kamari holela.

Hapa Sizungumzii Betting hizi za mipira (Japo nalo ni bomu). Nazungumzia Vending machines ambazo watu wanadumbukiza sarafu kucheza kamari. Hizi vending machines bubu zimetapakaa nchi nzima.Naambiwa hadi vijijini huko zipo
 
Zilemashine za luck-wheel zimesajiliwa na national gamming board..!

Halafu zile sarafu hawaondoki nazo, huwazinazungushwa pale pale kwa kuwauzia wachezaj..!

Kuna vimashine bubu vimewekwa hadi mitaani uswazi huko.

Kama wanasajili vimashine kama hivi mitaani basi ni dalili ya LOW IQ. Upumbavu mtupu
 
Siku hizi katika nchi hii kuna biashara ya kamari holela ambapo kuna watu husimika vimashine vidogo vya kamari katika mitaa ya wananchi. Mara nyingi utavikuta vinashine hivyo katika sehemu zenye mikusanyiko mingi ya watu lakini vinakuwa vimefichwafichwa...
Hatari sana hii
 
Wanalipa Kodi lakini.
Lakini Sasa hivi hata wabongo wanamiliki hizi mashine isipokuwa mashine zao wanaiba kwa wachina wanabadilisha mfumo wa ndani na motherboard ili mchina asiweze kugundua .

Hivyo wanapachika mashine hizo vijijini hasa kwenye vijiji vyenye minada ya watu wengi .

Kuhusu ufundi wake ,tayari Kuna wabongo wanajua mpaka jinsi ya kubadili mfumo kwa njia ya computer na kuzirekebisha pale zikiharibika .

Naripoti kutokea umalila
 
Kwahiyo hao Wachina wakichukua hizo sarafu wanazipeleka China? Hoja mfu kabisa.
 
Kwa sasa ni rahisi kununua kitu cha 200 kwa kutumia 10,000!
Elfu kumi ukiisha chenchi kwa ajili ya huduma ya mia mbili basi huna elfu kumi tena!
Ndio thamani ya hela inapokuwa ndogo.
 
Hii kitu naona iliandikiwa Taarifa ya Kiuchunguzi na gazeti la Jamhuri.

IMG-20241026-WA0048.jpg
 
Back
Top Bottom