Jinsi vyakula tulavyo vinavyotumaliza

Jinsi vyakula tulavyo vinavyotumaliza

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
LEO napenda kuchukua fursa hii kueleza kwa mapana na marefu suala la vyakula na namna ambavyo vimekuwa chanzo kikuu cha maradhi sugu yanayotukabili leo, ambayo mengi mwisho husababisha vifo.
Kuanzia wiki hii, taandika mfululizo wa makala kuonesha ni jinsi gani vyakula tunavyokula vimekuwa hatari kwa afya zetu. Naamini ukiungana nami kuanzia mwanzo hadi mwisho, utanielewa na bila shaka utachukua hatua za kubadili mtizamo wako kuhusu chakula.
Tukumbuke kwamba uzima wa mtu unategemea sana kinga aliyonayo mwilini, kinga ambayo hujengwa na ulaji wa vyakula vyenye virutubisho vya aina mbalimbali. Kwa namna ambavyo Mungu ametuumba, mwili unapaswa kujilindi wenyewe dhidi ya maradhi ya kila aina. Ukiwa na kinga imara ya mwili siyo rahisi kuugua mara kwa mara.
Magonjwa yanayojitokeza haraka pale kinga ya mwili inapokuwa chini, ni pamoja na kuugua malaria mara kwa mara, kifua kikuu, kutokwa na majipu, kutokwa uvimbe wa ajabuajabu katika mwili, kupatwa na mkanda wa jeshi, kupatwa na saratani na magonjwa mengine ya maambukizi.
Huo ni mfano wa kundi moja la magonjwa ya maambukizi, lakini hata magonjwa mengine hatari kama shinikizo la damu, magonjwa ya moyo, magonjwa ya viungo, kisukari, macho, na mengine mengi, huwa ni matokeao ya ulaji wa vyakula visivyo sahihi au uachaji wa ulaji vyakula muhimu.


CHANZO CHA KUSHUKA KWA KINGA
Ili uwe na kinga imara ya mwili, ni lazima uwe unakula mlo kamili unaojumuisha matunda, mboga za majani, nafaka na vyakula vingine vya asili, kwa sababu kila unachokula kina faida yake mwilini. Lakini siyo tu kula chochote kinachoitwa ‘chakula’, bali ule kilichosahihi na kilichosahihi.

Katika maisha tunayoishi sasa, hasa mijini, idadi Kubwa ya watu hawali kabisa vyakula sahihi, badala yake wanakula vyakula ambavyo si tu ni hatari kwa afya zao, bali pia hudhoofisha kinga ya asili ya mwili na hivyo kuufanya mwili kubaki dhaifu na unaoweza kupatwa na ugonjwa wowote.
Chanzo kikuu cha kushuka kwa kinga ya mwili kunasababishwa na ulaji wa vyakula visivyo sahihi ambavyo ndivyo vinavyopatikana kwa wingi kila mahali, hasa sehemu za mijini. Vyakula visivyofaa ndivyo vinavyotangazwa na kunadiwa kwenye vyombo vya habari kuwa bora.


VYAKULA HATARI VINAVYOLIWA KILA SIKU

Kuna orodha ndefu sana ya vyakula hatari ambayo huliwa kila siku, kuanzia asubuhi hadi jioni. Vyakula hivi yumkini huliwa kwa takriban maisha yote ya mtu na huonekana ni vya kawaida. Baadhi ya vyakula hivyo ni kama vile unga wa ugali, mkate, chips na juisi.

UNGA WA UGALI

Unga wa ugali unaotumiwa na watu wengi nchini ni sembe nyeupe. Chakula kikuu katika kaya nyingi zinazotumia ugali kama mlo wa kila siku huwa ugali mweupe uliotokana na mahindi yaliyokobolewa na kusafishwa, kisha kusagwa na kutoa unga safi mweupe. Kwa mtizamo wa macho na ladha ya mdomoni, wengi wanaamini kuwa ugali wa aina hii ndiyo mzuri na unaotakiwa kuliwa.

Ulaji wa ugali wa aina hii hauna faida yoyote mwilini, kwani hauna virutubisho, kwa sababu vilishaondolewa vyote wakati wa kukoboa. Virutubisho muhimu vya muhindi viko kwenye kiini chake, hivyo unapokiondoa unakuwa umeondoa lishe muhimu. Ndiyo maana hata panya hawali mahindi yaliyokobolewa
 

Attachments

  • Book-Fruits-Header.jpg
    Book-Fruits-Header.jpg
    29.3 KB · Views: 415
JINSI VYAKULA TULAVYO VINAVYOTUMALIZA-2



ce49cd4fe2a42cbcd83f0ca51f2d05e05adef965e3ee531ff40f1149420478bd069cc5ee28a1527b40154eb08098587feefe8482a4cfaa03036db64bd25094c93d55228dae8980453a0ea2ea48779ad96eb4bda2bac52d9144257f1720e4bd1e2ab8376144a43807c0999c892cfeeb22964

KATIKA makala zetu zilizopita, tulishaelezea madhara ya kula ugali uliotokana na mahindi yaliyokobolewa, tuliona kwamba chakula hicho kinapoingia mwilini hugeuka na kuwa sukari ambayo baadaye huweza kusababisha ugonjwa wa kisukari. Mgonjwa wa kisukari hukatazwa kula ugali wa aina hii na badala yake hutakiwa kula ugali wa dona, mtama au ulezi.

Kwa faida ya afya zetu na kwa ajili ya kuimarisha kinga ya miili yetu, sote tunatakiwa kula ugali wa dona, mtama au ulezi kabla hata ya kuugua. Vyakula hivi ni muhimu sana na siyo vya kimasikini kama ambavyo watu wengi wanadhani. Kwa bahati mbaya, upatikanaji wa unga wa dona umekuwa mgumu na ghali kuliko sembe nyeupe, hivyo kuwafanya watu wengi kukimbilia sembe nyeupe ambayo inapatikana kirahisi kila kona ya nchi na kwa bei nafuu.

Kwangu mimi naliona tatizo hili ni la kitaifa na kisera. Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ilipaswa kutoa elimu ya kutosha ya kuelezea madhara yatokanayo na ulaji wa sembe nyeupe kisha kuweka sera itakayokataza uzalishaji wa kibiashara wa sembe nyeupe kama ilivyo sasa. Sera ya namna hii ingeokoa maisha na afya za Watanzania wengi wanaoteketea kila situ kutokana na ugonjwa wa kisukari.

ce49cd4fe2a732a69f3c0bbf06210ae71bd3b86ba3f3090ae84b1109480278b21fc09ff136a754765d5b10add5db122eb1fca691b587a25c2061a55d8b5480c02a5f2299a083d954214dadb71d22964
Naamini kaya nyingi nchini hazijui kabisa kama ugali utokanao na sembe nyeupe wanaokula kila siku iendayo kwa Mungu, una madhara kiafya. Ni vigumu kuzieleza na zikakuelewa familia ambazo kwa maisha yao yote zimekuwa zikiamini kwamba kula ugali mweupe ndiyo kitu bora.
Serikali ilipaswa kuliangalia suala hili na kuona kama janga la kitaifa, ilipaswa kuanzisha kampeni maalum ya kutoa elimu kuhusu vyakula na lishe kwa njia mbalimbali, zikiwemo za matangazo redioni na kwenye televisheni.

ULAJI WA MATUNDA NA MBOGA
Hakuna kitu muhimu kwa mwili wa binadamu kama kujenga kinga ya mwili. Mwili unapokuwa na kinga imara, si rahisi kuugua magonjwa ya ajaba. Miongoni mwa kazi nyingi za matunda na mboga za majani, ni pamoja na hiyo kazi ya kujenga mwili na kuujengea uwezo wa kujikinga wenyewe.

Pamoja na umuhimu huo, ni watu wachache sana hula matunda na kuyachukulia kama sehemu ya milo yao ya kila siku. Watu wengi hula matunda au mboga za majani ‘kwa bahati mbaya’, huona siyo chakula muhimu sana. Hili ni kosa kubwa miongoni

mwa makosa mengi yanayofanywa na watu katika masuala ya afya.
Matunda yanatakiwa kuliwa kila siku na kwa wingi, vivyohivyo mboga za majani. Unapoacha kula matunda na mboga za majani za aina mbalimbali, jua unaukosesha mwili wako kinga dhidi ya maradhi yanayoweza kujitokeza mwilini.

VYAKULA HIVI NDIYO VINAVYOTUMALIZA

Vyakula tunavyotakiwa kuvila, hatuvili tena na pengine upatikanaji wake ni wa shida, hivyo tunalazimika kula vilivyopo licha ya kuwa vina madhara kwa afya zetu. Hali hii imeongeza idadi ya wagonjwa na magonjwa sugu.

Chakula kikuu cha mijini ni chips, kuku, mayai, soda, juisi za makopo au paketi, nyama choma na pombe. Pia kuna mkate mweupe, maandazi na chapati. Vyakula hivi huliwa kila siku, lakini ukivichambua utagundua havina faida yoyote mwilini zaidi ya kuingia na kutengeneza maradhi.
 
Dr usemayo ni kweli. Nikiwa mbali na nyumbani kwa wiki moja na zaidi, lazma nipate vidonda kwenye ulimi wangu. Nadhani vitamin C kutokana na kutokula matunda vizuri na mboga za majani zilizopikwa kichaga(zinapikwa hadi zinakoma zenyewe). Hapa nilipo utamu wa holiday umeingia shubiri, ulimi wote ni vidonda.
Endelea kutupa somo tafadhali.
 
Japo nikiri, mie muumini wa ugali mweupeee tena nataka mahindi yalowekwe kwanza. Dona halishuki asilani. Na chapati za atta zinanishinda, nimefanikiwa tu kwa kupenda kutumia brown rice.
 
JINSI VYAKULA TULAVYO VINAVYOTUMALIZA-3





KATIKA makala zetu zilizopita tulieleza madhara ya kula baadhi ya vyakula vya kukaanga kama chipsi na kuku, mkate mweupe. Leo tutaelezea madhara ya mayai na soda lakini tunamalizia mada ya chipsi.
attachment.php





CHIPS

Chips ambayo kwa kawaida hutengenezwa kutokana na viazi mviringo na kukaangwa kwenye mafuta, ni chakula kinachotakiwa kuliwa kwa kiasi kidogo na kwa nadra sana, kwa sababu kiko kwenye kundi la vyakula vyenye mafuta mengi ambavyo huliwa kwa uchache sana. Lakini hali halisi ni kinyume chake.

attachment.php





KUKU

Kwa kawaida, kuku wengi wanaotumika kwenye biashara ni kuku wa kizungu. Nyama ya kuku hawa haina virutubisho sawa na kuku wa kienyeji. Hii inatokana na ukweli kwamba kuku wa kizungu hulishwa madawa mbalimbali ya kuwakinga na magonjwa na hulishwa vyakula vilivyochanganywa madawa ili wakue upesi.


Kwa mazingira hayo, nyama itokanayo na kuku wa aina hii haiwezi kuwa bora. Kiasili kuku huishi mazingira huru kwa kula vyakula ambavyo hujenga na kuukinga mwili wake dhidi ya magonjwa mbalimbali, kuku wa aina hii ndiye anayefaa kuliwa na kuleta faida ya nyama ya kuku inayokusudiwa.

how-to-raise-chickens-to-lay-eggs1.jpg




MAYAI



Halikadhalika, mayai yanayopatikana kwa wingi mijini ni yale yatokanayo na kuku wa kufuga. Kiasili, mayai ya kuku wa kufuga, hayawezi kuwa sawa na mayai yatokanayo na kuku wa kienyeji. Huhitaji kuwa mwanasayansi kuona tofauti kati ya


yai la kuku wa kienyeji na kuku wa kufuga, kwani mayai hayo yakipikwa huwa tofauti kwa ladha na hata rangi.
Ni ukweli ulio wazi kuwa kuku wa kufugwa hulishwa vyakula vya kutengeneza ambavyo ndani yake huwekwa kemikali na madawa mbalimbali, wakati kuku wa kienyeji hula vyakula asili kwa kujitafutia wenyewe na mazingira wanayoishi ndiyo


yanayowafanya wawe tofauti na bora. Hivyo ni dhahiri kwamba mayai tunayokula ya kuku wa kizungu yana madhara zaidi kuliko faida mwilini.

15.jpg




SODA



Moja ya vinywaji vinavyopendwa na kutumiwa na watu wengi ni pamoja na soda. Matangazo mengi ya biashara yanafanyika kutangaza kinywaji cha soda na kuonesha kuwa ni kinywaji ambacho hakina madhara kabisa kwa mtumiaji. Kwa matangazo hayo na kampeni hizo, familia nyingi zimeamini kuwa soda ni kinywaji bora na hata watoto wetu wamerithishwa imani hii.


Lakini kwa upande wa pili wa kinywaji hiki, siyo kinywaji salama kama ambavyo imekuwa ikielezwa. Siwezi kusema moja kwa moja kuwa mtu huruhusiwi kabisa kunywa soda kama vile ni sumu, lakini watu walitakiwa kuelimishwa na kuelezwa madhara ya kupenda kunywa soda na athari anazoweza kuzipata mtu kiafya. Naamini tahadhari inayotolewa kwa wanywa pombe, hata kwa wanywa soda ilipaswa kutolewa pia.


Utafiti unaonesha kuwa soda, pamoja na vikorombwezo vingine, huwekwa sukari nyingi kiasi kisichopungua vijiko sita katika chupa moja. Kiwango hicho cha sukari ni kingi zaidi ya mara tano ya kile kinachoruhusiwa kwa mtu kutumia kwa siku. Na madhara ya sukari mwilini ni mengi, yakiwemo ya kudhoofisha kinga ya mwili na viungo kwenye sehemu za maungio na pia huongeza uzito wa mwili.


Ukitaka kujua soda ina madhara kiafya, fanya utafiti binafsi na utagundua haya ninayoyaandika. Kunywa soda zisizopungua tatu kwa muda mfupi, kisha lala usiku kama kawaida halafu wakati wa kuamka asubuhi, usikilize mwili wako. Utaamka ukiwa na maumivu mwili mzima, utajihisi uchovu, hasa sehemu za maungio, mfano wa mtu aliyefanya mazoezi mazito au kazi nzito siku iliyopita. Hiyo ni kutokana na kuingiza kiwango kingi cha sukari mwilini.


 

Attachments

  • chips.jpg
    chips.jpg
    20.2 KB · Views: 2,877
  • ESF_chicken_cooked.jpg
    ESF_chicken_cooked.jpg
    39.8 KB · Views: 3,152
JINSI VYAKULA TULAVYO VINAVYOTUMALIZA-4





WIKI iliyopita tulieleza matatizo ya kula vyakula mbalimbali kama vile chips. Tunaendelea kuwaeleza jinsi vyakula tunavyokula vinavyoweza kutumaliza, tukianza na juisi, sasa endelea.
JUISI


Katika hali ya kawaida, juisi ni kinywaji baridi kisicho na kilevi wala madhara kwa mnywaji. Lakini utakuwa sahihi ukizungumzia juisi zilizotengenezwa kwa matunda halisi bila kuongezewa vitu vingine. Katika zama hizi, hali iko tofauti,


juisi nyingi tunazodhani ni vinywaji baridi visivyo na madhara kwa afya zetu na za watoto wetu, hali haiko hivyo.
Juisi nyingi zinazouzwa kila sehemu ni feki. Ni jambo lakusikitisha kuona jinsi binadamu anavyojaribu kushindana na



Mungu kwa kutengeneza vitu vinavyofanana na vile alivyoumba Mwenyezi Mungu kwa ajili yetu. Juisi nyingi hutengenezwa kwa kuchanganya maji, sukari na rangi zilizotengenezwa kwa kemikali mbalimbali zikiwemo zenye ladha ya matunda.


Juisi za aina hii ndiyo nyingi na zinapatikana kila kona ya nchi hii, waathirika zaidi wakiwa watoto wetu ambao hupenda kunywa kwa kufuata utamu wa sukari nyingi zilizowekwa na ladha za matunda.
Utafiti umeonesha kemikali (Additives) zinazowekwa kwenye vinywaji hivi, hudhoofisha kinga ya mwili na huwa chanzo



cha magonjwa ya saratani na mengine hatarishi. Nakusihi kuacha kunywa kabisa juisi hizo na usimpe mwanao, unamuua.
Ukiacha hizo juisi zinazotengenezwa kwa kutumia kemikali ‘mwanzo mwisho’, kuna juisi zingine zinazodaiwa kutengezwa kutokana na matunda, zipo za ‘machungwa’, nanasi’, ‘pasheni’, n.k. Yapo makampuni pia yanayojitapa



kutengeneza juisi zao asilimia 100 kutokana na matunda na kwamba hakuna kinachoongezwa kingine. (100% fruit, No sugar added au No additives, huandika hivyo kwenye maboksi yao au makopo wanayoweka juisi).
Hata hivyo, utafiti wa hivi karibuni umeonesha kuwa makampuni mengi yanadanganya walaji.


Kwa sababu siyo kweli kwamba hawaongezi kitu kingine katika utengenezaji wa juisi zao za matunda. Imejulikana kuwa huweka vitu vya kufanya juisi ya kwenye boksi au chupa ikae kwa muda mrefu bila kuharibika, halikadhalika huweka vitu vya kuifanya juisi hiyo kuwa na ladha moja.


Acha nikupe mfano. Katika hali ya kawaida, ukichuma machungwa matano ya mti mmoja, lazima yatakuwa na ladha tofauti, yote hayawezi kuwa na ladha sawa japo yote yanatoka mti mmoja.
Kwa maana hiyo, kama ukitengeneza juisi kwa kutumia machungwa yaliyochumwa kutoka miti tofauti, ladha ya juisi



lazima itatofautina. Lakini utashangaa kuona ladha ya jusi za maboksi zote zinafanana.
Wanachofanya ni kuweka ladha moja kwenye utengenezaji wa juisi zao kabla ya kupeleka kwa mlaji. Halikadhalika, juisi ukishaitengeneza, haiwezi kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika. Kwa hiyo, ili kuifanya juisi hiyo iweze kukaa kwa



muda mrefu bila kuharibika, lazima iwekewe kemikali ya kuihifadhi isiharibike. Kwa kuongezewa vitu hivyo, hata kama juisi hiyo imetengenezwa kutokana na matunda halisi, inaifanya kukosa usalama kiafya.


Kwa maelezo hayo, hatushauriwi sana kunywa juisi hizo ‘ready made’ kwa sababu zimekosa uhalisia, kwani zina madhara kwa afya zetu, licha ya maelezo na matangazo mazuri tunayopewa na watengenezaji. Badala yake tutengeneza


juisi majumbani mwetu wenyewe kwa kutumia matunda halisi ili kupata faida katika miili yetu.
Jiepushe na matumizi ya sukari nyingi katika juisi unayoitengeneza mwenyewe, kwani kwa kufanya hivyo utakuwa unaiharibu, weka sukari kidogo sana ikiwezekana acha kabisa.




 
:target::target:watu wote tusome hii post... muhimu kwa afya zetu! bila kusahau kunywa maji mengi kila siku na kufanya mazoezi ya viungo!
:target::target:
 
JINSI VYAKULA TULAVYO VINAVYOTUMALIZA - 5

TUNAENDELEA kuwaletea mfululizo wa mada ihusuyo jinsi vyakula tunavyokula vinavyotumaliza, leo tuanze na mada ya nyama choma.

attachment.php





NYAMA CHOMA



Miongoni mwa vyakula vinavyopendwa na kuliwa na watu wengi ni pamoja na nyama za kubanika maarufu kama ‘nyama choma’ zitokanazo na wanyama (Red Meat). Kiuasili wake, nyama ni chakula muhimu kwa mwili wa binadamu kutokana na kuwa ndiyo chanzo kikuu cha protini. Na kwa kawaida, nyama choma huwa bora zaidi kuliko nyama za kukaanga au kuunga kwa mafuta.


Hata hivyo, ukiukwaji wa kanuni za mpangilio wa ulaji vyakula umeifanya nyama kuwa hatari kwa afya za watu wengi. Katika kundi la vyakula, nyama hasa nyekundu, imewekwa katika kundi la vyakula vinavyotakiwa kuliwa kwa kiasi kidogo kwa lengo la kuupatia mwili protini.


Lakini katika hali halisi, hali haiko hivyo. Watu wanapenda sana kula nyama kupita kiasi na kwa kiwango ambacho kiingiapo mwilini hugeuka kuwa sumu inayokimbilia kwenye ‘joints’ za miguu na kuwafanya walaji kupatwa na matatizo ya kuumwa miguu. Pia ulaji wa nyama kupita kiasi, huchangia ukosefu wa choo kwa muda mrefu kwa mlaji.


Ieleweke kwamba ulaji wa nyama siyo jambo la kuonyeshea ufahari au kujivunia, mtu anayekula mboga za majani au dagaa ni bora zaidi kuliko yule anayekula nyama kila siku. Hivyo kwa kujali afya zetu, tunashauriwa kula nyama kwa

nadra na kwa kiasi kidogo.Badala yake tupende zaidi kula mboga za majani, au samaki, kuku na dagaa.

Aidha, hata ulapo nyama choma au ya kukaanga au kupika, ikiwa ni jamii ya nyama nyekundi, ni lazima ujue jinsi ya

‘kubalansi’ mwilini. Itafaa zaidi ulapo nyama ukala pamoja na mboga za kutosha, zikiwemo nyanya, vitunguu na kisha kunywa maji mengi. Hii itakusaidia kuondoa sumu iliyopo kwenye nyama kwa urahisi zaidi pindi iingiapo mwilini.


Lakini kwa bahati mbaya sana, watu wengi hupenda kula nyama choma au mishikaki ya nyama nyekundu kisha kushushia na bia. Kwa mtindo huu wa maisha, watu hawa hutia mwilini vitu hatari ambavyo huleta madhara ya kiafya makubwa baadaye na hata tatizo lolote la kiafya likitokea, si rahisi kujua limetokana na staili hii ya maisha. Tunatakiwa kujiepusha na mtindo huu wa maisha.


attachment.php






MKATE

Wote tunakula mkate na tunapenda, kutokana na ukweli kwamba ndiyo chakula kikuu cha asubuhi kwa familia nyingi za mijini. Mkate unaopendwa na walaji wengi ni mkate mweupe ambao hutengenezwa kutokana na ngano iliyokobolewa,

kusafishwa na kutiwa vikorombwezo vingine ikiwemo sukari. Kwa ladha ni mitamu na limekuwa ndiyo chaguo la wengi.

Lakini kiafya chakula hiki ni miongoni mwa vyakula vinavyochangia matatizo mengi ya kiafya. Kinachofanya chakula hiki

kuwa hatari ni kwa sababu kinatengenezwa kutokana na ngano iliyokobolewa na kuondolewa virutubisho vyake muhimu vya asili na kuongezewa vitu vingine vya kuongeza ladha ambavyo siyo salama kiafya.


Mkate mweupe unapoliwa kwa wingi kila siku huchangia matatizo ya ukosefu wa choo kwa mlaji na huchangia matatizo ya ugonjwa wa kisukari. Inaelezwa kuwa vyakula vyote vinavyotengenezwa kutokana na nafaka iliyokobolewa,

ukiwemo ugali wa sembe nyeupe, viingiapo mwilini hugeuka na kuwa sukari, hivyo ulaji wa vyakula vya aina hii kwa wingi ni sawa na mtu anayekula sukari kwa wingi.



 

Attachments

  • Loaf-of-bread.jpg
    Loaf-of-bread.jpg
    108.6 KB · Views: 2,603
  • Mishikaki.jpg
    Mishikaki.jpg
    51 KB · Views: 414
  • Nyama choma.jpg
    Nyama choma.jpg
    694.6 KB · Views: 2,478
Ni elimu nzuri sana Mkuu Mzizi Mkavu. Nimeipenda sana. Ni kweli sasa hivi maradhi yamekuwa mengi kwa watu wanaoishi modern life style tofauti na watu wanaoishi vjijini. Tuzingatie ushauri huu maana hata kiuchumi una unafuu wa kutosha. Mzizi Mkavu hii elimu iendelee zaidi hadi kwa watu chini kabisa kupitia makala za magezetini, vitabu, vidio records, posters midahalo na mikutano. Itaokoa wengi.
 

VYAKULA HIVI NDIYO VINAVYOTUMALIZA

Vyakula tunavyotakiwa kuvila, hatuvili tena na pengine upatikanaji wake ni wa shida, hivyo tunalazimika kula vilivyopo licha ya kuwa vina madhara kwa afya zetu. Hali hii imeongeza idadi ya wagonjwa na magonjwa sugu.

Chakula kikuu cha mijini ni chips, kuku, mayai, soda, juisi za makopo au paketi, nyama choma na pombe. Pia kuna mkate mweupe, maandazi na chapati. Vyakula hivi huliwa kila siku, lakini ukivichambua utagundua havina faida yoyote mwilini zaidi ya kuingia na kutengeneza maradhi.

raw food is best but processed food is bad news altogether..................lakini kinachotumaliza hivi sasa ni hiv..................let us tell it the way it is.....young men are dying..................................and so are our beautiful gals..........................they are 2 young to die...............
 
Japo nikiri, mie muumini wa ugali mweupeee tena nataka mahindi yalowekwe kwanza. Dona halishuki asilani. Na chapati za atta zinanishinda, nimefanikiwa tu kwa kupenda kutumia brown rice.

Jamani King'asti jaribu basi kula habat sawdaa au muwa mweusi
 
Mkuu Mzizi asante kwa ujumbe mzuri, nina swali moja tu kwako;

Vipi kuhusu maji? Tunywe ambayo ni unprocessed? Yaani yasiyochemshwa na yasiyotoka kiwandani?

Je bottled drinking water such as Kilimanjaro, Coolblue, Uhai n.k. Ni salama?

Nitafurahi nikipata majibu yako!
 
vyakula vyenye testi ndio vibaya kwa afya.brown rice ina testi mbaya,kuku ana taste nzuri,chapati.au vitumbua vyote vitamu.angalau fruit zina testi nzuri tu.na hizo picha za fruit zimenitamanisha
 
Hizi ndizo mada tunazopenda kusoma. Zinatuelemisha. Nyie watoto wa MMU njooni mchote elimu huku. Acheni porojo zenu kule MMU. JF ni kisima cha elimu. Asante sana uliyeanzisha mada hii.
 
Umecheck afya lakini usikute kale kaugonjwa kakisasa kametia nanga ndani ya mwili wako ha ha ha ha just a joke.

Dr usemayo ni kweli. Nikiwa mbali na nyumbani kwa wiki moja na zaidi, lazma nipate vidonda kwenye ulimi wangu. Nadhani vitamin C kutokana na kutokula matunda vizuri na mboga za majani zilizopikwa kichaga(zinapikwa hadi zinakoma zenyewe). Hapa nilipo utamu wa holiday umeingia shubiri, ulimi wote ni vidonda.
Endelea kutupa somo tafadhali.
 
Yale yale tuliyokua tunayaona yamepitwa na wakati sasa tutayarudia ili tujiokoe na kubaki salama, miaka ya nyuma hapa watu walikua wanaona watu flani wakila ugali wa mtama na mhogo wanasema washamba sasa amawarudie maisha ya kiafrika halisi ama kila leo hosp kwa magonjwa kibao!!
 
Yale yale tuliyokua tunayaona yamepitwa na wakati sasa tutayarudia ili tujiokoe na kubaki salama, miaka ya nyuma hapa watu walikua wanaona watu flani wakila ugali wa mtama na mhogo wanasema washamba sasa amawarudie maisha ya kiafrika halisi ama kila leo hosp kwa magonjwa kibao!!

Ni kweli kabisa....
 
Ahsante sana doctor kwa ushauri mzuri nilio upata. Doctor nina swali moja naomba kuuliza. Umesema tule vya kula vya nafaka ambavyo havikobolewa,na mm nakubaliana kabisa na wewe. Je kwenye hii nafaka aina ya mpunga na ngano aina ya shairi na wali wengi wetu ni wapenzi sana.
 
Mkuu Mzizi asante kwa ujumbe mzuri, nina swali moja tu kwako;

Vipi kuhusu maji? Tunywe ambayo ni unprocessed? Yaani yasiyochemshwa na yasiyotoka kiwandani?

Je bottled drinking water such as Kilimanjaro, Coolblue, Uhai n.k. Ni salama?

Nitafurahi nikipata majibu yako!
Mkuu Brooklyn Maji hayo uliyoyataja kama yamethibitishwa na wataalam kuyatumia kwa kunywa yanafaa kunywa lakini kama wataalam wamesema hayafai kunywa basi usiyanywe na itakuwa jambo la maana maji ya kunywa ukayachemsha kidigo yawe maji ya uvuguvugu kisha ndio unywe itakuwa ni vizuri kiafya.

Ahsante sana doctor kwa ushauri mzuri nilio upata. Doctor nina swali moja naomba kuuliza. Umesema tule vya kula vya nafaka ambavyo havikobolewa,na mm nakubaliana kabisa na wewe. Je kwenye hii nafaka aina ya mpunga na ngano aina ya shairi na wali wengi wetu ni wapenzi sana.
Mkuu omben unaweza kula hivyo vyakula ulivyosema ni vizuri kiafya hakuna wasiwasi mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom