Rogojin The Idiot
JF-Expert Member
- Jul 25, 2017
- 2,969
- 3,392
Wanajiita mawakili wasomi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Achana nahao wameshaambiwa kama wanataka kucheza wasubiri filimbi ipigwe♧♧♧♧♧》《Tumia akili kidogo tu uliyobakiwa nayo, hivi waliotangaza kuwa hao watuhumiwa ni makomandoo ni Polisi ama Wakili wa Utetezi...
Kumbuka hayo maswali yote yanatolewa kwenye maandishi yaliyoandikwa na polisi wenyewe.
Internet ikizimwa na mapato ya serikali hayaingii hazinaSerikali ikitaka kudhibiti mitandao ya kijamii wazime tu internet... Kinyume na hapo watapata tabu sana.
Hawa Police wamejiweka kwenye KESI Kama 21, ila Kuna watu watakimbia, mahakama nasema,Mawakili wa utetezi wanashule Sana jamaniJinsi wakili msomi Dickson Matata alivyompeleka puta mtoto wa IGP Mahita.
MATATA: Nikumbushe Majina yako.
SHAHIDI: Naitwa Inspector Mahita Omary Mahita.
MATATA: nitakuwa Sahihi nikisema wewe ni Mtoto wa IGP mstaafu Omary Mahita.
SHAHIDI: Upo sahihi
MATATA: Wakati Baba yako akiwa IGP wewe Ulikuwa wapi?
SHAHIDI: Nilikuwa Chuo kikuu
MATATA: Wakati Baba yako akiwa IGP ulikuwa na akili timamu?
SHAHIDI: Ndio
MATATA: Unakumbuka madai ya baba yako kuwakuta CUF na visu akadai wamekusudia kufanya ugaidi.
WAKILI WA JAMHURI: Objection Mheshimiwa Jaji. Naomba swali hilo liondolewe.
MATATA: Wakati mnawakamata watuhumiwa mlikuwa na Kikosi Maalum?
SHAHIDI: Ndio
MATATA: Kikosi chote kilitokea Arusha?
SHAHIDI: Ndio
MATATA: Na kikosi hicho kilikuwa chini ya RPC Kingai ambaye wakati huo alikua RCO Arusha?
SHAHIDI: Sahihi kabisa
MATATA: Unapotoka kwenye kituo unapaswa kuwa na Movement Order?
SHAHIDI: Ndio
MATATA: Ulipotoka Arusha kwenda Moshi hukueleza kuwa na movement order.
SHAHIDI: Nilikua nayo.
MATATA: Ulimweleza nani?
SHAHIDI: Sikueleza lakini nilikua nayo
MATATA: Maelezo yako ya awali hayaelezi hivyo.
SHAHIDI: Kimya.
MATATA: Je unajua kwamba unapofika mkoa mwingine unapaswa uriporti kwanza kwa Mlmamlaka za Mkoa huo?
SHAHIDI: Ni kweli.
MATATA: Katika maelezo yako hakuna popote uliposema umeripoti kwa mamlaka za polisi Moshi.
SHAHIDI: Ni kweli lakini?
MATATA: Hakuna lakini, jibu NDIYO au HAPANA.
SHAHIDI: Niliripoti lakini labda kwenye maelezo nilisahau kuandika.
MATATA: sasa kama hukuandika ulitegemea mahakama iote?
SHAHIDI: Kimya
MATATA: Una ushahidi wowote unaoonesha mliripoti mamlaka za polisi Moshi kabla ya operesheni yenu?
SHAHIDI: Ndio
MATATA: Uko wapi?
SHAHIDI: sijaja nao
MATATA: mlipowakamata watuhumiwa mliwasafirisha kuja Dar?
SHAHIDI: Ndio
MATATA: walipofika Dar mliwatoa central na kuwapeleka Mbweni?
SHAHIDI: Ni kweli.
MATATA: Kwanini mliwapeleka Mbweni?
SHAHIDI: Kwa sababu ya usalama.
MATATA: Kati ya Cetral na Mbweni wapi kuna usalama zaidi?
SHAHIDI: Lakini..
MATATA: Jibu, acha lakini.
SHAHIDI: Mbweni.
MATATA: Kati ya Central na Mbweni wapi kuna askari wengi?
SHAHIDI: Central.
MATATA: Kati ya central na Mbweni wapi kuna silaha nyingi zaidi?
SHAHIDI: Central.
MATATA: Kati ya central na Mbweni wapi panaweza kupatikana msaada wa haraka ikitokea dharura?
SHAHIDI: Central.
MATATA: Sasa unasemaje Mbweni kuna usalama kuliko central?
SHAHIDI: ili watuhumiwa wasiweze kutoroka.
MATATA: Umewahi kusikia pale central kuna watuhumiwa wametoroka?
SHAHIDI: kimya
MATATA: Jibu swali, umewahi kusikia watuhumiwa kutoroka central?
SHAHIDI: wangeweza kutoroka.
JAJI: Mbona swali rahisi, jibu kama umeshawahi kusikia wametoroka?
SHAHIDI: Mheshimiwa Jaji mimi sijui.
MATATA: Kwanini mliwapeleka watuhumiwa Mbweni?
SHAHIDI: Ni kwa maelekezo ya viongozi wangu.
MATATA: Nakuuliza wewe, sio viongozi wako.
SHAHIDI: Kama nilivyosema ni sababu za kiusalama.
MATATA: Utakubaliana na mimi kwamba mlipowaleta watuhumiwa Dar hujasema mliripoti kwa nani?
SHAHIDI: Tuliripoti kwa mamlaka za polisi kanda maalumu na mkoa wa kipolisi Kinondoni.
MATATA: Kwenye taarifa yako kuna mahali umeeleza hayo?
SHAHIDI: Hapana.
MATATA: Unaelewa kabla ya kuwasachi watuhumiwa, ilibidi nyie mlisachiwe kwanza?
shahidi ni kweli sijazungumza hilo.
SHAHIDI: Ndio
MATATA: Lakini kwenye maelezo yako hujaeleza ka mlisachiwa kwanza kabla ya kuwasachi watuhumiwa.
SHAHIDI: Tulisachiwa japo sijaeleza.
MATATA: Kwa kuwa hujaeleza nitakosea nikisema hamkusachiwa.
SHAHIDI: Kimya.
MATATA: Umeeeleza kuwa watuhumiwa ni Makomandoo wa JWTZ?
SHAHIDI: Ni kweli.
MATATA: Utakubaliana na mimi kwamba Makomandoo ni watu ambao wanahitaji ulinzi zaidi?
SHAHIDI: Sahihi.
MATATA: Lakini katika maelezo yako hakuna popote umesema mliwasifirisha kwa pingu? Je utakubaliana na mimi nikisema mliwasafirisha makomandoo wa jeshi kizembe bila kuwafunga pingu?
SHAHIDI: Tuliwafunga
MATATA: Lakini maelezo yako uliyoandika hayaelezi hivyo.
SHAHIDI: Itakua nilisahau tu.
MATATA: Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.!
Malisa GJ
View attachment 1942312
weee nae km mtoto hujui walikuwa wan mtuliza kichawi??? haya mabo na uchawi unatumika sana ndo maana wanga wngi polisi siku hiziHalafu mtu unajiuliza...Hivi polisi walitoa wapi huruma ya kumnunulia mtuhumiwa wa ugaidi tena Komandoo supu na Mo energy?