Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Hawa wamisri wa kale ndiyo watu walioleta ustaarabu tunaouona duniani leo hii. Wagiriki walijifunza ustaarabu kutoka Misri ya kale. Moja ya mambo waliyogundua ni kuwa mwaka una siku 365. Waligundua namna hii.
Ukichunguza jua kwa mwaka mzima utaona kuwa sehemu linakichomoza na kuzama hubadilika ndani ya mwaka. Sehemu linapochomoza mwezi wa kumi na mbili ni tofauti na linapochomoza mwezi wa sita.
Sasa wamisri waliweka alama sehemu jua linapochomoza, kisha wakahesabu siku ambazo zitapita hadi jua lije kuchomoza sehemu ileile tena. Waligundua kuwa jua linachukua siku 365 kurudi kuchomoza sehemu ileile.
Hili linaweza kufanyika hata kwa kuangalia kivuli. Kivuli huwa kinabadili muelekeo ndani ya mwaka. Sasa ili kirudi kwenye muelekeo kilichopo leo kitatumia siku 365. Jamaa walikuwa wako vizuri sana upstairs.