thereitis
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 297
- 41
Tumeshuhudia matokeo mabovu ya kidato cha nne miaka miwili mfululizo, 2010 na 2011. Haya ni matokeo ya siasa uchwara katika mipango ya elimu. Ni wanasiasa wanaoshawishi au kulazimisha mipango mingi ya elimu hapa nchini. wataalam wa sekta ya elimu wamekuwa wakitekeleza matakwa ya siasa ili kunusuru ajira zao. Mfano mmojawapo ni uanzishwaji wa shule za kata mwaka 2006 chini ya uongozi wa waziri mkuu aliyejiuzulu; shule nyingi za kata zilianzishwa bila kujali ubora wa elimu.
Wanasiasa wamekuwa wakiwadanganya wananchi kwa kutumia takwimu ya wanaohudhuria shule na siyo ubora wa elimu. Swali kwa wanajamii wenzangu ni Je, ni jinsi gani wanasiasa wanachangia kuharibu au kuboresha mipango ya elimu hapa nchini? Mimi nimetoa mfano mmoja wa shule za kata.