Kumbe vita havitakuja kuisha duniani hata karne zijazo kwa sababu binadamu tunatofautiana mitazamo na imani. Historia inaonesha vita vilikuwepo karne na karne sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Ulaya. Baada ya vita vya pili vya duniani, vita vilibaki zaidi Afrika ambapo ilionekana Waafrika wanapenda vita. Leo hii tunaona vita vinataka kurudi kwa kasi Ulaya. Tulijua Ulaya wameishastaarabika wanakaa meza moja na kuzungumza lakini kumbe sivyo, vita ni hulka tu!
Habari kamili;
Katika uwanja wa mafunzo ya kijeshi karibu na jiji la Wroclaw, Wapoland wa kawaida wamepanga mstari, wakisubiri kukabidhiwa bunduki na kufundishwa jinsi ya kupiga risasi. "Mara tu duru inapopakiwa, silaha iko tayari kufyatua risasi," anafoka mwalimu, askari wa Poland, uso wake ukiwa umepakwa rangi ili kuficha utambulisho wake.
Vijana na wazee, wanaume na wanawake, wazazi na watoto, wote wamekuja hapa kwasababu moja: kujifunza jinsi ya kunusurika mashambulizi ya silaha.
Pamoja na kuwasha safu ya upigaji risasi, kipindi cha Jumamosi hii asubuhi, kiitwacho "Train with the Army" [Jifunze na Jeshi] , pia hufundisha raia mapigano ya ana kwa ana, huduma ya kwanza na jinsi ya kuvaa barakoa ya gesi.
"Nyakati ni hatari sasa, tunatakiwa kuwa tayari," anasema mratibu wa mradi huo, Kapteni Adam Sielicki. "Tuna tishio la kijeshi kutoka Urusi, na tunajiandaa kwa hili."
Chanzo; BBC Swahili