Amba Samedi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2024
- 207
- 346
Habari wanaJF,
Natumaini mnaendelea vizuri. Nimeamka salama. Nililala saa 8 usiku, baada ya kikao kirefu na mmarekani mmoja, hapa nkishamaliza kuandika nazama tena usingizini kidogo.
Leo katika pitapita zangu, nimekutana na ripoti moja iliyochapishwa na Sahara Ventures.
Waliwauliza watanzania kadhaa kuhusu wanavyochukulia akili mnemba. Na majibu yao haya hapa:
Swali la 1: Ni Sekta Zipi Zitakazoathiriwa na AI?
Imeonekana kuwa sekta zitakazoathiriwa ni kama zifuatavyo:
Swali la 2: Ni Sekta Zipi Zitakazoathiriwa na AI?
Asilimia 60 kasoro wanaamini kuwa AI itakuwa mshindani mkubwa kazini. Maoni yangu: ni zaidi ya hapo. Jifunze kutumia AI upone.
Swali la 3: Hivi Kati ya Akili Mnemba na Daktari wa Kawaida, Yupi Akutibu?
Zaidi ya nusu ya waliojibu hili wanaonekana kuweza kuamini AI katika matibabu. Hii pia inaonyesha imani ya watu iko wapi kwenye matibabu na kuwaamini madaktari wao!
Swali la 4: Hivi AI inaweza kuchora sera za Nchi?
Ni mwaka wa uchaguzi. Kati ya watu 3, wawili waliamini kuwa AI inaweza kufanya kazi nzuri zaidi katika kupanga mikakati ya kuendesha nchi hii ukilinganisha wa wanasiasa wetu.
Swali la 5: Je, AI itabadilisha sura ya Afrika ya Kesho?
Hapa, karibia wote walikubali. Hakuna serikali wala shirika la dini/kipagani ambayo inaweza kuzuia vuguvugu hili la mwendokasi. We adapt or perish (tuendane nayo au tuangamie).
Swali la 6: Upanuzi wa Teknolojia ya AI itakuwaje kesho?
Inasemekana kuzuizi kikubwa hapa kitahusiana na uwepo wa kanzidata (ni kweli), lakini pia sera za nchi (Tanzania bado kuna watu wanaamini AI inasema uongo), na elimu/ujuzi wa matumizi.
Swali la 7: Je, Unaiogopa AI?
Asilimia 60 walikiri kuogopa matokeo ya matumizi ya AI, ikiwemo cyber warfare (vita vya mtandaoni). Inabidi tuwe makini hapa, maana ni kweli. Mashine zitazidi kupata nguvu, na kuna haja ya kujifunza kutuliza nguvu hizi kwa manufaa yetu.
Endapo unataka kujifunza mengi zaidi kuhusu AI, niandikie SMS/whatsapp 0742308110 au email [email protected]

- Afya (71%)
- Kilimo (14%)
- Elimu (10%)
- Uongozi na utawala (5%)