Jinsi wauza Nyama Buchani wanavyowaibia wateja

Jinsi wauza Nyama Buchani wanavyowaibia wateja

Kichakoro

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2008
Posts
3,335
Reaction score
6,186
Nimetembelea mabucha mengi sana hapo Dar Mwenge na Kariakoo ndio vinara wa wizi wakifuatiwa na wa Shekilango, Mabibo, Goba Mwisho, Africa sana (mabucha ya nyama na samaki lao moja)

Ukienda kununua nyama kuna zile mizani ambazo ni digital ukinunua nyama kuanzia kilo moja na kuendelea lazima wakuibie. wanachofanya - kuna mabeseni ya kama aina tatu fauti dogo lina gram 225g, la kati lina gram 362gm na kubwa lina 825gm

Ukienda kununua nyama kama ni nyama nyingi zaidi ya kilo 3 wanatumia lile beseni kubwa nyama inawekwa kwenye besini ambalo halipo kwenye mizani, kisha mizani anaiset 00 mteja utaridhika ni 00 hapo tayari kakuibia nyama au samaki gm nyingi kulingana na besini alilotumia.

kumbuka mizani inapaswa kuwa 00 wakati beseni likiwa juu ya mizani bila nyama kisha aweke nyama mpaka kiwango kile unachopaswa kununua na si vinginevyo.

OMBI: Usikubali kupimiwa nyama na besini kama hilo beseni halikuwekwa juu ya mezani bila nyama na kulireset 00 ndipo nyama iwekwe juu yake.

watu wa mamlaka ya vipimo tembeleeni mabucha hasa siku za mwisho wa week na sikukuu ndio hali huwa mbaya zaidi. Unapogundua udhaifu kwenye bucha usiogope kuwajulisha wote waliopo buchani hapo ili wajui
 
Goba ndiyo wahuni kwelikweli nyama inauzwa kilo sh 5000 lakini ukinunua kilo kuanzia tano ujue unanunua kilo Tatu tu,ni wezi balaa Goba center
 
Daah kilo 5000 wakati huku kwetu hiyo ni nusu? Kweli mnakula maisha aisee
 
Tegeta kwa ndevu pale ni balaa, niliwahi kununua nyama kilo 3, nikaenda kwa mama muuza mchele nikamuomba anipimie ile nyama kwenye mzani wake ukasoma 2.25 kg nikarudi kwenye ile bucha nikawaeleza waipime tena upya maana na mashaka na kipimo huku nikiwa mkali kweli kweli, wale vijana walichukua jiwe lingine chini ya meza na kunipia upya, nikarudi tena kwa yule mama kupima ikasoma 3kg, yule mama akanieleaza kuwa huo ndiyo mchezo wao pale, kuanzia siku hiyo niliapa kutonunua nyama wala samaki pale.
 
Hata mbezi mwisho huu mchezo upo Sana na. Pia nimeambiwa hata wanapouza mchele na maharage nao wameanza huo nchezo
 
Achana kabisa na pale Goba center kuna bucha kama tatu hivi moja ipo upande wa kushoto mbele kuna mabodaboda nyingine zipo kulia tena kuna moja ukiiona ni kama ya kisasa jengo zuri vioo safi ila ujue ukinunua kilo moja ujue umenunua robo tatu nilishaachana nao kabisa katika kila kilo wanaiba robo
 
Inakuaje uki-tare (00) isisome sawa?!

Sema labda mzani unakua haujawa calbrated. Lakini kama mzani uko sawa, hata uweke tray na kilo 10 ju, uka-tare (00) nyama itakua uzito ule ule eg kilo 1.
 
Mimi ni mfanyabiashara ninayetumia mizani...katika vitu ninavyoviheshimu ni mzani.siwezi kucheza na mizani maana ukiona mfanyabiashara ameanza kuwaibia wanunuzi kwenye mizani ujue yuko karibu kufilisika
 
Bora ununue kuku/sungura/bata/kanga n.k hivi vitu vya kupima vinahitaji uwe na moyo wa uvumilivu
 
Back
Top Bottom