Wanajukwaa
Kwanza nikubali kwamba ipo post ya member wa hapa jf ambaye alijaribu kutoa somo kuhusu jambo hili ambayo inapatikana hapa
Jinsi ya kuacha kuvuta sigara (A Guide to Quitting Smoking)
Lakini baada ya
kuipitia na kuisoma kwa umakini nikagundua kwamba mwandishi hakuandika akaelewekaa hasa katika matumizi ya
lugha na taratibu za kufuata zikiwepo dalili (symptoms) za kuachana na tabia hii mbaya hasa kwa watanzania wengi ambao hawajaijua vyema lugha ile.
Hapa tutakuwa na uzi mrefu utakaokuwa
msaada kwa vijana na hata watu wazima ambao
KWA BAHATI MBAYA wamejikuta katika u
tumwa wa nicotine.
Kwanza ieleweke wazi kwamba
KUACHA SIGARA AU ZAO LOLOTE LA NICOTINE ni kama
vita dhidi ya mwili (hasa
ubongo) wa mtumiaji. Yaani ni vita ndani ya mwili huku sehemu yenye
nguvu zaidi katika mwili (mind/emotions/brain) zikisimama kinyume
(kwa muda) na matakwa ya conscious thinking (tuiite hivyo kwa sasa)
Wengi wameshindwa kuacha tabia hii kwa kukutana na magumu au majaribu (temptations) zinazopelekea urges (craving) au ile hali ya
kujisikia kuvuta tena. Lakini imekuwa kama janga kwamba kwa huku kwetu Afrika ni mara chache sana watu wanaovuta sigara kupewa hamasa ya kuacha
KWA KUAMBIWA UKWELI WOTE. Ni kama limekuwa tatizo sugu kwa
nguvu ya taifa (vijana).
Hapa tutapena
mbinu na dondoo (tips) za kuacha sigara bila kutumia dependancies (sigara za umeme au electronic cigarettes, vidonge vya nicotine au nicotine pills). Kwa lugha ya wenzetu njia hii inaitwa
Cold Turkey. Yaani kuacha sigara kwa
kujiwekea mkataba na mwili wako kwamba hutavuta kwa ajili ya afya yako, uchumi wako na zaidi
MAISHA YAKO.
Mvutaji wa sigara ana chance za kupata aina tofauti za saratani (cancer) 19 hadi 33 kulingana na eneo analoishi pia aina ya uvutaji. Hii ni hatari inayofumbiwa macho kwa kupewa kipaumbele kidogo sana hasa huku kwetu Afica.
COLD TURKEY
Ni njia ya kuacha uvutaji wa sigara kwa
kuachana au
kuepuka kabisa bidhaa zenye nicotine.
Yaani huhitaji chochote cha kuongeza ili kufanikiwa. Ni kusema sasa basi sivuti tena
(NO MORE PUFF!)
Njia hii imekuwa ikitumika duniani kote japo kwa hakika imekuwa ikihesabiwa kama ni njia ngumu ila
YENYE MATOKEO MAKUBWA kupita njia yoyote na haihitaji gharama zozote (
mara nyingi njia hii hukuongezea kipato kwa kuondoa gharama za sigara)
INAFANYAJE KAZI?
Hapa ndi[po wengi wanapokosea na kujikuta wanarudi tena kuvuta sigara, ipo elimu ambayo wengi huikosa hadi kushindwa kufanikisha malengo ya
kuwa na afya njema tena.
HEBU TUANZE SASA KUACHA SIGARA kwa kufuata mtirirkop huu wenye elimu na dondoo muhimu za kukusaidia wewe na unaowajali kurudisha tena afya na zaidi kupata
amani na uhuru kutoka katika GEREZA LA NICOTINE.
1. PANGA TAREHE RASMI
Sikushauri uanze muda huu kuacha sigara yako, hapana, ila unatakiwa kukaa chini na kalamu na karatasi (smartphone au simu yoyote yaweza kuwa mbadala), halafu
toka moyoni mwako, kuwa mkweli wa nafsi yako kwa kuandika
SABABU zinazokufanya uvute sigara, hii inaweza kuwa makundi (youth gangs) rafiki mmoja mmoja, au muda fulani (wengi hupenda kuvuta wakiamka tu) au kama ni occasions (sherehe, makutano, vijiwe). Hii itakusaidia kupanga kwamba hadi lini utakuwa umepata mbadala wa jinsi ya kuanza kuzitambua triggers (kitu kinachokufanya uwashe sigara na kuitia mdomoni.)
2. ANZA MWANZO MWEMA
Baada ya tarehe kupatikana
(nashauri iwe ndani ya siku 21 (ishirini na moja toka ulipoona bandiko hili). Hatua inayofuata ni kuondoa
(ikiwezekana kuharibu na kuvunja) vifaa vyote vya kuvutia sigara
ZIKIWEMO SIGARA ZENYEWE. Hapa sio lazima tuvikute jalalani kwako, hapana, waweza kuamua tu kuviweka mbali na wewe (kumbuka unayepambana naye yuko
mwilini mwako ila
hawezi kuwasha sigara hadi
mikono yako imsaidie). Pia wengine hasa wale waliotumia sumu hii (no citation needed) kwa muda mrefu huamua hata kujipatia kijisafari cha ghafla ili kujaribu kukaa mbali na triggers.
3. SIKU YA KWANZA BILA NICOTINE
Hapa ndipo palipo na ugumu na ndipo wengi
huamua kurudi nyuma, na wengi
tumewahi kuangukia hapa,
(mara nyingine kujaribu na kushindwa bila kukata tamaa ni njia mojawapo ya kuandaa mazingira mazuri ya jaribio lifuatalo) Lakini kumbuka ukishakuwa umejiwekea malengo ya kuacha,
yatimize pale unapoanza ili kupunguza chronic effects (madhara ya kujaribu mara nyingi bila sababu wakati ungeweza mara ya kwanza tu kama
ungepuuza (ignore) kichochezi).
Zipo dalili na magumu (yenye faida) kipindi mtu anaanza kuijali afya yake (mvutaji).
Nitazipanga kulingana na
MUDA
DAKIKA 90 ZA KWANZA
Mwili umeanza kuhisi kukosa
"kitu cha muhimu" ilichokizoea kwa kila siku. Ubongo unaanza kuziamsha nicotine receptors (vipokezi vya kemikali sumu za sigara kwenye ubongo) na hapa mvutaji huyu wa zamani anajikuta anapata
hamu kali zaidi ya kuvuta sigara, ubongo unafuta vitu vyote vya
msingi na kuiweka sigara namba moja. Hii inatokana na bond ambayo nicotine huiweka kwenye ubongo hasa upande wa unconsciousness needs ( yaani mahitaji ya ubongo yasiyoratibiwa na maamuzi yako.)
Dalili
Mwili kuwa mchovu bila sababu
Mdomo kuwa mkavu wenye emptiness (kuhisi kuna kitu kimepungua mdomoni)
Masaa 24 ya kwanza (siku moja)
Hapa mwili unakuwa umepunguiza hadi
64% asilimia ya nicotine kwenye damu (asilimia zinategemea mtu na mtu lakini haiwezi shuka chini ya 51%). Katika stage hii kuna vitu vya kuzingatia ili kubaki halali (hakuna anayependa harufu ya moshi wa sigara). Naposema kuwa halali namaanisha
KUWA BILA SIGARA.
Vitu vya kuzingatia ni
* Epuka vinywaji vyenye
caffeine kwa wingi, kama
kahawa na
soda nyeusi.
Hizi huufanya ubongo kuwa active zaidi na kupelekea mvuta sigara wa zamani (wewe)
kupoteza usingizi na hata kuweza kupelekea sleeping disorders (matatizo ya usingizi).
* Kula matunda yenye asidi (acidic fruits) kwa wingi.
Matunda haya ni kama
zabibu, machungwa, malimao, apples au hata embe japo ina acid kidogo sana. Haya husaidia
kupunguza uhitaji (cravings) wa sigara kwa wakati huo, pia husaidia kumeng'enya (ni kama kuvunja-vunja) nicotine kutoka katika damu yako na kuitoa nje kupitia mkojo. Hii itakusaidia kupunguza pia dalili (symptoms) za kuachana na sigara.
MASAA 72 (SIKU TATU)
Unapokamilisha siku tatu za kwanza bila sigara (nasisitiza
BILA MOSHI WA SIGARA) mwili unaanza
kufuta mahusiano ya matukio au mahali na uvutaji wa sigara, Kile ulichokuwa ukikifanya kwa siku tatu hizi katika muda wa cravings (uhitaji wa sigara) KINAKUWA KIMESAJILIWA KAMA MBADALA RASMI WA SIGARA.
Pia mwili unakuwa na kiwango cha nicotini kisichozidi 7% katika damu na brain receptors
(kumbuka ubongo huanza kuzijenga upya neva zako masaa 3 tu baada ya kupuliza moshi wa mwisho). Vya kuzingatia
USIWEKE TENA SUMU MDOMONI, HAMU YA SIGARA ITAKUSUMBUA TU KWA DAKIKA
ZISIZOZIDI 3 (TATU). Tafuta cha kufanya,
jiweke busy, endelea kunywa maji ya kutosha na matunda yenye asidi. Pia tegemea
hasira na
ghadhabu za bila sababu (ubongo unakuwa unapambana na wewe bila mafanikio NA NI HAKIKA UKIWEKA NIA UNAUSHINDA.)
SIKU 7
Sasa hamu ya kula (appetite) imerudi japo si kwa 100%, sigara inakuja kichwani
mara chache kwa siku (mara 2 mpaka 4) ukilinganisha na siku 3 za kwanza (mara 8 mpaka 100 kwa siku kulingana na ulikuwa
mfungwa wa nicotine kwa muda gani na
ulinunua kiasi gani)
Lakini siku ya saba sigara inaanza kuingia kwenye list ya vitu
vilivyopitwa na wakati katika akili yako. Si kwamba hutaitamani tena,
hapana, ila haitakuwa na nguvu kama siku 3 za kwanza. Hii inatokana na ratiba
mpya ya maisha uliyoianza.
Siku 30 (mwezi 1)
Hongera sasa
huna nicotine kabisa katika mwili wako, na utavuta sigara tu kwa sababu
mwenyewe umetaka (si kwa msukumo wa ubongo).
KUMBUKA SIGARA MOJA TU ITAKUFANYA UANZE MZUNGUKO HUU MWANZONI KABISA,
linganisha kati ya
sigara moja na muda ulioutumia kuziepuka
sigara 90 (mtumiaji wa kawaida huvuta
kuanzia sigara 3 mpaka
pakiti kwa siku, hivyo mara
siku 30 ni wastani wa sigara 90)
JIPONGEZE KWA KUHAMISHIA PESA YA SIGARA KATIKA MAENDELEO YA AFYA YAKO
BAADA YA SIKU 30 MPAKA 45, KAZI HUWA NI RAHISI KAMA KUEPUKA TU KUWASHA SIGARA TENA
MATOKEO YA KUACHA SIGARA (MAZURI NA mabaya KAMA YAPO)
1. Uzito unaongezeka hadi kilo 8 mpaka 15 (kulingana na mtu) hii inatokana na insulin (dereva wa sukari mwilini)
kuanza utendaji kazi tena baada ya
kupokonywa kazi yake na nicotine.
2. Oksijeni (oxygen) (hewa tunayovuta ili kuwa hai) inakuwa
nyepesi zaidi kifuani, huku
mapafu na koo vikiacha utalishaji wa tars (au
makohozi) yasiyo na lazima
3. Furaha halisi inarudi, (sasa furaha
haitegemei kiwango cha nicotine mwilini)
4. Poteza marafiki wavutaji (mimi napenda kuwaita
askari wa gereza la nicotine)
Ongeza za za kwako kulingana na sababu za wewe kuacha.
mods uzi huu usiunganishwe na ule na ikiwezekana uwekwe sticky ili uwe msaada kwa wengi wa Watanzania hasa vijana wanaopotea katika gereza dhalimu la nicotine
N.B muongozo huu ni kwa mujibu wa uzoefu wangu, (
mimi pia nimetoroka gereza hilo la nicotine nilikotumikia kifungo cha miaka minne 4, kabla ya kutoroka
january mwaka huu na sitamani kurudi tena) pamoja na msaada wa internet.
Best Wishes On Your Quitting!!