Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Njia pekee ya kuacha aibu ni kufanyia mazoezi.
Fanya mazoezi ya kuwa jasiri utakavyo.
Fanya mazoezi kwa wanawake wengi uwezavyo.
Ongea chochote na wanawake wengi uwezavyo. Huna cha kupoteza wakati unafanya mazoezi.
Kama utasoma haya na hufanyi mazoezi ni kazi bure.
Pia baada ya muda utaachana na aibu bila hata wewe kujua.
Lakini ujue mambo hubadilika kadri unavyozidi kukua.
Kuwa sehemu mpya kimaisha/ kimahali kuna vitu utagundua bado una aibu navyo. Sio kwamba aibu ikiisha mara moja ndo basi tena hutokua na aibu milele.
Pia ukiacha mazoezi tabia ya aibu itakurudia tu.
Sasa ili kupata urahisi na kujua nini ufanyie mazoezi endelea kusoma.
Jifunze kuongoza mwili wako.
Ongoza mwili wako kupitia akili yako na vitu unavyojiambia.
Badili unachojiambia ili usijikute unafanya kitu usichokitaka. Kama kung’ata kucha/ kuangalia chini ukiwa na mwanamke.
Pia unaweza jaribu kwa kila mtu;
Mwangalie mtu machoni unapoongea naye,
Mwanaume usijikunje kunje/ kujikuna kuna unapoongea na mtu, na,
Jiachie ukiongea, usihofie kuhusu sauti yako au ukisemacho.
Jidake pale mwili wako unapokusaliti alafu uuongoze tena vile utakavyo.
Usichoke kurudia rudia mpaka mwili uelewe kuwa wewe ni jasiri.
Jikumbushe.
Jikumbushe mara kwa mara kuwa unamuangalia machoni.
Jikumbushe kuwa hauna aibu na unajiamini.
Jikumbushe kuwa watu wanapenda wanaojiamini nawe unajiamini.
Jikumbushe kuachana na wasiwasi unaokufanya uwe na aibu.
Jikumbushe kujiachia.
Kama ulivyojikumbusha kuzidisha mbili mara … ukaikariri pia ukijikumbusha kujiamini mwisho wa siku utajiamini tu.
Chukulia ni mchezo unapojifunza.
Usiwe siriazi sana.
Usijiwekee mipaka.
Pia jifunze kupotezea unaposea. waweza jicheka kabisa. Na ukajisamehe.
Ukifanya hivyo utajifunza haraka zaidi kuliko kujiadhibu kila muda.
Ndo mana watu hawapendi hisabati, wanaadhibiwa sana.
Usifiche aibu.
Mficha maradhi kifo humuumbua.
Unaweza mwambia mtu/ mwanamke una aibu.
Unaweza jitania kwa hilo.
Lakini usikalie hilo na kuanza kujishusha au kujidekeza kwa mwanamke.
Pia usiombe mwanamke akufundishe kuacha aibu.
Acha kuwakweza wanawake.
Kuwaona kama ndo kila kitu.
Aibu huanza pale unapoona hustahili kuwa naye. Kwa sababu yoyote ile.
Jifunze kumshusha mwanamke na kumuona wa kawaida tu.
Pia punguza kumfikiria sana.
Na usinga’ang’anie mwanamke mmoja.
Ubongo wako utakusaliti pale unapokutana naye.
Jiendeleze.
Jiendeleze kiuchumi.
Jiendeleze kiakili.
Jiendeleze kimaendeleo.
Mwanaume kadri unavyokua na maendeleo ndio unavyozidi kujiamini.
Hili litakufanya ujisikie mshindi ndani yako. Utamuona mwanamke chini yako. Na hutokua na aibu ukiwa naye.
Wanaume wengi wanatumia njia hii, na wamefanikiwa kuishinda aibu yao. Nawe pia waweza itumia.
Kikubwa ni kuendelea kujijengea uzoefu. Ukiachwa leo sababu una aibu, usiwe na wasi, ukijifunza hayatajirudia tena. Pia kumbuka kujipa muda wa kuishinda aibu yako mbele za wanawake.
Pia jifunze kwa kila mazungumzo/ mahusiano uliyonayo.
Jifunze kwa watu kama Thomas Shelby sio kina Spider Man.