Jinsi ya kuachana na mpenzi

Jinsi ya kuachana na mpenzi

Ushauri na michango yenu, nimeeipenda sana. Nafanyia kazi mukichwa hapa.
 
Mweke wazi sema kweli nayo kweli itakuweka huru ofkoz ataumia bt ukwel lazima usemwe usimchezee kijana wa watu kwa 4yrs then uje umteme wakati time imekata, tafuta sehemu ya utulivu ketin then mpe dozi yake ya quinine! Ila Suprise vp impact ya prisoner imekukumba nn?

Kwa priosoner bado kanipromise anaenda kuongea na first love wake, ila namuombeaje wasielewane, its joke. Tatizo namhurumia huyu kaka na ye anajipa mahope aje, pia nikimwambia ukweli atakasirika na mie sitaki anichunie maana ntaugua, sijui nfanyaje.
 
Mweke wazi sema kweli nayo kweli itakuweka huru ofkoz ataumia bt ukwel lazima usemwe usimchezee kijana wa watu kwa 4yrs then uje umteme wakati time imekata, tafuta sehemu ya utulivu ketin then mpe dozi yake ya quinine! Ila Suprise vp impact ya prisoner imekukumba nn?
Hapo kwenye blue ujue umeniwahi Ciello!
 
mbona simple tu?

Mtoe lunch mle mshibe then mwambie kutokana na a,b,c,d sitoweza kuendelea na uhusiano huuu blah blah blah tutabakia kuwa friends ukipenda.......nakutakia maisha mema uende zako (usisahau kulipia bili ya msosi )

Bra-joe kaipenda hii.
 
Habari zenu lolz. Jamani naomba maushauri jinsi ya kuachana na mpenzi uliechoshwa na mambo yk ya Ajabu2.

Mdada kama una ujasiri wa kifisadi mfate na umpe makavu live. Kama huna huo ujasiri we kula buyu... hakuna kujibu sms zake wala kupokea simu zake ila kama anapajua kwako imekula kwako. becky:
 
habari zenu lolz. Jamani naomba maushauri jinsi ya kuachana na mpenzi uliechoshwa na mambo yk ya Ajabu2.


Kamata hii kitu:

https://www.jamiiforums.com/mahusia...-jinsi-ya-kumwacha-mpenzi-wako-kwa-amani.html



endrelationshipinline.jpg


Ziko njia mbili tu ambazo uhusiano baina ya wapenzi wawili utaandika historia. Ama uhusiano utadumu hadi kifo kiwatenganishe ama utavunjika. Hata hivyo uzoefu unaonyesha kuwa kwa walio wengi hawajaweza kuwa kwenye uhusiano wa kudumu, wanakuwa wamepitia katika mahusiano mengine na hivyo kupitia awamu Fulani Fulani za kuvunja mahusiano.Na kuna namna mbili ambazo uhusiano utavunjika. Ama kwa amani ama kwa ugomvi.

10649-1_n.jpg

Kumaliza mahusiano si kitu rahisi sana hata kama ni hakika umemchoka mwenzi wako na hata kama uhusiano wenu si mzuri kiasi kwamba uko tayari kuwa huru. Kwa hiyo basi, kuvunja mahusiano ya kimapenzi ni jambo ambalo haliwezi kuepukika. Hata hivyo kumaliza mahusiano kwa amani ni vizuri na inapendeza kuliko kuumaliza kwa ugomvi na jazba. Kumbuka "The Golden Rule": Kwamba ungekuwa ni wewe ungependa uachwe vipi? Kama upo katika mahusiano yasiyo na tija na unafikiri kwamba imefika wakati unahitaji uhusiano wenu uvunjike, basi dondoo zifuatazo zitakusaidia kumaliza mahusiano na mpenzi wako kwa amani. Kitu kimoja kikubwa cha kuzingatia ni kuweka Jazba pembeni:

phpThumb.php

1. Kuwa Na Uhakika Na Unachotaka Kufanya: Kama huna uhakika juu ya hisia zako kwa mwenzi wako unapotaka kuvunja uhusiano bora usifanye hivyo maana utafanya moyo wako usiwe na maamuzi dhabiti aka “Maamuzi magumu”. Kama una hisia naye pia itamfanya achanganyikiwe na ajisikie kuwa bado anayo nafasi ya kuwa na wewe ama anaweza akaamua na yeye kukukomoa na kukuacha kabisa wakati kumbe bado una hisia za mapenzi na yeye . Hata hivyo kama una uhakika kwamba ni kweli hauutaki uhusiano uliopo basi kuwa tayari kukata kabisa mahusiano yenu la sivyo kuwa tayari kukiona cha moto . . . maana utakuwa unachezea hisia zako.

End-your-Relationship.jpg

2. Fikiria Sababu za Kuvunja Uhusiano: Uhusiano unapovunjika mara nyingi ndugu, jamaa na marafiki wanapenda kujua sababu. Unapojua sababu zinazopelekea wewe kuvunja mahusiano itakusaidia kutoa majibu ya uaminifu pale unapoulizwa. Pia itakusaidia kumaliza mahusiano katika namna njema. Hata kama mwenzi wako hataamini au ataamini juu ya kuvunjika kwa uhusiano wenu, kuwa honest au mkweli ni muhimu. Mweleze unahitaji kusonga mbele na maisha yako bila yeye na mjibu maswali yote kwa uaminifu. (Fikiria huko nyuma kama uliwahi kuachwa bila sababu ulivyojisikia)

302797-4471-54.jpg

3. Maliza Mahusiano Wewe Binafsi: Kama umekuwa na mpenzi wako kwa muda mrefu au kuipindi chochote ambacho uliwekeza muda na nguvu zako za kujenga mapenzi, basi ni busara mahusiano hayo yakamalizwa na mwenyewe binafsi. Usitumie njia yoyote ile zaidi ya wewe mwenyewe, usitumie SMS, usitumie IM “Chat”, usitumie simu au email au barua au mtu yeyote kufikisha ujumbe. Ukitaka kumaliza mahusiano kwa amani, tafuta muda wa kukaa na mwenzi wako in person au face to face ili kuumaliza uhusiano huo katika hali njema.



4. Chagua Mahali Panapofaa. Mahali pazuri panapofaa ni pale ambapo wewe unayetaka kumwacha mwenzako ungekuwa wewe unaachwa ungependa iwe mahali gani ili uelezwe? Be on his/her shoes. Public Places si mahali pazuri sana kwani mwenzi wako anaweza kujisikia kadhalilishwa. Kama ukiweza chagua mahali patakapomfanya mwenzi wako awe confortable na kurelax kama yuko nyumbani kwake.


slide-138.jpg

Angalizo: Kama una uhakika kuwa mwenzi wako anaweza kuleta ukorofi, basi chagua Public Place kama kwenye restaurant ambapo wapo watu wengine. Hii itasaidia kuondoa uwezekano wa kuleta vurugu. Public Place patakufanya ujiamini. Pale mambo yatakapochachamaa unaweza kuondoka tu bila tishio la ugomvi kwa kuwa kuna watu. Ukiona hali si shwari ni vema uanze kuondoka wewe kuliko yeye kuondoka kwanza.


ending-relationships.jpg

5. Msikilize Mwenzi Wako: Hata kama umeshaamua huwezi kubadili mawazo juu ya kuvunja mahusiano yenu haina maana kuwa usimsikilize mwenzi wako. Kumsikiliza mwenzi wako kutamfanya mwenzi wako atoe yote aliyokuwa nayo moyoni kitu ambacho kwa uhakika kitasaidia kumaliza mahusiano kwa amani. Pia unaweza kujifunza baadhi ya mambo ambayo yatakusaidia katika mahusiano yako yanayofuata.


breakuptest.jpg

6. Kuwa Mpole Na Dhibiti Hisia Zako: Moja ya sababu kubwa ya mahusiano kuvunjika ni pamoja na wahusika wote kutokuwa na furaha na amani na mwenzi wako. Wakati wa kuvunja mahusiano hayo pia yanaweza kujitokeza hasa pale mtakapoanza kulaumiana na kuonyeshana vidole ni nani mwenye makosa. Hakikikisha unadhibiti hasira hisia zako na hasira hata kama anachoongelea mwenzio kitakutia hasira. Ukifanya hivyo utafanikisha kuwa na mazungumzo ya amani.


couples-dissagrement.jpg

7. Kuwa Mtulivu na Makini: Unahitaji kuumaliza uhusiano na kuondoka mahali mlipo. Hata hivyo ni busara kuwa mtaratibu na mpole. Kama kuvunjika kwa uhusiano wenu kutakuja kama Suprize kwa mwenzio, basi bila ya shaka atahitaji muda wa kuyameza unayomwambia, kuyatafakari ili aende sambamba na wewe katika mazungumzo yenu. Inaweza ikawa si habari njema kwa mwenzi wako kwa hiyo utulivu wako na upole katika maongezi yenu kutamfanya apunguze maumivu.


Get-Back-With-Your-Ex.jpg

8. Mkimaliza Maongezi Ondoka Haraka: Iko hivi: Kwa kiasi kikubwa anayeachwa anaweza kuwa alikuwa hajui kuwa ataachwa kwa hiyo hatakuwa na furaha kwa yeye kuachwa. Anaweza akakulaani sana na kukuita majina yote mabaya anayoyajua na hivyo kukufanya na wewe uwe na hasira. Tulia. Jizuie. Kwa kuwa umeshaongea na pia umemsikiliza kistaarabu, huna haja ya kuendekeza ugomvi au malumbano. Ondoka. Hakuna faida utakayoipata kwa kuendelea kutoa maelezo yoyote ya ziada. Kama ni mwelewa na mmemaliza maongezi kwa amani basi mwage na nenda zako.


Broken%20heart.png

Je, ni nini uzoefu wako kuhusu kuacha au kuachwa katika mahusiano mbalimbali uliyopitia? Na je, kuna lolote la kujifunza?



Nawakilisha Na Nitarudi Kuna Mdada wa JF kaomba lift:


superman700cropped.jpg

 
Mmh hii ngumu lakini usitumie simu eti nenda physically, looo cna huo uthubutu aisee
 
Kubadili mpenzi si suruhisho la matatizo ndani ya ndoa bali ninachosema kaeni chini tatueni tatizo/matatizo yenu
 
Mbona easy hyo mwite mweleze ukwel then kata mawasiliano naye akiona umempa cold sholder mwenyewe atajistukia!! Ila ukaze kwelkwel kuonyesha uko real
Huyu ntu siyo strong kwenye maamuzi ana aibu,kwahiyo mwambie akili yangu imenituma nijiunge na watawa (celibacy) so no moore fu......g!!!!!!!!!
 
huyu mtoa mada kama alikua kwenye akili yangu, kiukweli me nimechoka kumchezea kijana wa watu , bt yeye ni tofauti he is so innocent kumbwaga naona aibu na kuendelea kumchezea i fil guilt so na mimi mnishauri tu nitumie njia gani isiyo na madhara, nimvizie tukiwa out nimpe live, au nitume sms au nimpigie lakini nataka anielewe na asikasirike coz bado nautamani mchango wake kwenye maisha yangu, sio financially pls
Duh! Mshika mbili hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom