Jinsi ya Kuandaa Questionnaire ya Research yako na vitu vya msingi vya kuangalia

Jinsi ya Kuandaa Questionnaire ya Research yako na vitu vya msingi vya kuangalia

FestoKaguo

Senior Member
Joined
Apr 1, 2022
Posts
128
Reaction score
202
Moja kati ya hatua muhimu sana unapokuwa kwenye process ya kufanya research, especially hii aina ya quantitative huwa ni kipengere cha kuandaa questionnaire. Lakini ukweli ni kwamba kuandika questionnaire huwa siyo tu kitendo cha kuamka unakukusanya maswali kama unavyoonaga walioandaa na kukuletea ujaze au uyajibu nali huwa kuna kaprocess na pia huwa kuna muundo, mantiki na uhusiano wa moja kwa moja na research objectives zako.

Kwahiyo inabidi utambue kwamba kabla hujaandaa questionnaire, unahitaji kuwa na vitu vitatu vya msingi kutoka kwenye hiyo research yako kama ifuatavyo;
1️⃣ Title ya research
2️⃣ Objectives za research yako
3️⃣ Research design and methodology ( hapa tunaangalia aina ya data unazotaka kuzikusanya, population unayoilenga kama ni wasomi n.k, sampling method n.k.)
Hapo nafikiri utakuwa umeanza kunipata pata kidogo na nataka twende kwa mfano huu maana kuna research nilikuwa naifanya hapa title yake ni "Exploring the Impact of Fintech Adoption on Customer Trust in Retail Banking”
Sasa kupitia title ya hiyo research hapo niliweza kupata objectives tatu ambazo ni hizi hapa
1️⃣ To determine the relationship between fintech adoption and customer trust
2️⃣ To assess the impact of fintech usage on customer loyalty
3️⃣ To explore the challenges customers face in trusting fintech systems

Hivyo basi kupitia hizo objectives tatu hapo ndio nikaweza kuanza kupatumia kuandaa hiyo questionnaire au dodoso langu kama wanavyoita wataalamu wa lugha ya kiswahili.
Niliandaa section kuu nne ambazo ila section ilikuwa ina reflect objective moja na hizo section ni;
Section A niliweka hii inaitwa
Demographic info ya respondent yaani hapa utakutana na maswali kama gender, age n.k
Section B nikaweka hii inaitwa Matumizi ya fintech (apps, mobile banking, digital payments) lengo kuu lilitaka kutambua kuhusu experience ya watu juu ya matumizi ya hizo app

Section C nikaweka Maswali ya ku-measure trust & loyalty kwa kutumia Likert scale hapa ndio unakutana na yale maswali ambayo majibu yake yanakuwa yana strong agree, au strong disagree
Section D nikaweka hii heading ya
Changamoto au vikwazo vya kuamini fintech nikitaka nijue ni vitu gani watu wanaviexperience kwenye kutumia huduma hizo za fintech company.
Sijaelezea kuhusu population na sample size yangu ilivyo ila ukirudi kwenye objectives zangu kuna namna zina relate na hizo title hapo ambapo kwenye kila title kunakuw ana maswali yake matatu au manne yanayoulizwa kwa watu na majibu watakayotoa yanakuja kuvalidate objective yangu na kunisaidia kutatua au kupata jibu la swali langu.
​
Mfano wa swali kwenye Section C ambayo inalezea kuhusu kumeasure trust and loyalty kwa hao customers linaweza kuwa:
🟩 “Je unajiona ukiwa salama unapotumia huduma za kibenki kwa njia ya simu.”
Then respondent atachagua moja kati ya: Strongly Agree, Agree, Neutral, Disagree, Strongly Disagree
Kwahiyo sasa mambo ya kuzingatia kabla ya kuandaa questionnaire yako ni haya hapa: 👇👇👇​
  • Kwanza kabisa Soma objectives zako kwa kina na kila swali lako lazima liwe lina-measure kitu kutoka kwenye objective yako/zako.​
  • Pili, hakikisha design ya questionnaire ina-flow vizuri (demographics hadi behavior hadi perception)​
  • Tatu, tumia Likert scale ili kupata data na taarifa ambazo zinakuwa ni rahisi kuzimeasure.​
  • Kabla ya kuipeleka kwa wahusika questionnaire yako hebu ifanyie pilot test kwanza yaani wape watu wachache wakusaidie kujibu ili uone ni maswali gani ni irellevant uyatoe hivyo hii itakusaidia kubaini kama maswali yanaeleweka​
Mwisho kabisa cha kuzingatia hapa ni kwamba Kwenye proposal yako, sehemu unazopaswa kutumia ili kuandaa questionnaire ni pamoja na:​
  • Research objectives​
  • Research methodology (aina ya data, sampling, instruments utakazozitumia kufanya analysis)​
  • Research questions ( Ikitokea umetumia)​

Kila questionnaire nzuri hutokana na alignment nzuri ya title, objectives, na aina ya data unayokusudia kukusanya. Bila hivyo, utajikuta unakusanya majibu ambayo hayana maana kwa analysis yako.​

Nifunge kwa kusema kama unahitaji msaada kuandaa questionnaire yako kwa ajili ya research ya degree au project ya kisomi niko tayari kusaidia. Nitafute WhatsApp 👉 +255 765 772 976
 
Back
Top Bottom