Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Nimeona hapa JF watu wengi wakija na kusema wanahitaji wabia/wawekezaji kwa miradi au biashara anuai.Katika mialiko yao hio wengi walikuwa ama wakisema uje PM for details na unapofika PM unajikuta ado hawajajiandaa kikamilifu.Wengi unakuta wana wazo zuri ila hawajaliweka vizuri.
Leo nataka tujadili namna na umuhimu wa kuandika Investment Proposal/Business Proposal/Project Proposal au kwa kiswahili (Andiko la Wazo la Biashara/Mradi/uwekezaji).Unapoandika andika wazo lako ni muhimu ukatambua kwamba namna ya uandishi inategemea na lengo la wazo lako.Hata hivyo kuna maeneo ya msingi ambayo lazima uyazingatie katika kuandaa wazo lako.
Ni muhimu kutambua kwamba Andiko la Wazo sio mpango wa biashara ingawa kuna maeneo mengi ambayo yatakuwa na ufanano.Andiko la wazo linalenga zaidi kumvutia na kumuonesha mlengwa uzuri na upekee wa wazo lako wakati Mpango wa biashara unalenga kuonesha namna ambavyo wazo au mradi utatekelezwa.
Wazo la biashara ni lazima liwe na vipengele vifuatavyo:
Ni muhimu kutambua kwamba kila eneo hapo linahitako maelezo ya kina na taarifa za uhakika ambazo mlengwa anaweza kuthibitisha pasi na shaka yoyote.Mbia makini atataka kufahamu kwa kina iwapo uliyoandika yana ukweli hivyo ni muhimu kuhakikisha kwamba unaweza thibitisha taarifa zote unazoweka katika andiko lako.

- Maelezo mafupi na ya msingi kuhusu mradi husika
- Maelezo ya wasimamizi,wadhamini na wasifu wa wasimamizi
- Maelezo ya historia ya wazo husika
- Maelezo ya masoko na mauzo yanayotarajiwa kufikiwa pamoja na wateja wanaolengwa kuhudumiwa
- Maelezo ya utaalamu unaohitajika na rasilimali zinazohitajika
- Maelezo juu ya faida za mradi kwa mazingira na jamii
- Maelezo ya madhara kwa mazingira na jamii na namna ambavyo yatashughulikiwa
- Maelezo ya kiwango cha fedha,mteja au uwekezaji unaohitajika na faida inayotarajiwa kupatikana
- Maelezo kuhusu uhusika wa serikali,kama vile sheria,vibali n.k.
- Ratiba ya hatua ya utekelezaji wa mradi husika na muda wa utekeleza wa kila hatua