Kuangalia madeni yako ya makosa ya barabarani (Traffic Fines) kwa urahisi na haraka, unaweza kutumia njia zifuatazo:
1. Kupitia Tovuti (Online)
- Hatua ya 1: Fungua kivinjari (browser) kwenye simu yako na tembelea tovuti rasmi ya RTOC au TMS Check.
- Hatua ya 2: Chagua aina ya taarifa unayotaka kutumia (kama vile Namba ya Usajili ya Gari au Namba ya Leseni ya Udereva).
- Hatua ya 3: Ingiza namba hizo kwenye kisanduku husika na ubonyeze kitufe cha "Search" ili kuona kama kuna makosa yaliyosajiliwa na faini unayodaiwa
2. Jinsi ya Kulipa Faini Hizo
Ukigundua una deni la faini ya barabarani, unaweza kulilipa moja kwa moja kupitia simu yako bila kwenda polisi:
- Namba ya Kampuni (Biller Number): 001001
- Namba ya Kumbukumbu: Weka Namba ya Malipo/Kumbukumbu uliyopewa kwenye mfumo wa TMS (Control Number).
- M-Pesa: Piga *150*00#, chagua "Lipa kwa M-Pesa", kisha chagua "Malipo ya Kampuni".
- Airtel Money: Piga *150*60#, chagua "Lipa Bili" kisha chagua "Faini za Polisi" au ingiza namba ya kampuni moja kwa moja.
Wengi mna magari yenu, yanatembea na madeni na mwisho wa siku mnaishia kusumbuliwa na askari wa usalama barabarani