Kidagaa kimemwozea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 3,680
- 6,554
Kwa mana rahisi tunaweza kufasili duka la mtandaoni kuwa ni jukwaa maalumu kwaajili ya kuuzia bidha au huduma mtandaoni. Mfano wa maduka ya mtandaoni ni Amazon, Ebay, Jumia market, na Kikuu .Bidhaa unazoweza kuzifungulia duka mtandao ni, vitabu, vifaa umeme, mavazi na kadhalika. Zipo faida mbalimbali za kuendesha duka mtandao kwaajili ya kuuza bidhaa zako kama vile, kutokuhitaji gharama kubwa, wateja kutoka sehemu mbalimbali, na pia unaweza kuliendesha ukiwa popote.
Mahitaji muhimu kwaajili ya kuanzisha au kufungua duka mtandaoni; Yapo mahitaji muhimu ambayo yatasaidia duka lako kukamilika na kuwa mtandaoni mambo hayo ni pamoja na,
Platform; Kama ni duka la kawaida/kienyeji basi hii nikama ardhi ya kujengea duka lako hivyo hapa tuiite ardhi mtandao kwaajili ya kutengenezea duka lako. Zipo platform mbalimbali kwajili ya kutengeneza duka lako kama vile Wordpress, Joomla na nyinginezo.
Uendeshaji(Hosting) Hii ni huduma itakayoendesha duka lako nakulifanya lionekane mtandaoni na kwa usalama. Yapo makampuni mbalimbali yanayotoa huduma hii kwama vile Hostinger nakadhalika
Jina miliki (Domain name) Hili nijina maalumu kwaajili ya duka lako na hukaa katika kiungo(link) Kwa lugha nyepesi tunaweza kusema ni njia ya kuja dukani kwako, majina haya huambatana na vikoa kama vile .co, .net na kadhalika. Zipo kampuni mbalimbali ambazo ndizo huuza majina yenye vikoa hivi ambazo ni pamoja na Godady,na Google,
Mambo ya muhimu yanyotakiwa kuonekana katika duka mtandao lako
Mosi, Mwonekano mzuri unaovutia pamoja na mfumo rahisi wa kununua na kulipia bidhaa; Wateja hupendelea maduka mtandao yanayovutia pamoja na maduka yenye njia rahisi za kufanya malipo hivyo ni muhimu kulizingatia hili. Kuhusu nji za kufanya malipo unaweza kuingia ubia na makampuni yanayojihusisha na kutoa huduma hizo au malipo yakaja moja kwamoja katika akaunti za kibinafsi.
Pili, Weka sera ya faragha na umhakikishie mteja usalama wa njia zake za kufanya malipo kama vile ulinzi wa taarifa za siri atakazoziweka katika mtandao wako. Hii hujenga uaminifu kwa mteja na kutokuogopa kufanya miamala ya kifedha katika duka mtandao lako.
Tatu, Sera ya kurudisha fedha, katika duka mtandao lako nilazima sera hii iwepo ili mteja ajue ikiwa anaweza kurudisha bidhaa aliyoinunua na kurejeshewa fedah yake au la!
Nne, Mawasiliano na maelezo kuhusu duka hilo, Mawasiliano ni muhimu sana katika duka mtandao pale mteja atakapohitaji usaidizi katika kununua bidaha au ikiwa anamalalamiko fulani. Maelezo kuhusu duka hilo na maelekezo kuhusu ofisi au wanapopatikana watoa huduma wa duka hilo ni muhimu kwani hujenga uaminifu.
Tano, Ukurasa wa msaada kwa wateja; huu ni ukurasa maalumu ambapo mteja huweza kutafuta majibu ya maswali yake mfano, kama bidhaa haikumfikia afanye nini? Hivyo ukurasa huu ni muhimu sana.
Sita njia ya usafirishaji wa bidhaa; Ili mteja aweze kununua bidhaa kwako nilazima ajiulize bidhaa aliyoinunua itamfikiaje? Hivyo ni muhimu katiaka duka lako kuwe na njia za kusafirisha bidhaa za wateja. Unaweza kuanzisha huduma hii wewe au ukaingia ubia na makampuni ya usafirishaji kwaajili ya kusafirisha bidhaa za wateja.
Bidhaa utakazopakia katika mtandao wako nilazima ziwe na taarifa zifuatazo,
Jina la bidhaa; Nimuhimu kuweka jina halisi la bidhaa napia ni vizuri kufanya utafiti kuhusu maneno msingi/keywords hii itakusaidia kuleta wateja watakao tafuta bidhaa hiyo kutoka mitambo tafutishi kama Google
Picha nzuri ya bidhaa inayovutia ; hakikisha unapakia picha ya bidhaa yenye mwonekano mzuri lakini halisia
Maelezo ya kutosha kuhusu bidhaa. Nilazima uweke maelekezo au maelezo kuhusu budhaa husika hii itakusaidia pia kuleta watafutaji kutoka mitambo tafutishi.
Muhimu, Kumbuka uuzaji wa mtandaoni katika duka binafsi linachangamoto zake hivyo inaweza kukuchukua muda kuanza kuuza bidhaa lakini mikakati kabambe kam akuanza kutangaza duka lako inaweza kuondoa changamoto hiyo. Unaweza kutangaza bidhaa za duka mtandao lako katika makampuni makubwa ya matangazo kama vile Google adwords, Facebook na kadhalika
Logo ya duka mtandao la Amazon, picha na mtandao

Upvote
6