Mimi mwenyewe mpira sijui kabisa, ila siku hizi nimeanza kubet na nakula kila siku hela ndogo ndogo.
Nilichogundua, usiwe na tamaa ya kupata mapesa mengi, manake kubashiri matimu 13 kwa usahihi sio kazi ya kitoto.
Nimewauliza wakongwe wa kubet,wingine ananiambia ana miezi minne hajala hata mia na kila siku anabet kwa sh 500. Lakini mimi nikiweka buku buku kwa timu 3, lazima nitoke na hela.
Siujui mpira, sasa nafanyaje! Ni kweli sijui kabisa mpira, yaani wachezaji wa ulaya kwa ujumla wake ninaowajua hawazidi 15, nawajua tu rondomly na sijui wanatokea timu gani! Sasa nafanyaje?
Nanunua bundle, nazisoma timu husika mtandaoni, napata jibu, nalinganisha na pointi za kampuni husika, halafu mimi nakuwa mwamuzi wa mwisho, then naweka dau.
Siku za kwanza nishawahi kuliwa 4000, nilikuwa naangalia timu yenye mapesa mengi.