tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Uzalendo na uwajibikaji ni mambo ambayo yanapaswa kwenda sambamba kwani moja likilegalega, jingine huenda mrama. Ili kujenga uzalendo wa dhati na wa kudumu katika nchi hii, ni lazima uzalendo huo uanzie kwenye uongozi wa juu. Katika familia, baba na mama wanapaswa kuwa mfano bora kwa watoto wao kwa kuenenda vema ili watoto wao wanakiri mwenendo mwema kutoka kwao. Ikiwa wazazi wana mwenendo wa ajabu, ni rahsi watoto wao kuwa na mwenendo sawia kwani mtoto wa nyoka ni nyoka.
Katika nchi hii, suala la uzalendo limekuwa likipigiwa kelele upande mmoja tu huku upande wa pili ukiwa hauguswi. Siku zote viongozi wanatuhimiza kuwa wazalendo, wawajibikaji na kuipenda nchi yetu. Hadi wamefika hatua ya kuwalazimisha vijana waliohitumu kidato cha sita kwenda JKT kujifunza uzalendo. Lakini viongozi hao wanaodhani uzalendo unajengwa na JKT, nao wamepita huko. Cha kushangaza wengi wao hawana uzalendo hata chembe!
Ukitazama kwa jicho lisilokuwa na makengeza, utagundua uhimizaji huu unaegemea upande wa chini zaidi kuliko juu. Kwa mfano, utakuta kigogo mkubwa tu ametapanya matrilioni ya fedha za serikali ama kwa tuhuma zilizo wazi au baada ya ufisadi huo kuibuliwa na CAG, lakini hatua hazichukuliwi dhidi yake. Na kama zikichukuliwa zinachukua muda mrefu hadi mtuhumiwa au fisadi anaharibu ushahidi.
Aidha, wale wanaofanikiwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ama huachiwa huru kwa kisingizio cha ‘kukosa ushahidi’ au wakikutwa na hatia hupewa adhabu ndogo ukilinganisha na kiasi cha uhalifu waliofanya. Kwa mfano, mtu kaiba fedha za umma au kaisababishia serikali hasara ya Tsh bilioni 5 lakini inapotoka hukumu huamriwa kulipa faini ya Tsh milion 5 tu! Uwiano uko wapi? Kwa namna hii ufisadi utakomaje katika nchi hii? Nafikiri pia watunzi wa sheria (wabunge) na wale wanaozisaini hawana uzalendo wa kutosha. Wanatunga sheria laini zinazowalinda kwa sababu wanafahamu wao ndio vinara wa utapanyaji wa rassilimali za umma.
Kwa sababu hii, watu hawawezi kuwajibika kufuata sheria na taratibu zilizopo. Bila shaka kabla ya kufanya ufisadi wezi hupitia kwanza sheria na kuona ni wapi penye matobo na kisha kutumia mwanya huo kufanya ufisadi wa kufuru. Ni dhahiri sheria zetu hazitungwi kizalendo.
Ninapoongelea suala hili la uzalendo na uwajibikaji sigusii muhimili mmoja tu; la hasha! Mihimili yote mitatu, yaani serikali, bunge na mahakama, inahusika kuanzia chini hadi juu. Na hii inatokana na watunga sera na viongozi kutoonyesha mifano ya uzalendo itakayoigwa na kila mtanzania. Msisitizo wangu hasa upo kwa uongozi wa juu wa hii mihimili yote mitatu. Ikiwa viongozi wa juu wataonyesha uzalendo na uwajibikaji, sina shaka watumishi wa kada za chini pamoja na wananchi wa kawaida watafuata mkondo huo huo.
Tukija kwenye halmashauri zetu, kwa mfano, unakuta mkurugenzi anashirikiana na mweka hazina kutafuna mapato ya halmashauri, wakati watumishi waliopo chini yake wanapata shida kila kukicha. Fikiria maofisa ugani na walimu hawana vitendea kazi vya kuwafikia wakulima na kufundishia, mtawalia, ilhali fedha za halmashauri zinatafunwa na mkurugenzi. Na bahati mbaya taarifa zikifikishwa kwa mkuu wa mkoa au wilaya hawachukui hatua zozote ama kukemea au kushughulikia wahusika.
Kwa hali kama hii, tutarajie watumishi wengine nao kuiga mfano huo huo. Ofisa ugani naye ataiba mbolea za ruzuku za wakulima au mwalimu atauza chaki za shule ilmradi naye aambulie chochote. Utovu wa uzalendo ni kama kansa ambayo ikishakamata kiungo kimoja cha mwili na isipodhibitiwa kwa wakati, itasamabaa mwili mzima na hatimaye kusababisha kifo. Kwa maana hiyo, uzalendo sharti uanzie kwa viongozi wa juu ili viongozi wa chini na wananchi nao wawaige.
Ikiwa kiongozi mkuu atakuwa mnyoofu na wasaidizi wake pamwe, kila kitu kitakwenda sawa. Kinyume chake ni maafa na maangazmizi ya kitaifa. Ni sawa na kumuona mpuuzi mmoja anatoboa mtumbwi mkakaa kimya; kinachofuata ni wasafiri wote kuzama na kuangamia!
Tukirejea kwenye muhimili wa bunge nako mambo ni yale yale. Posho ya mbunge kwa siku moja ni Tsh 300,000. Mshahara wa mwalimu kwa mwezi Tsh 250,000. Aidha, mbunge akistaafu baada ya miaka 5 anapata kiinua mgongo Tsh milioni 400 huku mwalimu akilimwa kikokotoo na kuambulia Tsh milioni 15 tu! Uwiano uko wapi? Mgawanyo wa maslahi usio linganifu kama huu unadidimiza uzalendo na kuchochea vitendo vya ufadhirifu wa mali za umma.
Mbunge wa zamani wa Mwibara, Kangi Lugola, alivyotetea maslahi ya wabunge kuhusu kukatwa kodi ya mapato ya viinua mgongo (Chanzo: Youtube)
Kwa kuwa mtumishi anapunjwa kiasi hiki, siku zote atakuwa anawaza kuiba ili walau alingane na mbunge. Kujenga uzalendo na uwajibikaji katika mazingira kama haya, itakuwa vigumu sana. Lazima serikali iangalie namna nzuri ya kuwathamini watumishi wa chini badala ya kuwarundikia rasimamli vigogo na wanasiasa huku watumishi wa chini wakiendelea kuishi maisha ya kuhudhunisha wakiwa kazini na baada ya kustaafu.
Kana kwamba ukosefu wa uzalendo katika hiyo mihimili miwili hautoshi, ukija upande wa serikali ndiko kuna kufuru kabisa. Fikiria waziri analipwa mshahara wa kufuru na analipwa posho ya kujikimu, nyumba, mafuta, vitafunwa, viburudisho, safari na posho nyingine kedekede huku walimu huko mashuleni wanalipwa mshahra sawa na posho ya mafuta ya siku moja ya naibu waziri. Uzalendo wa mwalimu utatoka wapi hapo?
Walimu hawalipwi posho ya kufundisha, hawalipwi fedha za likizo wala kuthaminiwa na mwajiri. Halafu mtu anatoka kusikojulikana anakuja kuwaambia walimu kwamba serikali inashindwa kuwalipa posho ya kufundisha kwa sababu idadi yao ni kubwa…..kwamba serikali ikiwalipa walimu wote posho za kufundisha, itafilisika! Hii sio hoja ya kizalendo bali inakatisha tamaa na kuvunja moyo wa uwajibikaji.
Waziri aliyetamka maneno haya alitakiwa akemewe na awaombe radhi walimu kwa kuwadharau na kuwabagaza Maneno ya kejeli kama haya ndiyo yanachangia kuvunja watumishi morali na kuua nguvu ya uzalendo na uwajibikaji miongoni mwao.
Viongozi wa ngazi za juu wanapaswa kuonyesha uzalendo si kwa kufanya ulinganifu wa maslahi tu, bali hata kwa kauli zao chafu dhidi ya watumishi na wanachi wa kawaida.
Nimeona niyaseme haya kwa uchache na kwa ufupi ili kuonyesha jinsi ambavyo uzalendo katika nchi unashuka kutokana na viongozi wa juu kutokuwa wazalendo na kuwa mfano bora wa kuigwa na pia mambo ambayo yakifanyika yataongeza na kuchochea chachu ya uzalendo miongoni mwa wananchi, lengo kuu likiwa kuboresha ustawi wa kila mtanzania bila kujali hali yake kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.
Nawasilisha.

Upvote
2