Jinsi ya kudhibiti hisia zako

Jinsi ya kudhibiti hisia zako

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
JINSI YA KUDHIBITI HISIA ZAKO
Nifanye nini ili kuhakikisha sina hisia mbaya?

control_thinking.jpg


Unajua jinsia ya kuepukana na fikra mbaya? Je unaweza kudhibiti hisia zako? Jinsi ya kukabiliana na hisia zako?

Tunapozungumza juu ya kudhibiti hisia zetu, basi tunapaswa kuongelea juu ya imani. Jambo ambalo ni muhimu sana ambalo unatakiwa uwe makini nalo ni imani yako na jinsi unavyoongea na nafsi yako mwenyewe. Mawazo na fikra ambazo zimo katika kichwa chako ndiyo nguvu kali sana zinazoweza kuwa ndiyo sababu ya kukuletea hisia ambazo sasa unazo.

Wanafunzi huonyesha kwamba asilimia kubwa ya fikra za watu wengi ulimwenguni ni mbaya na asilimia saba (7%) ya fikra hizo husababisha msongo wa mawazo na matatizo ya moyo. Unapaswa uulize kama asilimia kubwa ya fikra za watu sio nzuri basi ni vipi kwa wale wanaoishi na amani, furaha na maisha ya mafanikio?


positive_thinking.jpg


Watu wa aina hii wamejifunza siri za kukabiliana na hisia zao kwa kudhibiti fikra zao. Wengine hufanya kwa kujua na wengine hufanya bila ya kujua. Asilimia kubwa ya imani zao huiamini mambo mazuri tu na huwa makini na kuhusika na mambo mazuri siku zote katika maisha yao.

Unahitaji kujifunza njia za kuepukana na fikra mbaya na kujifunza njia za kubadili mwenendo wako ili uweze kutazamia juu ya mambo mazuri na mambo unayohitaji ili uweze kukamilisha malengo yako katika maisha.

Imeonekana kuwa 90% ya imani zetu hujitengeneza katika umri wa miaka 7 na mpangilio huu unahitajika sana kutoka kwa wazazi wetu kisha marafiki na ikifuatiwa na vyombo vya habari kama vile Radio, TV, Computer N.K. kama mtoto amejengewa mawazo ya kujifikiria

mwenyewe kama vile "Mimi ni mpumbavu” au "mimi nina sura mbaya” hali hii atakuwa nayo mpaka ukubwani na ndiyo itakuwa imani yake siku zote kuwa yeye ni mpumbavu au ana sura mbaya au vinginevyo kulingana na alivyozoeshwa. Nitakupa mfano mdogo ulio hai

kabisa. Kihistoria inasabikika kuwa yule aliyekuwa mwanamziki maarufu ambaye kwa sasa ni marehemu Michael Jackson, wakati akiwa mdogo mzazi wake alikuwa akimbeza sana kuhusu pua yake nakuambiwa kuwa ana pua kubwa hadi kufikia kupewa jina la "babu

mapua”. Hali hii ilimgusa sana hivyo ilimjengea imani hiyo kuwa yeye hana pua nzuri hivyo athari yake ilikuja kuonekana baadaye pale alipopata uwezo wake binafsi na kubadili kile aliochokiona kwake kuwa ni kibaya. Wazazi na walenzi ndiyo msingi bora wa ukuaji wa

vijana wetu hivyo wakiamua kutengeneza basi hutengeneza vizuri na wakiamua kuharibu basi huharibu kweli kweli. Hivyo kumbuka kuwa umri huu sio wa kumjengea mawazo mabaya kijana. Samaki mkunje angali mbichi!



Jinsi ya kukabiliana na hisia zako:


Kujifunza jinsi ya kudhibiti hisia zako na kuondoa fikra mbaya, fuata hatua hizi hapa chini:
1. Angalia jinsi unavyojiona na kusema wewe mwenyewe
2. Angalia jinsi unavyoonekana na kuongea na rafiki zako au familia yako.
3. Angalia jinsi watu wanavyokusema.

Ukidhibiti fikra zako, jinsi unavyojiona na kusema, jinsi watu wanavyokusema, ndipo utakapoweza sasa kukabiliana na hisia zako. Gundua kuwa huwezi kuwa na hisia bila ya kuwa na fikra. Mwanzoni inaweza kuwa ni ngumu, lakini kwa mazoezi ya kudumu, utakuwa na uwezo wa kuondoa fikra mbaya na kukabiliana na hisia zako.

Siku zote kumbuka kuwa ukitaka kubadili maisha yako, anza kwa kubadili maneno yako. Anza kuongea maneno yanayohusu ndoto zako za kuwa nani unapenda uwe hapo baadaye, na wala sio maneno ya hofu na kufeli.
&#8203;[/SIZE]]JINSI YA KUDHIBITI HISIA ZAKO - PERSONAL DEVELOPMENT <!--if()-->- <!--endif--> - Publisher - Staryte - Education, Entertainment & Development
 
hii nimeikubali mkuunimejaribu pia kupitia hiyo link chini ya hii makala,kiukweli nimejifunza kitu kipya katika maisha yangu
 
Back
Top Bottom