GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Mtu mmoja aliomba, "Mungu, naomba unibariki mimi na mke wangu na mtoto wangu John na mke wake. Sisi wanne tu, na si zaidi"
Hiyo inatoa picha jinsi binadamu alivyo mbinafsi kwa asili. Ndiyo maana watu wengine hupika kiwango cha ustaarabu wa mtu kwa kuangalia kiwango ambacho amefanikiwa kuushinda ubinafsi.
Kwa kuwa ubinafsi ni hali ya kawaida ya binadamu, nitakujulisha njia mbili zinazoweza kukusaidia kuushinda:
1. Kuwa na bidii kufuatilia upande chanya wa mtu. Ukiwa "focused" kutafuta madhaifu yake, utayapata mengi sana. Lakini ukiamua kuyatafuta mema yake, utayaona.
Hakuna mtu ambaye ni mbaya tu asiyekuwa na upande mzuri, na hutakutana na binadamu aliye mkamilifu bila madhaifu yoyote.
2. Sifia mema yake
Kwa mfano, hata kama ni mpinzani wako wa kisiasa au kibiashara, anapofanya vizuri na hata kukushinda, sifia mafanikio yake bila kujali kama hatapata taarifa kuwa ulimsifia. Ukikwepa kusifiwa mafanikio yake, unaweza ukaingia kwenye mtego wa kumwonea wivu na kujikuta unaamza kumpigia majungu.
Hizo ni mbinu chache nizijuazo. Naamini kuna wana JF wanaofahamu mbinu nzuri na bora zaidi!
Karibuni!