Jinsi ya kufanya malipo online 2017 (online payments)

Jinsi ya kufanya malipo online 2017 (online payments)

Equity bank

Why Equity?
- Wana flat rate ya makato ya TZS 300 (Mia tatu tu) kwa kila utakachofanya kwa kadi yako
- Wakati kwa benki zingine makato ni asilimia fulani ya muamala utakaofanya. Hivyo ukifaya muamala Mkubwa na makato makubwa.

Andaa TZS 15,000.
Kumbuka hiyo fedha ni yako na waweza kuitoa baada ya kupewa kadi.
Mkuu nimeenda BancABC na Equity kwa ajili ya kupata VISA card maana MasterCard ya CRDB imenichefua. Benki zote wameniahidi kwa uhakika kuwa hakuna charges zozote za kutumia kadi kwa ajili ya malipo online. Hili jambo napata nalo ukakasi mkubwa kuliamini maana najua biashara ya mabenki inapenda makato kuliko kitu chochote.

Niko kwenye hatua za kupata kadi ya Equity, nitaleta mrejesho juu ya hili la makato. Asante.
 
Mwl.RCT

BancABC wanatoa hiyo huduma ya card bila account. Equity ni lazima uwe na account. Hata hivyo BancABC wanataka barua ya utambulisho wa serikali za mitaa ambayo inatia uvivu watu kama mimi.

Equity nimewapenda sana. App yao inasaidia mno. Ni kweli hakuna charges isipokuwa 10,000 ya kupata card. Kinachotokea ni ile currency conversion rate ni kubwa, kama 1USD = 2394. Hapo ndipo wanapopatia mshiko naamini.

CRDB wana slight issue unapoitumia kwa MasterCard kwamba wanalock funds zako na inachukua muda kuachiwa. Wanaweza kukustress sana.
 
Mwl.RCT

Equity hakuna charges per transaction ya Visa card. Ni exchange rate tu iliyosimama kiasi fulani. Pia kwenye app yao unaweza kuangalia mini statement na balance mida wowote bila gharama.
 
Back
Top Bottom