Kwa mujibu wa practical, near death experiences. Meditation ni moja wapo ya njia ya kugundua hivyo vitu
Unajua kama alivyosema Mashaxizo, huwezi ukaelimisha watu kwa kunukuu kitabu ambacho haukiamini mambo yake kufikisha ujumbe wako huku ukidai hicho kitabu hakipo sahihi.
Biblia hiyo hiyo inaelezea tumetoka wapi, kwa nini tuko hapa, na tunakwenda wapi baada ya haya maisha ya hapa duniani. Mleta mada anaongeleaje upande wa pili wa hayo mafundisho ya Biblia?
Nakuomba usubiri ninaleta vitu vyote na ninaviandaa vizuri ili watu waweze kusoma
Huoni kwamba ingekua bora zaidi ukaja moja kwa moja na hizo practical (kama unazo) moja kwa moja badala ya hii njia uliyokuja nao mkuu?
Lete hizo practical tuzipime ila hiyo near death experince hata usijaribu kudanganya watu wote walioexperince hiyo kitu wamekufa hawapo, kwa hiyo sitegemei kupata maelezo sahihi kutoka kwako.
Mkuu umeshaahidi mengi na tofauti ya kuyaelezea huko.
Nahisi maswali mengine ungejibu hapa ili kuepusha mseto kwa hiyo thread nyengine coz naamini hata hiyo thread itazaa vitu vipya vingi tu, so ukiendelea kusema kila swali ujibie thread nyengine nahisi ni kupoteza tu mda na kukwepa maswali.
Biblia ni moja wa vitabu vya tamaduni za kale. Kuna vitabu vingi sana. Sikatazwi kukisoma kwaajili ya kuunganisha habari zangu nilizogundua kutoka kwenye vitabu vya tamaduni zingine. Mtu aliyeandika biblia alikuwa unconscious ndio maana utakuta kitabu hicho hicho kinajipinga chenyewe.
Mambo ambayo yapo kwenye tamaduni zingine na yapo kwenye biblia inabidi tuyafanyie uchunguzi na tujue ukweli wake.
Kwa mfano kuhusu meditation ipo kwenye torah, quruan na kwenye vitabu vya tamaduni za kihindi, kichina. Na tamaduni za kiafrica "misri". Japo kuwa tamaduni zingine hazijatoa vitabu lakini kuna mafundisho ya kitamaduni tunaweza yapata. Hatimaye tumajua ukweli.
Ninadhani hujui unachoongelea hapa. Umeniuliza mimi nimepata wapi hayo maelezo. Hapa nimekueleza kama mimi. Mbona unasahau ulicho uliza? Na sijasema mtu afanye practical ya near death. Kwa huwezi ukaifanya huwa inatokea tu.
Kwa mfano mtu anaweza akaumwa sana na akawa amekufa kabisa na mkajua amekufa hata kwa mda wa 24h baadaye akawa amerudi.
Baadhi ya maswali nimeanza kuyajibu hapa. Kwa kifupi sana.
Kwa mantiki hiyo, kimsingi ni kwamba utakubaliana na majibu au hoja zitakazofuata kutoka kwa wachangiaji watakaokuja na nukuu kutoka vitabu vingine ikiwamo Biblia na Quran (Samahani kama nimekosea kuandika).
Ningeshauri utumie neno kutokuamini kuhusu yaliyomo kwenye Biblia kwa sababu najua hauna uelewa wa kutosha kujua iliandikwa vipi mchakato ulikuaje na ndio maana unasema mwandishi, ila kwa lengo la huu mjadala hayo tuyaweke pembeni tujikite kwenye uzi wako.
Utakubali nukuu za Biblia zinazoelezea tumetoka wapi, kwa nini tuko hapa na tunakwenda wapi baada ya hapa?
Ati sijui nnachokiongea? sasa huyo si hajafa? Kwani tafsiri ya kifo ni nini?
Sijasahau nilichokuuliza, nilikuuliza hayo maelezo ni kwa mujibu wa nani? ukasema practical na near death experiences, kuhusu practicals umesema unajipanga utakuja na somo kamili, nikakwambia usigusie near death experiences! sijaelewa nini hapo?
Ninaposema mtu amekufaa ninamaanisha physical body not functioning. Yaan mwili unakuwa kama maiti. Katika hiyo state hapa duniani katika ulimwemgu wa damu na nyama tunaona huyu mtu kafa. Na vipimo vyote vinaweza onesha huyu mtu kafa. Nilikuwa ninaongelea katika hali hiyo.
Nafikiri hapa kila mtu anajua tunapoongelea mtu amekufa tunajua tunaongelea kitu gani ndio maana nikakwambia hakuna mtu aliyewahi kufa akaja kukupa huo ushahidi wa mfumo mzima wa kifo kuanzia maandalizi yake, kifo chenyewe na nini kinatokea baada ya hapo hayupo.
Imeandikwa......Kipofu kamwe hawezi kumuongoza kipofu mwenzie...kwani wote watatumbukia shimboni.....
Sema kwamba hujawahi kumuona wewe. Lakini unaposema hayupo basi nitakuja kwenye upande wa imani yako kusema mungu hayupo.
[FONT=Arial,Helvetica]"Waacheni wenyewe! Wao ni vipofu, viongozi wa vipofu; na kipofu akimwongoza kipofu, wote wawili hutumbukia shimoni."
Mathayo ​15:14[FONT=Arial,Helvetica][/FONT][FONT=Arial,Helvetica][/FONT]
15:14
[/FONT][FONT=Arial,Helvetica]15:14
[/FONT]
Mkuu nataka kutoa explanation kidogo kuhusu hayo ulioandika
Kwanza sikuwahi kusikia juu ya degree 13
Pili meditation zipo aina nyingi but mainly is insight meditation na outside meditation
Out sight ni Kwa ajili ya visualization na insight Ni Kwa ajili ya kuongeza ufahamu wako. Hapo ndipo ufahamu kuhusu wewe unapokua na pia energy yako inaongezeka
Uchawi Ni Sanaa inayotumia vitu physically kuhamisha energy kutoka sehemu moja kwenda nyingine na hausiani kabisa na meditation
Meditation depends on nothing but meditation but uchawi unadepends on vitu
Naomba turahisishe mambo, lete hizo practical na near death experinces mkuu. Hapo tunaweza kujadili hii topic kwa mapana yake.
Unapoongelea agano jipya ni moja ya vitabu kwenye biblia quality yake ni ya chini sana. Maana kati ya kitabu cha injili na kitabu kingine stori moja unaongelewa tofauti kabisa.
Hebu jaribu kufuatilia kuzaliwa kwa yesu kwenye mathayo na luka ni stori tofauti kabisa.