Jinsi ya kufanya miujiza (Education is power)

Jinsi ya kufanya miujiza (Education is power)

wiki inayoanza kesho. Ninafanya maandalizi yake.

kwanza kabisa nashukuru kwa mafundisho kama haya ambayo yanatuelimisha juu ya misingi ya dunia na ni nini kinaendelea.

Jitahidi mkuu nasi tutoke kwenye giza hili.(reference ni vizuri zaidi kama kwenye uzi wa dunia(

nawakilisha mkuu
 
I believe in meditation but only in the world of God!
Meditation in the world of God brings revelation. This is the grace of God in our souls.
 
Nawasalimia wana JF wote.

Leo nipo hapa kuongelea swala hili la kufanya miujiza na uponyaji.
Kwanza awali ya yote ningepeda kutoa utangulizi kama ifuatavyo.

UTANGULIZI
Sisi binadamu tuko na nguvu kubwa sana ndani yetu. Ni kitendo cha kujua jinsi ya kuitumia. Nguvu tuliyonayo ni nguvu ya kiroho ambayo huwezi ukaiona kwa macho ya damu na nyama lakini unaweza ukaitumia na ikaleta matokeo katika ulimwengu wetu huu.

Nguvu tuliyonayo sisi haijui kuwa hiki chema au kibaya ni mtu tu atakavyo amua kuitumia. Wengine wanaitumia kufanya uchawi lakini wengine wanaitumia kufanya miujiza ya uponyaji. Ni wewe tu utakavyoamua kuitumia hiyo nguvu. Yenyewe ipo.

NAMNA GANI WAWEZA KUIPATA HIYO NGUVU.
Watu wengi sana duniani wamekuwa hawajui hawa watu wanaofanya miujiza au wanaofanya uchawi wanapata wapi nguvu? Je hao watu ni special one? Mimi nina sema hapa ni kwamba tumesahau au tumekataa maarifa na tukakubali kuwa tunasimuliwa na kuwa sio watendaji.
Kwa wale mnaosoma biblia (Hosea 4:6 inasema "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa....."). Inamaana watu wamekosa maarifa ndio maana waenda tu bila kujua nini cha kufanya.

Nguvu yetu ya kufanya makubwa ipo ndani ya nafsi zetu (Consciousness). Au ninaweza kusema sisi watu tunaishi katika ulimwengu wa aina mbili(Ulimwengu wa damu na nyama pia Ulimwengu wa kiroho). Sasa ulimwengu wa kiroho ndio unaguvu na ndio chanzo za nguvu zote. Na ndio uhalisia wetu sisi na ndio reality yetu sisi.

Sasa basi kiwango cha kutumia nguvu au kuwasiliana na nafsi zetu unapungua kadri umri wetu unaposogea. Mtoto anapozaliwa asilimia kubwa sana anakuwa yupo pamoja na nafsi ya ili tatizo lake anakuwa ni mgeni duniani hajui kuongea hajui chochote kilichopo duniani. Kwamaana hiyo hawezi akafikisha ujumbe wowote. Lakini kwakuwa tumekosa maarifa mtoto anapoanza kukua tunaanza kumfundisha vitu vya dunia tu na kusahau asili ya ni nini. Jambo hilo ninamfanya huyo mtoto awe mbali na nafsi yake. Kadri anavyo zidi kukua anazidi kuwa mbali.

Njia yakuweza kuwasiliana na nafsi zetu ni kuhakikisha tunafunga milango ya fahamu ya miili yetu (macho, masikio, mawazo, ngozi nk). Tunapofunga milango hiyo ya fahamu ndio tunakuwa na uwezo wa kuanza kuwasiliana na nafsi zetu.
Kwa wale wasomaji wa biblia: (mathayo 6:6 "
Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.")

Jambo kubwa ninalojaribu kuongea hapa ni kuwaweka sawa waumini wa dini ya kikristo waelewe ni mambo gani yameandikwa kwenye kitabu chao na kwanini hawayafuati.

Njia ili uweze kuwasilina na nafsi yako kwa ufupi ni kufanya meditation (Sina neno zuri la kiswahili). Hii ndio njia bora ya kuweza kuwasilian na nafsi. Kadir unavyozidi kufanya meditation unzidi kupata uwezo mkubwa wa kufanya mambo hapa duniani.
Asilimia zote za watu waliofanikiwa au wanaofanikiwa hapa duniani wanafanya meditation.
Joshua 1:8
This Book of the Law shall not depart from your mouth, but you shall meditate on it day and night, so that you may be careful to do according to all that is written in it. For then you will make your way prosperous, and then you will have good success.
Genesis 24:63 And Isaac went out to meditate in the field toward evening. And he lifted up his eyes and saw, and behold, there were camels coming.
Psalms 119:97 Oh how I love your law! It is my meditation all the day.

Kwa hiyo meditation ndio njia nzuri ya kuweza kuwasilina na nafsi zetu.
Unajua sisi tunauwezo wa uungu ndani yetu? Unajua tunauwezo wakufanya mambo makubwa na dunia yetu ikawa sehemu nzuri ya kuishi? Sisi ni gods na tuna nguvu ya kuitwa gods na ni kweli sisi ni gods Zaburi 82:6 "
Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia."

Utafanya nini ukikaa katika nchi ya watu walio na uwezo na unaona kabisa wanauwezo lakini wanalia shida? Je utawaacha tu hivyo au utawafundisha namna gani walivyo na uwezo? Ni mawili hapo. Ukiwafundisha watajitambua na utakosa watumwa kwa sababu unafurahia wao kuwa watumwa wako. Utawajaza vitu vingi vya ajabu na kuwafanya wakutegemeewewe. Jambo la pili utawafundisha ili waweze kujitambua na kuleta amani katika jamii hiyo kwa kuwa hakutakuwa na tofauti maana watu wanajitambua na wanaelewa wao ni nani.

Je hili jambo la pili linafanyika sasa. La hasha hawataki kabisa wanatufundisha makanisani kuhusu utoaji wa sadaka na kuwa waadilifu ilituweze kwenda mbiguni. Jambo ambalo ni tofauti lkabisa na inavyotakiwa.

Ninayo mengi sana ya kuweza kuongea nanyi rafiki zangu. Lakini hebu niweke kalamu yangu chini na niwaache nanyie muweze kuusoma waraka huu na kuniuliza maswali. Na mimi nitakuwa tayari kujibu inaweza kuwa siyo yote nitajimbu maswali yaliyo ya msingi.

By Annael
EDUCATION IS POWER

Ulizaa uelezewe kwann maajabu mengi yanatikea na mungu yupo kimyaa sio unaropoka kwamba mungu hayupo.et kisa umeona dunia ina maovu
 
mkuu anael heshima kwako nilikuwa naogopa kufanya meditation lakini nikajuliza kama kitu kipo duniani kipo kwa ajiri ya nini ndo nikapata uamuzi wa kutenda jamani nina experience ya wiki moja tu lakini nawathibitishia kwa mpango huu watanzania wenzangu wakiuelewa nchi itatajirika kwa kasi tutapunguza import kwa hali ya juu jamani jaribuni mjione mlivyo sio wa kuchezea
 
Naanza kuamini kwa kuona feedback yako.

Tuambie njia ulizopitia maana mm nimejaribu hii kitu nikaishia kuwa mtu wa kuota ndoto za mfululizo na kutokwa na kajipu kidogo kwenye jicho la kuume lakini hakaumi.
Natanguliza shukrani.
 
ndg mnatupa wakati mgumu tuliolelewa kanisani... iweje niskie leo kua 1.hamna uzima wa milele kwa mtenda mema na kuzimu kwa movu 2. ntaamini vp kua dunia ilidanganyika kwa uongo kiasi hiki ilihali walikuepo wengi wenye busara..3.hizi nguvu naamini hata mungu anatupa lakn za kujitaftia naona cnzr
 
mkuu mimi huwa naanza mida ya saa tano usiku pakiwa tulivu basi huwa nakaa kwenye zuria na kuifunga milango yangu ya faham na kutulia tulii (kataa mawazo yoyote yatayo kuijia concentrate kwenye pumzi) mwanzo nilikuwa natumia karibu dakika 14 lakini kwa sasa huwa ni ndani ya dakika 4,5na 6. utaanza kuona rangi zinabadilika badilika kisha inakuja rangi moja inatulia kisha unakuwa hujioni tena kama umekaa.mkuu nashindwa kueleza yote,ila baada ya kuwa umefanya hayo ndani ya siku mbili tu hutahitaji tena kusikia maneno ya kudhania dhania utapendezwa na mambo yaliyo ya kweli tu (kuona ndio kuamini).utakuwa na uwezo wa kuona jambo haraka na ama kuzuia,kulikwepesha au kulifanyia kazi. nashindwa kueleza yote mkuu. hilo swala la kipele kwakweli sijakutana nalo labda tu kichwa kuuma tena siku za mwanzoni
 
Asante kwa mrejesho...hebu nambie jinsi au jambo ambalo unaamini ni kutokana na med umeweza kulifanyia kazi au kulikwepa kwa maana umeona lina madhara nk....yaan mfano wa kihalisia....tafadhali
 
Mungu sio dicteta maana katupa uhuru wa kuchagua na kupenda chochote ilimradi usimkwaze mwingine.
 
Asante kwa mrejesho...hebu nambie jinsi au jambo ambalo unaamini ni kutokana na med umeweza kulifanyia kazi au kulikwepa kwa maana umeona lina madhara nk....yaan mfano wa kihalisia....tafadhali

sina uwezo wa kueeleza kilakitu na mpaka sasa naona kabisa kuwa nimekosea kuwaelezea watu ambao bado hamjaanza kuona
 
mkuu mimi huwa naanza mida ya saa tano usiku pakiwa tulivu basi huwa nakaa kwenye zuria na kuifunga milango yangu ya faham na kutulia tulii (kataa mawazo yoyote yatayo kuijia concentrate kwenye pumzi) mwanzo nilikuwa natumia karibu dakika 14 lakini kwa sasa huwa ni ndani ya dakika 4,5na 6. utaanza kuona rangi zinabadilika badilika kisha inakuja rangi moja inatulia kisha unakuwa hujioni tena kama umekaa.mkuu nashindwa kueleza yote,ila baada ya kuwa umefanya hayo ndani ya siku mbili tu hutahitaji tena kusikia maneno ya kudhania dhania utapendezwa na mambo yaliyo ya kweli tu (kuona ndio kuamini).utakuwa na uwezo wa kuona jambo haraka na ama kuzuia,kulikwepesha au kulifanyia kazi. nashindwa kueleza yote mkuu. hilo swala la kipele kwakweli sijakutana nalo labda tu kichwa kuuma tena siku za mwanzoni

Dah! Yaani mimi nikianza tu huwa dakika ya kwanza hadi ya pili naishilia usingizini.
Nisaidieni jinsi ya kukwepa usingizi.
 
Dah! Yaani mimi nikianza tu huwa dakika ya kwanza hadi ya pili naishilia usingizini.
Nisaidieni jinsi ya kukwepa usingizi.

Nadhan huwa unafanya kama kitu cha mwisho kabla hujalala....ni vema ukafanya ama baada ya kupumzika au yaan umelala kidogo kisha ukiamka ndo ufanye...lah ufanye asubuhi ile alfajiri....ila usifanye ukiwa umelala kitandani.....jaribu
 
Poa, lakini hata hii ninayofanya kidogo kidogo nimeona mabadiliko.
Mfano kwa sasa nasikia macho yote yanavibret alafu naota ndoto mfululizo kana kwamba mimi nikilala tu naingia ulimwengu wa ndoto mpaka asubuh,
Pia kuna kajipu kidogo kalinitokea nilipoanza kufanya meditation lakini hakaumi.
 
Basi unaenda vyema...karibu utatoboa....mie bado najikongoja....sijatoboa bado....ama kuhusu kijip....sidhan kama vina uhusiano na med. Pengine ni jambo la kitabibu zaidi...maana hakuna ambaye ameshareport kadhia ya aina hyo...au at least kuihusisha na med.
 
Asante kwa ushauri wako mkuu, ngoja nijitahidi.
 
Back
Top Bottom