Jinsi ya kufikisha kuku 1000 wa asili ndani ya muda mfupi

Jinsi ya kufikisha kuku 1000 wa asili ndani ya muda mfupi

farmersdesk

Senior Member
Joined
May 26, 2012
Posts
164
Reaction score
125
JINSI YA KUFIKISHA VIFARANGA 1000 WA KUKU WA ASILI

Habari ndugu zangu wafugaji pole na majukumu ya kila siku katika harakatu za kutafuta mafanikio

Leo nimeona ni vema kushare na nyinyi jinsi mfugaji unavyoweza kufanikiwa kufikisha vifaranga 1000 ndani ya mwaka mmoja na nusu kwa kuanza na kuku wachache tu endapo utaamua kuwa tayari kufikisha lengo Hilo

Unatakiwa kuwa na mitetea 20 ya kienyeji ambayo imefikisha umli wa kutaga na jogoo wawili

Wape Bora chenye virutubisho vyote muhimu kwa kuku na kilicho na mchanganyiko sahihi
Waandalie viota kwaajiri ya kutagia visivyopungua 16

Kwa kuwa umeanza na kuku wenye umli wa kutaga muda sio mrefu wataanza kutaga mayai tafuta mayai yasiyo na mbegu au ambayo hayafai kutotoresha na uweke kila kiota mayai 3 kuku watakapokuwa wanataga kusanya mayai yako katika tray Safi na trei nzur ni zile za box na sio plastic weka sehemu isiyo na joto kubwa na unyevu kumbuka kila siku unapokusanya mayai Unatakiwa uyaandike tarehe ya kutagwa

Ikitokea kuku ameanza kuatamia muachie aatamie Yale mayai ambayo uliyaweka wewe yasiyo na mbegu au yasiyo faa kutotoresha Hadi pale kuku wakifika 12 wanaoatamia

Wawekee mayai Yale uliyokuwa unakusanya na kuyatoa mayai ambayo Yale yasiyofaa kutotoresha

Muda mzuri wa kuwawekea mayai kuku ni wakati wa giza(usiku) unapoweka mayai zigatia yafuatayo
1.mikono yako pakaa majicu
2.weka mayai Yale ambayo hayajazidi siku 14 toka yatagwe ( hiyo utajua mwa kuangulia tarehe ambapo yai limetagwa

Kwa kuwa kuku wanaoatamia ni 12 wawekee kila kuku mayai 12 kwa hao kuku 12 utakuwa I mewapa mayai 144 na kwa hayo mayai 144 Kuna uhakika wa kupata vifaranga zaidi ya 120 baada ya siku 21 hao kuku 12 wataangua vifaranga unachotakiw kukifanya ni kuwanyanganya vifaranga hivyo na kuvitunza wewe katika chumba maarumu ndani ya bruda wawekee chanzo Cha joto maji Safi yenye glucose na chakula maarumu Cha vifaranga(startt) watunze vifaranga hao kwa kuwalisha starter kwa muda wa miezi miwili ndipo uwabadiishie chakula

Zingatia chanjo kama ifuatavyo

✅siku ya 7 Newcastle vaccine

✅siku 14 Gumbolo vaccine

✅siku ya 21 Newcastle vaccine

✅siku ya 28 Gumbolo vaccine

✅ Week ya 5 wape fowlpox vaccine
Baada ya hapo wape dawa ya minyoo

Kumbuka Newcastle vaccine na dawa za minyoo utakuwa unawapa kila baada ya miezi 3

Kwa hapo tutakuwa na vifaranga Zaid ya 120 walio na chanjo Zote .uhimu hiyo tutaita batch ya Kwanza

Kumbuka kwakuwa kuku walinyanganywa vifaranga mapema baada ya kuanguliwa kabla hawajafikisha miezi miwili wale kuku watakuwa wametaga na kutotoa ila utafuata utaratibu was kukusanya mayai kama ilvyokuwa kwa batch ya Kwanza hivyo basi hi batch ya pili tutapata vifaranga zaidi ya 120 kwahiyo batch ya Kwanza na ya pili tutakuwa na vifaranga zaidi ya 240 baada ya miezi nane batch Zote mbili zitaanza kutaga tutapunguza kwa kuuza baadhi ya kuku na kuacha tete 100 na jogoo 10 Hawa tutawatunza watataga na kuatamia tutawaachia mayai kuku 90 waatamie kwa kumuwekea kila kuku mayai 12 kwa kwa idadi hiyo hapo utapata vifaranga nga zaidi ya 1000 itakuwa ni jukumu lako kutunza hao vifaranga Hadi wakuwe li ukija kuuza baada ya miezi sita utakuwa na zaidi ya tsh 10,000000 kama utawauza kwa Bei ya tsh 11000 au zaidi kwa kuku mmoja

👉Kutokana na ukuwaji / utagaji bora itakuongezea kipato.
Ungana na familia ya wafugaji kupitia

1.TELEGRAM tafuta neno "farmers desk" kisha jiunge
2.INSTAGRAM KAMA @farmersdesk_tanzania
 
Uzi mzuri umeandika kiuzoefu japo ujainisha changamoto ufugaji wa kuku una mengi ya kujifunza usiwape tu watu matarajio makubwa sana hasa kwa mtu ambaye hajawahibkbisa kufuga bora aanze na kuku hata nane au kumi tu ili ajifunze kwanza ndo aende huko ulipoelekeza
 
Mkuu zungumzia kuhusu chakula zaidi. Maana hao ni kuku wa kiasili. Kwamba watalishwaje na bajeti ikoje. Maana chakula ni asilimia 70 ya gharama za uendeshaji. Unapokuwa na kuku 1000 wa kiasili unawalishaje na uendeshe vipi huo mradi. Asante.
 
Sina shaka na njia ya utamiaji wa kutumia viota. Ni gharama nafuu kwa maana ya matumizi ya nishati. Na unaweza kutamishia mara 2 au 3 ikiwa utamnyanganya vifaranga na kumtamishia tena.
 
Mkuu Vipi kama issue ya kutotolesha ukaamua kutumia Mashine ya kutotoleshea ili kuongeza uhakika na ufanisi zaidi?
Hii ndo hasa njia ya kusasa na ndani ya muda mfupi tu ukizingatia kanuni bora za ufugaji utakua mtu mwingine
 
Mkuu mayai yakikaa sana percentage za kutotolewa huwa chini ya 40%...yai lisikae chini ya siku 7 ..zamani nilikua nabisha...sasa hv nakisanya mayai kwa siku 5 napeleka incubator..yanatoka zaidi ya 98%..ukiyaweka kwa 14 yanatoka 80% chunguza hilo...! Sio rahisi kama ulivyoandika...unaweza wapa chanjo zote lakini unakuta vifo bado vinatokea....changamoto iko hapo
 
Mkuu mayai yakikaa sana percentage za kutotolewa huwa chini ya 40%...yai lisikae chini ya siku 7 ..zamani nilikua nabisha...sasa hv nakisanya mayai kwa siku 5 napeleka incubator..yanatoka zaidi ya 98%..ukiyaweka kwa 14 yanatoka 80% chunguza hilo...! Sio rahisi kama ulivyoandika...unaweza wapa chanjo zote lakini unakuta vifo bado vinatokea....changamoto iko hapo
Kwenye kila mradi changamoto hazikosi,uwepo wa changamoto haimaanishi kua jambo haliwezekani,la msingi ni kuwa tayari kupambana na changamoto
 
Wana mafua hao fanya mpango uwape tiba mapema ukichelewa wataambukiza wengine.kingine nilichogundua wauza dawa za mifugo wengi sio waaminifu wengi uwa wanatoa chanjo feki
Mhhh sijui kama haya ni mafua nimewapeleka wanaishia kunipa dcp
 
Back
Top Bottom