Njia nyepesi ya kupata kuku 1,000 kwa muda mfupi saana ni kukusanya mayai ya pure kienyeji - lets say tray 50 ambayo kila tray ina mayai 30 - Jumla mayai 1500 - Kila tray ya kienyeji ni Tshs 10,000 mikoani Plus usafirishaji pamoja na packaging fanya 20,000. Jumla ya Pesa yote 1,000,000/=
Mayai yatotoreshe kwenye Incubator with average ya 70% both Hatching & fertility
Kutotoresha tray 1 = 10,000 tray 50 = 500,000.
Baada ya siku 21 utapata vifaranga 70% times 1500 = 1050.
Utawatunza hawa kwa wiki 12, wiki nne za mwanzo ukiwapa chanjo za Gombolo na Newcastle na wiki ya 5 ukichanja ndui.
Chakula na matunzo yao kwa wiki hizo 12 ni 1.5m (Chanjo & Chakula)
Wiki ya 13 - utawahamishia shambani kwako - Free range zone.... hapo utawapatia supporting food tu wakati wa jioni kama Pumba & Mashudu kidogo.
Baada ya wiki ya 20 wataanza kutetea na vijogoo vitaanza kuwika. Wiki ya 24 wataanza kutaga - baadhi ya majogoo utaanza kuuza kwa 20,000.
Hii ndiyo njia nyepesi kuliko ile ya mwanzo ila hii utahitaji kuwa na walau 5m ili uwe confortable - anayehitaji kufanya hii ani PM nitamuunganisha na jamaa.